JOKETI AENDESHA MNADA WA KONDOO WA AMANI
Mbunifu
wa mitindo nchini, Jokate Mwegelo juzi aliendesha mnada wa Kondoo wa
amani maalum kupinga matukio ya kuhatarisha amani yaliyotokea Zanzibar
hivi karibuni.
Mnada
huo uliandaliwa na kikundi cha wanamichezo cha Taifa Jogging kwa
kushirikiana na wageni wao kutoka Zanzibar wajulikanao kwa jina la
Kitambi Noma.
Mbali
ya kufanya mazoezi, wanamichezo hao walikusanyika kwenye viwanja vya
Mnazi Mmoja chini ya mgeni Rasmi, Kanali Mstaafu na mwenyekiti wa zamani
wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Idd Kipingu ambaye aliwapongeza
waandaaji wa shughuli hiyo kwa kuhamasisha amani nchini.
Kipingu
alisema kuwa amani ndiyo silaha pekee kwa sekta zote pamoja na michezo
kwani kutokuwepo kwake hakuna kitakaochofanyika katika jamii.
Alisema
kuwa kilichofanyika kwa wanamichezo hao ni mfano wa kuigwa na kuwataka
wanamichezo nchini kupigania amani mbali ya kushiriki katika michezo
tofauti.
Katika
Mnada huo, Jokate ambaye kwa sasa ni Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya
ubinifu wa mitindi ya Kidoti aliweza kumuuza kondoo huyo kwa sh. 200,000
kutoka kwa wanamichezo hao.
Mrembo
huyo wa zamani alisema kuwa baada ya kumuuza kondoo huyo, aliondoka na
kundi la Kitambi Noma na kwenda Zanzibar ambako atachinjwa na kuliwa
kama ishara ya kudumisha amani.
“Nimefarijika
sana kwa kushiriki katika mnada huu, mwaliko wangu umetokana na jinsi
gani ninavyojishughulisha katika masuala mbali mbali ya Jamii, mbali ya
mitindo au kama mmoja wa warembo waliofanya vizuri katika mashindano ya
Miss Tanzania,” alisema.
No comments:
Post a Comment