Monday, June 25, 2012

 
Ofisa usalama akiuchukua mwili wa kichanga. 

MTOTO mchanga aliyezaliwa muda mfupi na kutupwa chooni katika eneo la Hosteli ya Lilian Ngoyi katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) cha Morogoro, anadaiwa kufanyiwa hivyo na mwanafunzi wa kike anayesoma hapo.
Tukio hilo la kuhuzunisha, lilitokea Ijumaa iliyopita majira ya saa nne asubuhi kwenye chemba (mifereji ya maji machafu) za hosteli hiyo ambazo zilikuwa zimekwamba kwa kufurika maji baada ya kichanga hicho kushindwa kupenya kwenye shimo la chemba mojawapo.
Mmoja wa wahudumu wa usafi chuoni hapo, Andrew Seluhimbo, ndiye aliyegundua tukio hilo la kuhuzunisha baada ya kugundua kwamba kilichokuwa kimesababisha kuziba kwa mifereji hiyo ni mwili wa mtoto mfu wa kiume.
Hii ni mara ya tatu kwa miili ya vichanga kutupwa katika Manispaa ya Morogoro katika kipindi cha siku nne ambapo mwanzoni ilitokea katika Mto Morogoro eneo la Mji Mpya, ikafuatia huko Kihonda Mizani kabla ya hili la eneo la SUA.

 
Eneo la hosteli ya SUA palipofanyika tukio hilo.
 
 
Shimo ambalo mwili wa kichanga ulipatikana.
 
 
Wanafunzi waliofurika eneo la tukio.

 
Mashuhuda waliokumbwa na simanzi.

 
Ofisa wa polisi akiwa kazini eneo la tukio.

No comments:

Post a Comment