Saturday, December 29, 2012

TBL YAFANIKISHA UPANDAJI MITI 2600 MWANZA

 Mgeni rasmi katika kampeni ya Mradi wa Upandaji Miti jijini Mwanza, Henry Mongi, akipanda mti  wakati wa kampeni hiyo katika moja ya mitaa ya jiji hilo.Anayeshudia kulia ni Afisa Ubora wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Caroline Muhonoli na wa pili kutoka kulia ni Diwani wa Kata ya Mkuyuni, Fasheni Lugo. Mradi huo umefadhiliwa na Kampuni ya Bia Tanzania.

 Mgeni rasmi katika kampeni ya Mradi wa Upandaji Miti jijini Mwanza, Henry Mongi, akipanda mti  wakati wa kampeni hiyo katika moja ya mitaa ya jiji hilo.Anayeshudia kulia ni Afisa Ubora wa TBL, Caroline Muhonoli na wa pili kutoka kulia ni Diwani wa Kata ya Mkuyuni, Fasheni Lugo.

 Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Steven Kilindo, akifukia udongo kwenye shimo alilopanda mti wakati wa kampeni ya upandaji miti jijini Mwanza mwishoni mwa wiki..Wanaoshuhudia katikati ni Meneja Ubora wa kampuni hiyo, Caroline Muhonoli na nyuma ya Kilindo ni Diwani wa Kata ya Mkuyunim, Lugo Fashen.TBL imetumia zaidi ya milioni 30 kupanda miti 7000 katika mikoa ya Mwanza,Kilimanjaro na Mbeya. Kwa Mkoa wa Mwanza pekee imetumia sh. mil. 10 kupanda miti 2600. 
 Meneja wa TBL Mwanza, Richmondx Raymond akipanda mti katika uzinduzi wa mradi wa upandaji miti jijini Mwanza mwishoni mwa wiki, uliofanywa na kampuni hiyo kwa kupanda miti 2600 kando kando ya barabara za Balewa, Kenyatta, machemba na shule za sekondari Nyamaganana na Nyegezi na Kiwanda cha Bia cha kampuni hiyo.
 Diwani wa Kata ya Mkuyuni, ambaye alimwakilisha Meya wa Jiji la Mwanza, Stanslaus Mabula , Lugo Fasheni akipanda mti katika uzinduzi wa mradi wa upandaji miti  unaotekelezwa kwa msaada wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL ), jijini Mwanza mwishoni mwa wiki. TBL tayari imesaidia kupanda miti 2600 jijini Mwanza.

  Afisa Misitu Jiji la Mwanza, Kaombe Phidelis, akitoa taarifa ya hali ya misitu kwa mgeni rasmi , Henry Mongi wa pili kutoka kushoto,katika uzinduzi wa mradi wa upandaji miti jana.Wa kwanza ni Meneja wa kiwanda cha Bia (TBL) Mwanza, Raymond Richmond na kushoto wa kwanza ni Mkurugenzi wa Uhusiano wa Jamii na Sheria TBL, Steven Kilindo.
Mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Nyegezi na mtumishi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), wakipanda mti kwa pamoja katika shule hiyo, jijini Mwanza juzi. TBL imetumia zaidi ya milioni 30 kupanda miti 7000 katika mikoa ya Mwanza,Kilimanjaro na Mbeya. Kwa Mkoa wa Mwanza pekee imetumia sh. mil. 10 kupanda miti 2600

Catherine ndiye Unique Model wa mwaka 2012

Mwanamitindo bora wa mwaka 2012 Catherine Masumbiga (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Unique Model Photogenic Elizabeth Pertty (kushoto) na Unique Model Talent Vestina Charles mara baada ya kutangazwa kwa mshindi.
Mwanamitindo wa mwaka 2012 Catherine Masumbiga (katikati) amepatikana jana usiku kwenye shindano lililofanyika kwenye Klabu ya New Maisha jijini Dar es Salaam akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa pili Cesilia Michael (kushoto) na mshindi watatu Amina Ayubu.
Washiriki waliongia tano bora.
Washiriki waliongia tano bora.
Majaji wa shindano hilo kutoka kushoto ni Gymkhana Hilal kutoka Paka Wear , Asia Idarous na Martine Kadinda.
Unique Model Talent of the year 2012 Vestina Charles akionyesha uwezowake wa kucheza jukwaani.
Wakitumbuiza mashabiki mapema kabla ya kuingia kuonyesha mavazi ya aina mbalimbali.
Washiriki 12 wa shindano hilo wakiwa wamejipanga tayari kusubiri kutangazwa mshindi.




Na Mwandishi Wetu
FAINALI za shindano la kumsaka mwanamitindo mwenye sifa za kipekee ‘Unique Model’ 2012, limemalizika usiku wa kuamkia leo huku Catherine Masumbigana akishinda taji hilo lililofanyika kwa mara ya kwanza ndani ya ukumbi wa New Maisha Club, Oysterbay, jijini Dar es Salaam.

Shindano hilo lililokuwa likiwaniwa na warembo 12,  ambao waliweza kuonesha mavazi mbalimbali  ikiwemo ya ubunifu, usiku na mengineyo warembo hao  pia waliweza kukonga nyoyo kwa kuonesha uwezo wao wa kuimba na kucheza.

Majaji wa shindano hilo, Gymkhana Hilal, Martin Kadinda na chifu jaji,  Asia Idarous walikuwa kwenye wakati mgumu kuchagua mshindi kutokana na warembo wote kuwa na sifa za juu ambao baadaye walichuja na kubakisha watano kabla ya kubaki watatu.

Chifu Jaji wa shindano hilo, Asia Idarous ndiye alimtaja Catherine Masumbigana kuwa ndiye mshindi na kuufanya ukumbi kulipuka kwa shangwe za wapenzi na mashabiki waliokuwa wamefurika ukumbini huku nafasi ya pili ikienda kwa
Cesilia Michael na Amina Ayubu akiwa wa tatu.
Mbali ya washindi hao, pia taji la  Unique Model Photogenic  lilinyakuliwa na Elizabeth Pertty  huku Unique Model Talent litwaliwa na Vestina Charles.

Awali, akizungumza  muda mfupi kabla ya kuanza fainali hiyo, Mkurugenzi wa Unique Entertainment inayoratibu shindano hilo, Methuselah Magese aliwashukuru wadau mbalimbali  kwa kufanikisha shindano hilo mpaka hapo lilipofikia.

“Nashukuru sana wadhamini wa shindano hili kwa kutuunga mkono mara kwa mara, na tutaendelea kuleta mambo makubwa zaidi katika tasnia ya mitindo na urembo nchini” alisema Magese.

Wahiriki walioshiriki shindano hilo wengine ni Janecy Maluli, Judith Sangu, Darling Godfrey, Lulu Mramba,  Sadory Kendra, Elizabeth Borniface na Zeenarth Habib ambao hawakufaniiwa kunyakua nafasi youyote.
Fainali hizo zilizodhaminiwa na makampuni mbalimbali, zilisindikizwa na burudani kutoka kwa wanamuziki mahiri waliokuwa kivutio kingine ukumbini hapo kwa kila mmoja.

Wadhamini wa fainali hiyo walikuwa Free Media Ltd wachapishaji wa magazeti ya Tanzania Daima na Sayari, Giraffe Ocean View, Kitwe General Traders, Sophanaa Investment, Dtv, Clouds Fm, gazeti la Kiu, Mashujaa Investment Ltd, Blogu za Michuzi, Jiachie, Mtaa kwa Mtaa, Unique Entertainment, Lamada Apartments & Hotel, Fabak Fashions, Genesis Health Center na Yungdon Records, Paka Wear na Mtoko Design.
Hapa ndio TAZARA pa kuondokea.
Ni DMM 88.5 yani Dar mpaka Moro huku 88.5 ikiwa ni namba rasmi kwa kila mwanafamilia wa CLOUDS FM Dar es salaam na Morogoro ambapo CLOUDS FM licha ya kuwa imeandaa party ya kwanza ya aina yake inayoanzia kwenye treni mpaka bush party, kwa mujibu wa TAZARA hii inakua party ya kwanza na ya kipekee kwenye historia ya Tanzania.
Ni bata kwenda, bata kufika na bata kurudi ambapo Watanzania waliovutiwa kujiunga nasi kwa pamoja tunaenjoy kwenye miaka 13 ya kuzaliwa kwa CLOUDS FM lakini pia kusherehekea ujio wa kamanda mpya wa 88.5 Dar es salaam baada ya kumaliza mkataba wa 88.4 kwa kipindi cha miaka 13.
Hii ni sehemu ya kulia chakula kwa wale watakaopenda.
Sehemu ya mebehewa yatakayotumika.
Safari itaanza asubuhi december 28 2012 saa mbili kamili pale TAZARA na tutatumia saa nne njiani tukiwa kwenye treni huku tukipita kwenye vivutio mbalimbali vya Tanzania kama mbuga ya wanyama ya Seluu na kwenye chemchem inayotoa maji ya moto.
Kwenye treni kutakua na huduma ya chakula na vinywaji ambavyo vitakua vinatembezwa na kigari maalum ndani ya treni, mtu yeyote akiwa kwenye behewa lolote anaweza kutembea na kuingia kwenye behewa jingine, vilevile kuna madaktari wameandaliwa kuhusika na huduma ya kwanza iwapo itahitajika, pia pamoja na mambo mengine kuna behewa special ambalo limetengwa kwa watu kupumzika.
Jingine.
.
.
V.I.P
.
.
.

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.