Thursday, June 20, 2013

AIRTEL YAKABIDHI VIFAA KWA TIMU ZINAZOSHIRIKI AIRTEL RISING STARS

 Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando Akiongea na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano wa TFF wakati wa kukabidhi vifaa vya michezo kwa ajili ya timu zinazoshiriki mashindao ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars mwaka huu
 Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando (kushoto) akikabidhi vifa vya michezo kwa Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF Sunday Kayuni na Mwenyekiti wa DRFA Almasi Kasongo kwa ajili ya timu zinazoshiriki mashindao ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars mwaka huu.hafla hiyo ya makabidhiano yamefanyika ukumbi wa mikutano wa TFF.

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania leo wanakabidhi jezi, vikinga ugoko, mipira na soksi kwa timu za chini ya umri wa miaka 17 zitakazoshiriki kwenye michuano ya Airtel Raising Stars ngazi za mkoa ambayo zinatarajiwa kuanza kutimua vumbia kuanzia Juni 23, 2013.
Mikoa ya kisoka ya Ilala, Temeke na Kinondoni wataingiza timu za wasichana na wavulana kwenye mashindano hayo huku Mwanza, Morogoro na Mbeya wakileta timu za wavulana pekee wakati mikoa ya Tanga, Ruvuma na Kigoma ikishirikisha timu za wasichana tu.

Timu zote zimeonyesha mwitikio na hamasa kubwa kwa kuwa na maandalizi ya awali kwa ajili ya kushindana na kushinda katika michuano hiyo. Michuano ya mikoa itafuatiwa na fainali za taifa ambazo zitapigwa kwenye uwanja wa Kumbu Kumbu ya Karume jijini Dar es Salaam.

Akiongea na waandishi wa habari kwenye makabidhiano ya vifaa yailiyofanyika kwenye ukumbi wa mkutano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) leo, Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando alisema Airtel wanajivunia kuwa sehemu ya programu ya kuendeleza vijana katika soka la Tanzania. 

 “Tunaamini kuwa ushirikiano wetu na timu ya Manchester United pamoja na TFF utachangia maendeleo ya mpira wa miguu Tanzania. Tunaimani vijana wanaweza na ndio maana tunawapa nafasi na kuwasaidia ili waweze kufanya vizuri zaidi kwenye medani ya soka, “ alisema.

Naye Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Sunday Kayuni alisema amefurahishwa na mwitikio ulioonyeshwa na vijana waanaoshiriki kwenye michuano ya Airtel Raising Stars. “Michuano ya Airtel mwaka huu imekuwa na msisimko mkubwa, tunawashukuru Airtel kwa kudhamini michuano hii ambayo inatusaidia kubaini zaidi vipaji vilivyojificha“, alisema Kayuni. 
Programu hii ya Airtel Rising Stars ilimeandaliwa mahsusi kwa vijana wa bara la Afrika, kwa lengo la vijana wanaochipukia katika soka kuonyesha vipaji vyao na kupata nafasi kupata mafanikio katika soka.

Katika kipindi cha miaka miwili iliyopita cha programu hii timu ya Manchester United walituma walimu wa mpira kwa ajili ya kliniki kwa wachezaji katika nchi za Tanzania, South Afrika, Gabon na Kenya kwa wachezaji waliofanya vizuri na kuchaguliwa kwenye michuano hiyo walipata nafasi ya kufundishwa kusakata kandanda.

Ili kuwahamasisha vijana, Airtel imeanzisha mashindano ya kimataifa ambayo mwaka jana yalifanyika kwa mara ya kwanza jijini Nairobi ambapo wavulana na wasichana walipata fursa ya kuonyesha vipaji vyao. Michuano hiyo ilishirikisha wachezaji nyota wa ARS kutoka nchi 14 ambazo kampuni hiyo inafanya biashara.

No comments:

Post a Comment