Mshambuliaji
wa timu ya Taifa ya Italy, Mario Balotelli (kulia) akishangilia na
kucheka baada kufunga bao wakati wa mchezo wa nusu Fainali wa kuwania
Kombe la Euro 2012, kati ya timu yake na Ujerumani, uliochezwa jana
usiku.
Italy
waliibuka washindi kwa mabao 2-1, huku mabao yote yakitiwa kimiani na
Balotelli, katika dakika ya 20 na 36 katika kipindi cha kwana, huku bao
la kufutia machozi la Ujerumani likifungwa na Mesut Oezi, kwa mkwaju wa
penati katika dakika ya 91.
Kwa
ushindi huo sasa Italy watashuka dimbani siku ya Jumapili kuwavaa Spain
katika Fainali, baada ya Spain nao kuwaondoa Ureno kwa mikwaju ya
penati 4-2 juzi usiku.
Kipa
wa Ujerumani, Manuel Neue, akijaribu kuilazimisha Nyonga kurudi upande
wa pili ili kuokoa shuti la Mshambuliaji wa Italy, Mario Balotelli
(katikati) bila mafanikio, wakati wa mchezo huo uliochezwa jana usiku.
Mashabiki wa Italy, wakishangilia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ujerumani, baada ya kumalizika kwa mchezo huo jana.
Baada
ya mchezo huo Jiji zima lililipuka kwa shangwe na nderemo ambapo
ilikuwa ni furaha kwa mashabiki wa Italy na kilio kwa mashabiki wa
Ujerumani.
Mashabiki
wa Ujerumani waliokuwa wakifuatilia mchezo huo kupitia Screen nje ya
uwanja huo wakiwa hawaamini kinachotokea ndani ya uwanja huo.
Shabiki
huyu wa Ujerumani akiwa haamini kilichoitokea timu yake baada ya
kupigwa bao 2-1 na mpira kumalizika, ambapo alijikuta akiwa amebakia
peke yake uwanjani hapo huku akiwa amejifunika uso asione
kinachoendelea, wakati mashabiki na wachezaji wa Italy wakishangilia
ushindi wao.
Mashabiki
hawa wa Ujerumani pia walikuwa makini kufuatilia mchezo huo kupitia
Screen katika maeneo ya jiji hilo, lakini nao wakiwa hawaamini
kinachotokea uwanjani.
No comments:
Post a Comment