Huu
ndio msafara wa magari tofauti ya kampuni ya CFAO Motors Group
yakiendeshwa na wateja kutoka kampuni tofauti wakati wa Ride & Drive
yakiwemo Nissan, Benz, VW ‘AMAROK’ na Suzuki yakichanja mbuga kwenye
mabonde na milima kujaribu ubora wake.
Wateja wa Kampuni ya CFA0 Motors wakibadilishana mawazo kuhusiana na ubora wa magari hayo.
It’s Ride & Drive time……Kinamama nao wamo.
Mkurugenzi mpya wa kampuni mpya ya Alliance Motors Bw. Alfred Minja akipozi na gari yake aina Volks Wagon ‘AMAROK’.
Meneja
Bidhaa wa CFAO Motors Tanzania Alex Oelofse (mwenye T-shirt nyekundu)
akijumuika kupooza makoo na wageni waalikwa baada ya zoezi la Ride &
Drive kwa wateja wa kampuni hiyo.
Sales
Representative wa CFAO Motors Magdalena Mpeku (wa pili kulia) na Tender
Manager Bw. Marco Kahabi waki entertain wageni waalikwa baada ya zoezi
la Ride & Drive.
Meneja Masoko mpya wa CFAO Motors Tharaia Ahmed akiteta na mmoja wa wageni waalikwa.
Mkurugenzi Mkuu wa CFAO Motors Uganda Bw. Eric Ruiz akibadilishana mawazo na Meneja Masoko Mpya wa CFAO Motors Tharaia Ahmed.
Meneja
Masoko mpya wa CFAO Motors Tharaia Ahmed akizungumzia tukio la Ride
& Drive kwa wateja wa CFAO Motors kutoka kampuni mbalimbali ambapo
amewahakikisha ubora wa magari yanayoagizwa na kampuni hiyo na jinsi
walivyojidhatiti katika kutoa huduma bora kwa wateja wao.
Kampuni
maarufu ya kuuza na kusambaza magari nchini Tanzania ya CFAO Motors kwa
mara nyingine imewapa fursa wateja wake kuyajaribu kwa kuyaendesha
magari wanayoyauza na gari mpya aina ya Volks Wagon katika viwanja vya
maeneo ya Coco beach.
Wateja
hao kutoka kampuni mbalimbali wamepata nafasi ya kupakia na pia
kuyaendesha magari mapya yanayoingizwa hapa nchini na kampuni hiyo ili
kujua upya na uimara wa magari hayo hivyo kuweza kuchagua magari bora ya
kununua.
Akizungumza
Meneja Masoko wa CFAO Motors Tharaia Ahmed amesema kampuni hiyo
imechagua viwanja hivyo kwa kuwa vina sehemu zenye mawe, miinuko na
barabara korofi ili wateja wao waweze kuthibitisha uimara wa magari
yanayouzwa na kampuni hiyo.
Naye
Mkurugenzi mpya wa kampuni mpya ya Alliance Motors Bw. Alfred Minja
amesema kampuni yake ambayo ni moja ya makampuni ya CFAO Motors Group
imeingiza magari mapya aina ya Volks Wagon yakiwemo ‘Amarok’ ikiwa ni
katika kuwapatia watanzania nafasi ya kuchagua gari bora wanalolipenda
kwa gharama nafuu.
Nao
baadhi ya wateja waliopata nafasi yak u-‘Ride and Drive’ wamesifia
ubora na upya wa magari hayo na kuhimiza watanzania na kampuni mbali
mbli kununua gari hizo.
Dereva
wa siku nyingi na mwanajeshi wa zamani Bw. Issa Swalehe amesema kuanzia
gari kubwa aina ya ‘Benzi Zitros’ ni nzuri hasa katika sehemu
sizizopitika kirahisi na gia zake zinaingia kirahisi kama unavyoendesha
gari ndogo.
Kampuni
ya CFAO Motors ambayo kwa sasa imefungua kampuni ya Alliance Motors
itakayokuwa chini ya Bw. Alfred Minja na kuuza aina tofauti za magari ya
‘Volkswagon’, Nissan, Benzi na mengineyo hufanya tukio kama hilo la
kutoa fursa wa wateja wake ku-‘feel’ ubora wa magari hayo mara tatu kwa
mwaka
No comments:
Post a Comment