Wednesday, June 19, 2013

ZITTO KABWE ATAMBA KUMCHAPA RAY KIGOSI RAUNDI YA PILI TU KATIKA TAMASHA LA MATUMAINI



Mbunge wa Kigoma Kaskazini amesema atamchakaza vibaya Ray Kigosi katika raundi ya pili tu kwenye pambano lao la ngumi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.

Pambano hilo limepangwa katika Tamasha la Matumaini litakalofanyika Julai 7 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kweli mimi nimejiandaa vizuri kisaikolojia na mazoezi ni ya kutosha hivyo watu waje waone tu nitakavyomchakaza Ray.

“Kuhusiana na nitashinda katika raundi ya ngapi, jibu langu ni raundi ya pili. Nina hakika hakutakuwa na ubishi, hivyo watu waje waone,” alisema Zitto akionyesha kujiamini.

Pambano jingine litakuwa ni kati ya, mbunge wa Kawe, Chadema,Halima Mdee ambaye atazichapa na mwana Bongo Movie, Jacqueline Wolper.

No comments:

Post a Comment