Wednesday, June 19, 2013

Mhe. Andrew Chenge 'ameipa kubwa' serikali kuhusu kukopa pesa na kuishia kusikojulikana!

Mhe Chenge ambae ni mwenyekiti wa kamati ya bunge ya bajeti na mbunge wa bariadi magharibi (CCM) amesema serikali imeelemewa na mzigo wa madeni na faida ya madeni hayo haionekani kwa vile miradi yote ama imekufa au imedumaa kwa ulaji wa pesa hizo za mkopo.

Mhe Chenge ameyasema hayo jana akiwa nje ya ukumbi wa bunge baada ya mkutano wa majadiliano baina ya kamati ya bunge ya bajeti na kamati za miundimbinu, ulinzi na usalama, mambo ya nje, Hesabu za serikali (PAC) na Hesabu za serikali za mtaa (LAAC).

 “NIMEISHAURI SERIKALI KUONDOA FEDHA MAENEO KADHAA NA KUITAKA KUTENGA FEDHA KWA AJILI YA MAENDELEO, LAKINI WAKATI MWINGINE, HATA HIZO FEDHA ZENYEWE HAKUNA KWA KUWA TUNACHO KITEGEMEA HAPA NI PATO LA NDANI.

SASA WATU WALIPE KODI. TABIA YA UKWEPAJI KODI INA SABABISHA SERIKALI KUSHINDWA KUKUSANYA MAPATO YAKE. WATU WANA LALAMIKA HAKUNA HIKI NA HIKI, LAKINI WANANCHI NA TAASISI MBALIMBALI WENYEWE NDIO HAO WANAKWEPA KODI, WANAIBA PESA BILA SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA, SASA TUTAPATA WAPI PESA KWA AJILI YA MAENDELEO?, Chenge alihoji…!!!

SERIKALI INABAKI KUKOPA NA TUKIKOPA PESA HAZIPELEKWI SEHEMU HUSIKA NA ZIKIPELEKWA ZINATUMIKA SI KAMA ILIVYO PANGWA NA KUISHIA KWENYE MATUMBO YA WATU. LAZIMA SERIKALI IWE KALI ILI PESA ZINAZO TOLEWA NA WAHISANI ZIFIKIE MALENGO YALIYO KUSUDIWA.”


    My Take;

    Mzee wa vijisenti, kwa hii kauli yako kwa serikali mimi naona kama unataka kujisafisha tu kwa wananchi, sidhani kama kwa ‘dhambi’ uliyoifanyia Tanzania unapaswa kuongea chochote kinacho husu maslahi ya nchi.

    Mhe Chenge wewe ni mmoja wa viongozi ambao umetia doa kubwa chama changu (CCM), ingekuwa ni busara kukaa pembeni kwa kujiuzuru nyadhifa zako zote badala ya kuanza ‘kuzuga’ kwamba unaijali nchi wakati wewe mwenyewe umekuwa miongoni wa wachumia matumbo.

No comments:

Post a Comment