‘Brands of China African Showcase’
2012 Kufanyika Dar es Salaam,
Tanzania julai 1-5 katika maonyesho ya TANTRADE Sabasaba
Maonyesho haya yatachukua ukubwa wa mita 2,600 za mraba, vibanda 150 na exhibitors 110 kutoka mikoa 8 ya China. Maonyesho haya yamegawanya katika makundi manne kulingana na bidhaa ambazo ni; mashine, magari, vifaa vya umeme, vifaa vya nyumbani, vyombo vya mawasiliano, elektroniki, nishati ya jua, bidhaa za matumizi ya kila siku, vifaa vya ujenzi, , kemikali , huduma za afya na bidhaa za kisasa.
Sherehe ya Ufunguzi wa Brands of China African Showcase 2012 itafanyika tarehe 2 Julai 2012, kuanzia saa 9.00 mchana katika viwanja vya maonyesho vya sabasaba na imeandaliwa na Wizara ya Biashara ya Jamhuri ya Watu wa China. Kadika siku tano za maonyesho, Kongamano kati ya kampuni hizi za kiChina na wafanyabiashara wa Afrika utafanyika ili kutoa nafasi ya exhibitors na wanunuzi kuzungumza uso kwa uso, na kubadilishana mawazo na mbinu za kibiashara.
Katika miaka ya hivi karibuni, China imezidi kuboresha uwezo wa kiuchumi, kisayansi na ugunduzi. Mauzo ya nje ya China kwa Afrika imekuwa imara katika ubora, bei na huduma. China imefanya mchango chanya katika kutengeneza bidhaa zinazotimiza mahitaji ya watu wa Afrika, ili kuboresha hali ya maisha ya umma kwa ujumla na jitihada za kuinua uchumi wa ndani na maendeleo ya kijamii
Waonyeshaji bidhaa hao 110 kutoka China watakaofanya maonyesho wamechaguliwa kwa makini sana na mwandaaji wa maonyesho. Makampuni haya yamechaguliwa kutokana na kuwa na uzoefu wa miaka mingi katika mauzo ya nje na pia yanaaminika na kusaidia jamii. Makampuni haya yanajulikana kwa kutoa bidhaa zenye ubora imara zinazotambuliwa na kupokelewa duniani kote. Maonyesho haya yanatoa nafasi kubwa kwa bidhaa za Kichina kuonyeshwa Afrika, na hivyo kuwezesha watu wa Afrika kufahamu vizuri bidhaa za Kichina.
Hii ni nafasi muhimu kwa wanabiashara wa Afrika kufanya ushirikiano wa
kibiashara na makampuni yanayotambulika China ili kupata faida kwa pande zote mbili.
No comments:
Post a Comment