Monday, July 30, 2012

MWENGE YATWAA KOMBE LA POLISI JAMII WILAYA YA KIPOLISI KINONDONI

Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kinondoni,(SSP)Willbrod Mutafungwa akisom risala mbele ya mgeni rasmi Naibu meya wa manispaa ya Kinondoni Songoro Mnyonge, wakati wa kufunga michezo ya Polisi jamii katika wilaya ya Kipolisi Kinondoni juzi. (Picha na Abdallah Khamis)

Na Abdallah Khamis

TIMU ya Polisi Jamii Mwenge, juzi ilijinyakulia zawadi ya shilingi milioni moja, kikombe pamoja na jezi seti moja baada ya kuibamiza timu ya Polisi jamii ya Mwananyamala Kisiwani kwa bao 1-0, katika fainali ya Polisi Jamaii wilaya ya Kipolisi Kinondoni mchezo uliofanyika katika uwanja wa Biafra.

Katika michuano hiyo iliyoanza julai 9 mwaka huu,mshindi wa pili timu ya Polisi jamii Mwananyamala kisiwani ilijinyakulia sh.500,000, jezi pamoja na Kikombe huku timu ya Polisi jamii Kinondoni muslim ikijipatia zawadi ya Sh.250,000 kwa kuwa washindi wa tatu

Akikabidhi zawadi kwa washindi mgeni rasmi katika fainali hizo Naibu meya wa manispaa ya Kinondoni Songoro Mnyonge, alisema watahakikisha michezo hiyo inakuwa endelevu kwa manispaa kushirikiana na jeshi la polisi pamoja na wadau wengine ili kuwafanya vijana waepukane na uhalifu

Mnyonge alisema malengo ya mashindano yamefikiwa  kwa kiasi kikubwa kwa kuwa vijana wa kata zote katika wilaya ya kipolisi Kinondoni, walipatiwa elimu  ya kuachana na madawa ya kulevya namna ya kutoa taarifa za kuzuia uhalifu pamoja na kuachana na dawa za kulevya katika siku zote za mashindano.

Kwa upande wake mkuu wa polisi wilaya ya Kipolisi Kinondoni Willbrod Mutafungwa alisema timu zilizoshiriki zilikuwqa 14 kutoka katika kata nane za wilaya hiyo.

Mutafungwa ambaye pia ndiye alikuwa mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya michezo hiyo alisema kwa kuwa ni mar ya kwanza kwea michezo hiyo kusimamiwa na wilaya yake Kipolisi watahakikisha mapungufu yaliyojitokeza hayajirudii pindi watakapoandaa michezo hiyo kwa wakati mwingine.

KIDUNDWA ADUNDWA OLIMPIKI

Bondia wa Tanzania, Selemani Kidunda (kulia) akiwa hoi baada ya kudundwa kirahisi kwa pointi 20-7 dhidi ya bondia wa Moldova, Vasilii Belous katika pambano la uzito wa welter (69kg) mzunguko wa 32 kwenye Ukumbi wa ExCeL katika michuano ya Olimpiki ya London 2012.
Bondia wa Tanzania, Selemani Kidunda (kushoto) akishambuliwa na bondia wa Moldova, Vasilii Belous wakati wa pambano lao la uzito wa welter (69kg) mzunguko wa 32 kwenye Ukumbi wa ExCeL katika michuano ya Olimpiki ya London 2012.
Bondia wa Tanzania, Selemani Kidunda (kushoto) akiendelea kuadhibiwa na bondia wa Moldova, Vasilii Belous wakati wa pambano lao la uzito wa welter (69kg) mzunguko wa 32 kwenye Ukumbi wa ExCeL katika michuano ya Olimpiki ya London 2012.

AIRTEL YAENDEA KUSAMBAZA MAWASILIANO KANDA YA ZIWA-MWANZA

 Naibu waziri ofisi ya makamu wa Raisi Mh charles Kitwanga akikata utepe kuashira uzinduzi wa mawasiliano uliojengwa na Airtel nje kidogo ya mkoa wa Mwanza katika wilaya ya Misungwi ili kurahisisha upatikanaji wa huduma zake zote kama intaneti, Airtel Money na kupiga simu vijiji vya  Nyamainza, Buhunda, Ishoke na Seke, wakwanza kulia ni Meneja uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando. hafla ya uzinduzi wa mnara huu wa ilifanyika katika kijiji cha Nyamayinza wilayani Misungwi mwishoni mwa wiki.
 katikati ni Naibu waziri ofisi ya makamu wa Raisi Mh charles Kitwanga akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa kijiji cha Nyamayinza (kulia) na wakati kushoto ni wafanyakazi wa Airtel Tanzania kwenye picha ya pamoja mara baada ya kukata utepe kuashira uzinduzi mnara wa mawasiliano wa  Airtel nje kidogo ya mkoa wa Mwanza katika wilaya ya Misungwi kurahisisha upatikanaji wa huduma zake zote kama intaneti, Airtel Money na kupiga simu vijiji vya  Nyamayinza, Buhunda, Ishoke na Seke, . hafla ya uzinduzi wa mnara huu wa ilifanyika katika kijiji cha Nyamayinza wilayani Misungwi mwishoni mwa wiki
 katika alivalia shati la bluu ni Naibu waziri ofisi ya makamu wa Raisi Mh charles Kitwanga meneja mauzo kanda ya ziwa Galus Mgawe na meneja uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando wakishangilia na wananchi mara baada ya kukata utepe kuashira uzinduzi wa mawasiliano wa  Airtel nje kidogo ya mkoa wa Mwanza katika wilaya ya Misungwi kurahisisha upatikanaji wa huduma zake zote kama intaneti, Airtel Money na kupiga simu vijiji vya  Nyamainza, Buhunda, Ishoke na Seke, hafla ya uzinduzi wa mnara huu wa ilifanyika katika kijiji cha Nyamayinza
wilayani Misungwi mwishoni mwa wiki.
 Meneja wa Airtel Kanda ya Ziwa Bw Galus Mgawe akiongea na wananchi mbele ya Naibu Waziri ofisi ya makamu wa Raisi Charles Kitwanga wakati wa uzinduzi wa mnara wa mawasiliano wa Airtel wilaya ya Misungwi kijiji cha Nyamayinza, mmnara huo wa Airtel kurahisisha upatikanaji wa huduma zake zote kama intaneti, Airtel Money na kupiga simu vijiji vya  Nyamainza, Buhunda, Ishoke na Seke

Mbele ni Naibu waziri Ofisi ya Makamu wa raisi Mh Charles Kitwanga na Meneja Mauzo wa Airtel wakiwa wamejiunga wananchi wakiserebuka ngoma ya asili kufurahia uzinduzi wa mnara wa mawasiliano wa Airtel wilayani Misungwi. mmnara huo wa Airtel kurahisisha upatikanaji wa huduma zake zote kama intaneti, Airtel Money na kupiga simu vijiji vya  Nyamainza, Buhunda, Ishoke na Seke

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Raisi ashauri Wananchi wa nyamayinza, “tumieni fulsa ya mawasiliano haya ya Airtel kwa kuendesha shughuli za masoko”

Mtandao huo wa Airtel kurahisisha upatikanaji wa huduma zake zote kama intaneti, Airtel Money na kupiga simu vijiji vya  Nyamainza, Buhunda, Ishoke na Seke

Mwishoni mwa wiki hii Mwanza Airtel Tanzania imezindua mtambo kabambe wa mawasilano katika mkoa wa kanda ya Ziwa nje kidogo ya mkoa wa Mwanza katika wilaya ya Misungwi ikiwa ni mkakati wa Airtel uliojiwekea katika kuendelea kufikisha huduma zao bora  vijijini Akizindua mnara huo mpya Naibu mwishoni mwa wiki Naibu Waziri Ofisi ya makamu wa Raisi Mhe, Charles Kitwanga (mawe matatu) amesema Maendeleo vijijini yatakuwakwa kasi sana iwapo wananchi watatumia mawasiliano ya simu za mkononi kutafuta masoko ya madini, mifugo au vyakula wanavyozalisha  sehemu mbalimbali Waziri kitwanga alibainisha hayo katika kijiji cha Nyamayinza kata ya Gulumungu wilaya ya Misugwi Mkoani Mwanza wakati akiongea na wananchi na kuzindua mnara wa mawasiliano uliojengwa na kampuni ya Airtel Tanzania.

Alisema “Mawasiliano yanafaida kubwa sana duniani na ndio hufanya maendeleo ya jamii kwenda kwa kasi, hivyo wananchi wa vijiji vyote vinavyoizunguka nyamayinza tumieni fulsa ya kupata mawasiliano haya ya Airtel kwa kuendesha au kuendeleza biashara zenu,pia anzisheni biashara za kutuma na kupokea pesa za Airtel Money  na mtumie mawasiliano haya haya pia kutafuta wateja wakutosha katika bidhaa za kilimo na mifugo mnazozalisha”
Nae Meneja mauzo wa Airtel Kanda ya Ziwa Bw, Galus Mgawe akiongea kwaniaba ya mkurugenzi wa Airtel Tanzania, alisema “Airtel kwa kukamilisha dhamira yetu ya kutoa mawasiliano yenye uhakika kwa mwaka huu tunaanza na kuzindua wa mtambo huu wa mawasiliano hapa wilayani Misungwi utakaowezesha zaidi ya watu 15,000 waliopo vijiji vya Nyamainza, Buhunda, Ishokela, na Seke kuwasiliana na ndugu na jamaa kwa uhakika wakiwa Airtel Kupatikana kwa mtandao huu wa Airtel pia kutasaidia wakazi wa vijiji vyote na jirani  kufurahia huduma zote za Airtel ikiwemo ile ya Airtel Money, kutuma na kupokea sms, pamoja na kufurahia mtandao bora na nafuu wa Intaneti.

Uboreshwaji na uwekaji wa Minara ya mawasiliano ya Airtel katika vijiji unawezeshwa kwa ushirikiano na serikali na mamlaka za mawasiliano nchini kwa kuwa imetuwekea mikakati bora zaidi wakati wa uwekaji wa miundo mbinu hii ya mawasiliano kila mahali Akiongezea kuhusiana na mpango wa kusambaza mtandao unaoendelea alisema Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Bw Jackson Mmbando alisema “kuongezeka kwa mahitaji ya huduma za mawasiliano kutokana na mazingira au kupanuka kwa shughuli za jamii husika ndio yanayotufanya Airtel kuitikia wito na kutanua zaidi wigo wa mtandao wetu kwa eneo husika.

“Huduma ya mawasiliano imekuwa moja kati ya nyenzo muhimu katika kuwezesha shughuli nyingi za kijamii  nchini Tanzania na duniani kote, kupanuka na kufikisha mawasiliano vijijini ni chachu ya kukua kwa uchumi na kuwezesha jamii iliyopo maeneo hayo kupata miundo mbinu mbadala katika shughuli za uzalishaji Airtel bado tunategemea kuendelea kupata ushirikiano wa kutosha kati yetu na serikali  katika kuhakikisha tunafikisha mawasiliano vijijini
kwa kutuwekea mfumo bora wa kulipa kodi na kupata vibali vya kuweka mitambo ya mawasiliano ili kufaidisha jamii.

Airtel ni mtandao bora ulioenea zaidi na kutoa mawasiliano nchini kote kwa kufikisha  mawasiliano ya uhakikia kwa takribani asilinia 85 kwenye maeneo ya miji na vijiji nchini Tanzania.

Mahojiano na Mr. Japhet Kalindu (Afisa Tawala wa Hospitali Ya Igogwe wilayani Rungwe katika mwaka ambao hospitali hiyo inaadhimisha Jubilei ya Almasi (Diamaond Jubilee, miaka 50 ya kuasisiwa).

1.   Tafadhali jitambulishe kwa wasomaji wa Globu ya Jamii kwa kifupi.
Naitwa Mr. Japhet Mwabuluki Kalindu (MPA – HSM, ADHA, Cert. Philosophy) na nimekuwa Afisa Tawala wa Hospitali ya Igogwe kwa miaka 12 sasa- tangu 2000.  

2.   Tupe historia kwa kifupi ya hospitali ya Igogwe:
Ilianza kama Zahanati mwaka 1957. Mwaka 1958 Askofu Van Ooschot aliongea na Masista Wafransiscan wa Uholanzi na Ujerumani kuja Tanzania kejenga na kuendesha Hospitali. Julai 1960 Masista Watatu ambao ni Sr. Tarcisius, Sr. Bonifacio na Sr. Gemma walifika na kuanza kazi mara moja. Uanzishwaji wa huduma za hospitali ulienda sambamba na ombi la wenyeji wa maeneo ya Igogwe kwa sharti kwamba watatoa eneo kujenga Parokia/Kanisa endapo Jimbo litakuwa tayari kuakujenga hospitali. Ndio maana mwaka huo huo 1957 iliponzishwa parokia na huduma za afya zilianzishwa. Kwa haraka sana huduma za afya zilikuwa na watu wengi walifika Igogwe kwa ajili ya kupata huduma. Mwaka 1962 walianza ujenzi rasmi wa hospitali ambayo ilifunguliwa rasmi mwezi Mei 1963. pamoja na ujezi wa hospitali pia walijenga kwa vipindi tofauti zahanati na Kliniki za Mama na Mtoto katika sehemu mbali mbali za Wilaya ya Rungwe na Mbeya vijijini. Katika Wilaya ya Rungwe zahanati zifuatazo zilijengwa na Hospitali ya Igogwe ambazo baadae zilikabidhiwa na Masista kwa serikali: Ibililo, Kipande, Swaya, Ndaga, na Kyimo. Pia walijenga vituo vya chekechea yaani Lubala kilichopo Kijiji cha Lukata, Kiwira na Kanyegele. Vituo vyote hivi vilijengwa ili kusogeza huduma kwa wananchi hasa magonjwa ya akina wakati wa kujifungua.

3.   Hospitali ina uwezo gani?
a.    Rasilimali watu: Madakari wanne (mmoja anasoma surgery), madaktari wasidizi watatu , Afisa Wauguzi Wasaidizi 11, Wauguzi 22, Wateknolojia wanne (wawili maabara, Mfamasia na mmoja Mionzi), Afisa Tawala, Katibu wa Afya, Wahasibu wawili na statistician mmoja na support staff wengi. Kwa ujumla hospitali imeajiri watumishi 120.
b.   Miundombinu: Zipo wodi tano (Wodi ya wanaume na wodi ya wanawake, wodi ya Watoto, wodi ya akina mama, wodi ya Bima, wodi ya magonjwa ya kuambukizwa na wodi ya wagonjwa private. Hospitali ina jumla ya Vitanda 140 vya kulaza.
c.    Throughput: inatibu wagonjwa kati ya 70 hadi 100 kwa siku. Inalaza wagonjwa 5,600 kwa mwaka. Upasuaji kwa mwaka ni 503 kwa mwaka kati ya hizo 182 ni upasuaji wa akina mama wakati wa kujifungua.
d.   Ina uwezo wa kutoa huduma zifuatazo: Huduma za kinga: Huduma ya Uzazi na afya ya Mtoto, Kuzuia Magonjwa ya Maambukizi kama vile UKIMWI nk; Huduma za Tiba: Wagonjwa wa Nje, wagonjwa wa kulazwa na Kliniki ya Wagonjwa wenye maambukizi ya UKIMWI; Promotion and rehabilitation services: Huduma majumbani kwa magonjwa sugu
e.    Uwezo wa hospitali umekuwa ukikuwa katika miaka hamsini ya kuwepo kwake? Kwa vipi? Kama ilivyolezwa hapo awali hospitali imekuwa ikikua kila wakati. Mwaka 1957 kama zahanati, mwaka 1962 hospitali vitanda 40, mwaka 1968 jengo la Watoto Yatima lilikamilika na kuanza kutumika rasmi, miaka ya 1970 ikaongezeka hadi kuwa vitanda 60 pamoja na nyumba za wafanyakazi zilijengwa, jengo la Kliniki likaongezwa mwaka 1974, mwaka 1985 jengo la Maternity na NURU lilikamilika, mwishoni mwa 1990 jengo la kutengenezea maji dawa (Infusions) lilikamilika, Mwaka 1993 jengo la hospitali lilipanuliwa kwa ajili ya maabara ya zamani (sasa chumba cha ultrasound), Upasuaji na mionzi), mwaka 1997 chumba kiliongezwa kwenye wodi ya Watoto kwa ajili ya kitengo cha mionzi ultrasound ambacho kwa sasa ni chumba cha meno, mwaka 1998 nyumba mbili za wafanyakazi zilijengwa zinazoweza kuwa na watumishi 18, mwaka huo huo wa 1998 nyumba wanamokaa Masista wa Jimbo ilikarabatiwa na walianza kuitumia mwishoni mwa 1998, mwaka 2002 nyumba mbili za madaktari zilikamilika, mwaka 2003 jengo jipya la wodi ya magonjwa ya kuambukizwa lilijengwa na kukarabatiwa mwaka 2008, mwaka huo huo wa 2003 kitengo cha Tiba kwa wagonjwa wa UKIMWI kilikarabatiwa, mwaka 2006 jengo jipya la maabara ya kisasa lilikamilika na kuanza kutumiaka, ukarabati wa mara kwa mara umekuwa ukiendelea mwaka hadi mwaka.

4.   Catchment area: Inatibu wagonjwa kutoka katika Tarafa ya Ukukwe Wilayani Rungwe isipokuwa kata ya Malindo. Lakini mara kwa mara tunapata wagonjwa kutoka kote Mkpani Rungwe.

5.   Dhima ya hospitali: Kuendeleza uponyaji alioufanya Kristu katika kuendeleza na kutoa huduma bora za afya kwa wote zaidi sana wale wanaohitaji zaidi msaada wetu.
Hospitali ya Igogwe imekuwa ikitoa mchango mkubwa sana katika Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe. Inahudumia zaidi ya watu 150,000 wanaotoka katika eneo rasmi lililotengwa na Wilaya kwa ajili ya kuhudumiwa na hospitali ya Igogwe kati ya watu 400,000 ndani ya wilaya ya Rungwe. Ni hospitali mojawapo kati ya hospitali tatu zilizopo Rungwe (Itete na Tukuyu). Hata hivyo hospitali inahudumia watu wengi kutoka maeneo mengine ya Wilaya ya Rungwe. Pia Hospitali inatoa huduma zilizo bora kwa wananchi wote ndani ya Mkoa wa Mbeya. Wagonjwa wanaohudumiwa hapa wanatoka wilaya zote za Mkoa wa Mbeya: Mbeya vijijini, Ileje, Kyela, Mbeya Jiji, Mbarali, Mbozi na Chunya. Akina Mama wengi wajawazito wanapenda kujifungulia hapa hasa kutoka wilaya za Mbeya (JIJI na Vijijini), Ileje, Kyela na wachache kutoka Mbarali. Pia wapo wanaohudumia kutoka mikoa ya jirani Iringa, Njomba na Rukwa, na kutoka nje ya nchi kama Malawi na Zambia. Pengo gani amabalo linajazwa na hospitali hii katika utoaji huduma za afya wilayani Rungwe,
Kituo cha Watoto Yatima kinatoa huduma kwa wakazi wote wa Mkoa wa Mbeya na mikoa ya Jirani. Kimekuwa mfano wa kuigwa kwa huduma bora zinasozaidia sana kuwakuza watoto kiafya na malezi bora. Na juzi tu kituo kilingia mkataba kuwahudumia watoto wadogo ambao wamepatikana na wakimbizi wakati taratibu zingine za sheria zinaendelea.

6.   Hospitali ya Igogwe inamiliki ungo wa mawasiliano kwa ajili ya shughuli za mawasilaino ya aina gani hasa?
Ungo unaturahisishia mawasiliano ya aina nyingi. Mawasiliano ya internet kama vile kutuma na kupokea barua pepe, kusoma makala  za fani aina mbalimbali, pia telemedicine. Tulikuwa tunawasiliana na wenzetu wa KCMC kupitia MEMS lakini kwa sasa yamesimama kidogo kwa sababu yule aliyefundishwa hayupo. Telemedecine ni muhimu sana kwa maendeleo ya hospitali katika kutoa huduma iliyobora kwani daktari wa Igogwe aweza kuwasiliana moja kwa moja na daktari wa mahali pengine. Pia hospitali ina mpango wa kuanzisha mawasiliano ambayo daktari wa hapa aweza kuwasiliana na daktari bingwa wa mahali popote duniani na wakashaurinana namna nzuri ya kumhudumia mgonjwa ikiwa ni upasuaji au namna yoyote ile.

7.   Mkoa wa Mbeya una huduma za ‘physiotherapy’ (mama cheza na baba cheza) kwenye hospitali ya Rufaa tu iliyopo jijini Mbeya. Mpango wa hospitali ni kuanzisha huduma hii muhim ili kuwasaidia wananchi wanaohitaji huduma hii wanaotoka maeneo ya wilaya za Rungwe, Kyela, Mbeya Vijini na Ileje.

8.   Changamoto za Hospitali ya Igogwe?
ü  Upatikanaji wa raslimali za kuendeshea hospitali umekuwa mgumu sana: Raslimali watu wachache. Hasa wataalam wa fani mbalimbali (waganga, wauguzi na wafamasia). Imekuwa vigumu kuwaretain watumishi kwani watumishi tulionao wanalipwa kama wale wa serikalini lakini utakuta hapa wanafanya kazi zaidi hivyo wengi hupenda kwenda kufanya kazi serikalini ili wakapumzike kidogo
ü  Raslimali fedha kwa ajili ya kulipa mshahara, kulipa NSSF, kununua dawa, na kufanya shughuliza maendeleo za hospitali
ü  Miundo mbinu imeanza kuchakaa kwani fedha zimekuwa hapa
ü  Kupata kwa wakati fedha za ruzuku kutoka wizarani. Lakini pia wachache ndio wameingizwa kwenye payroll ya serikali hivyo kuipa mzigo mzito hospitali kulipa huduma
ü  Huduma bure kwa mama na mtoto chini ya mika mitano na hali fedha hazitengwi kutoka serikali kuu kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli hii kama ilivyoelekezwa kwenye sera. Sera huduma bure, utekelezaji hauonyeshi wapi fungu la fedha kutekeleza hayo
ü  Upatikanaji wa vifaa tiba vya kisasa

9.   Mipango ya hospitali katila miaka 5, 10 au 50 ijayo?
Hospitali katika miaka mitano ijayo imepanga kufanya yafuatayo:

ü  Kuboresha na kuimarisha raslimali watu – kuwalipa vizuri pale inapowezekana na kuwaendeleza
ü  Kutoa huduma bora za afya kwa watu wote hasa akina mama wajawazito na watoto
ü  Kujenga jengo la mionzi (X _Ray)
ü  Kukarabati theatre
ü  Kununua ambulance kufanikisha huduma za rufaa hasa kwa mama mjamzito
ü  Kujenga jengo la maiti
ü  Kuandika maandiko kwa ajili ya kununua dawa na vifaa tiba
ü  Kujenga chuo cha waganga
ü  Kujenga nyumba ya masista
ü  Kujenga nyumba za watumishi
ü  Kukarabati jengo la Watoto Yatima
ü  Kukarabati hospitali (wodi na OPD)
ü  Kukarabati nyumba za watumishi
ü  Kujenga jengo la maiti

10.        Ndoto yako: kama ungetokea muujiza wa pesa na rasilimali takribani 100 milioni   zingepatikana ghafla ungezifanyia nini katika Hospitali ya Igogwe leo?
Mungu bariki kama zingefikia 120 millioni ningenunua mara moja gari la kubebea wagonjwa. Kwa 100,000,000 cha kwanza ni kukarabati hospitali na kituo cha watoto yatima kwani majengo yote ya hospitali yamepakwa kwa rangi ya mafuta ambayo ni hatari kama kukitokea janga la moto. Hivyo kubadilisha rangi na kuweka marumalu kwa ajili ya usafi wa hospitali na kituo cha watoto yatima (Tshs 55,000,000), kujenga jengo la mortuary 35,000,000 na kukarabati baadhi ya nyumba za watumishi (10,000,000)

11.       Mipango ya kusheherkea Jubilei ya miaka 50: Hospitali inapanga kufanya nini, lini, wapi kwa nini?
Katika kuadhimisha miaka 50 ya uwepo wa Hospitali ya Igogwe, Hospitali imepanga kuyatekeleza yafuatayo kwa uwezo wa Mungu na msaada kutoka kwa wadau mbalimbali wenye nia nzuri na hospitali:
ü  Kukarabati Hospitali wodi na OPD Tshs 30,000,000/=
ü  Kukarabati Jengo la Watoto Yatima Tshs 25,000,000/=
ü  Kujenga Jengo la Idara ya Mionzi Tshs 72,000,000/=
ü  Kukarabati Chumba cha Upasuaji Tshs 26,500,000/=
ü  Kujenga jengo la maiti (mortuary) Tshs 35,000,000/=
ü  Kukarabati nyumba za watumishi Tshs 41,400,000/=
ü  Kununua gari la kubebea wagonjwa Tshs 120,000,000/=
ü  Adhimisho la Jubilei Tshs 22,550,000/=

12.        Unauaonaje mgogoro na mgomo wa madaktari na wauguzi uliyotokea hivi karibuni nchini?
Hali tukijua madaktari wanaendeleza kazi ya uumbaji na uponyaji aliyoifanya Mungu hapa duniani na pia wanaendeleza uponyaji wa Kristu, kwa namna yoyote ile mgomo wa madaktari haukuwa mzuri kwa pande zote mbili serikali na madaktari wenyewe kwani watu wengi wameathirika na mgomo huo, kupata ulemavu wa kudumu au hata kupoteza maisha. Yafaa pande mbili zikae na kukubaliana ili kulinusuru Taifa. Wagonjwa wengi waliokuwa wamelazwa hospitali kama Mbeya Rufaa walikuja kupata huduma hapa. Japokuwa pato la hospitali huongezeka kwa kuwahudumia wagonjwa lakini pia mzigo uliongezeka sana kwani madaktari na wauguzi waliweza kufanya kazi masaa hata ya ziada ili kuhakikisha wagonjwa wote waliofika wanahudumiwa.

13.       Unatoa wito gani katika kusheherekea Jubilei hii: kwa nani, wito gani, wa aina gani, lini, kwa nini, kwa namna gani?
Naomba Mungu atujalie sote salama katika maisha yetu. Sote tuwe na afya nzuri ili tuweze kutekeleza majukumu yetu vizuri. Naomba Mungu mipango yote iliyo mbele yetu iweze kufanikiwa tena sana na ikiwezekana tupate zaidi ya pale tulipotegemea kwani Hospitali ina mipango mingi lakini kwa ufinyu wa bajeti tunashindwa. Wito wangu kwa wadau wote wote tunashirikiana ili kufanikisha tukio hili kwa ustawi wa watu wetu na taifa kwa ujumla. Kila mmoja achukulie umuhimu wa pekee katika kufanikisha adhimisho hili la Jubilei. Na wale watakaotuunga mkono nawahakikishia kile watakachochangia kitafanya tu yale yaliyopangwa na Kamati na kupata baraka za Baba Askofu Chengula na si vinginevyo. Kushuhudia hili shughuli zote zitakazofanyika zitakuwa wazi kwa wadau wote ili wote waliochangia wajinue kuwa fedha zao ziliingia katika mikono mizuri na kutumika kama ilivyokusudiwa.
Akaunti ya Hospitali kwa ajili ya kuchangia walio mbali na wenye mapenzi mema:

IGOGWE HOSPITAL – JUBILEE AT NBC TUKUYU BRANCH A/C = 038201127120

IGOGWE HOSPITAL – AT NMB TUKUYU BRANCH 1/C = 61403500064

Vuta Mkwanja TVC with Diamond Platinum

Diamond Arudisha Majeshi kwa Mpenzi wake!!!!!!!

GERRY TEGETE, NGASA WASHEREHEKEA UBINGWA PAMOJA NDANI YA WHITE HOUSE KIMARA KOROGWE.

Mwanamuziki nguli wa Bendi ya Mashujaa Musica Chaz Baba akiimba kwa furaha kubwa ndani ya Ukumbi wa White House Kimara Korogwe usiku wa kuamkia leo. Kutoka kulia Chaz Baba, Mrisho Ngasa Mchezaji wa Azam na Gerry Tegete Mchezaji wa Yanga wakiwa ndani ya viunga vya White House Kimara Korogwe jana baada ya kutoka kwenye Mechi kali baina ya timu zao, ya kombe la Kagame ambayo Yanga waliibuka mabingwa kwa mabao 2 kwa bila. 
Kulia Gerry Tegete akishoo luv na Mchezaji mwenzake Mrisho Ngassa anayechezea club ya Azam.
 
Mrisho Ngassa na Chaz Baba wakifurahia kwa pamoja Ushindi waYanga, Mrisho ngassa ni Mshambuliaji mahiri wa Club ya Azam.
 
Rapa maarufu wa Bendi ya Mashujaa Fagasoni akiimba ndani ya ukumbi wa White house Kimara Korogwe.
 

Rais Kikwete afutari na viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini ikulu jijini Dar es Salaam

 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na viongozi na wawakilishi wa madhehebu mbalimbali ya dini walioshiriki katika futari aliyoiandaa kwa viongozi wa dini ikulu jijini Dar es Salaam leo jioni(picha na Freddy Maro)
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na viongozi na wawakilishi wa madhehebu mbalimbali ya dini walioshiriki katika futari aliyoiandaa kwa viongozi wa dini ikulu jijini Dar es Salaam leo jioni(picha na Freddy Maro)
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na viongozi na wawakilishi wa madhehebu mbalimbali ya dini walioshiriki katika futari aliyoiandaa kwa viongozi wa dini ikulu jijini Dar es Salaam leo jioni(picha na Freddy Maro)

MASAI CAMP ARUSHA YAZINDULIWA UPYA

 Wageni maalum katika uzinduzi huo Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Teddy Mapunda (kushoto) na timu yake wakipata burudani na vyakula vya aina mbalimbali wakati wa uzinduzi wa
Klabu ya  MASAI CAMP ya jijini Arusha ambayo  itakuwa ikitoa vionjo tofauti kwa vyakula na burudani za aina mbalimbali pamoja na vinywaji vya kila namna kwa wageni watakao kuwa wakitembelea kituo hicho cha maraha kutwa nzima.
 
  Wageni kutoka nje ya nchi ambao wapo jijini Arusha kwa shughuli za utalii, masomo na kazi za kujitolea wakifuatilia burudani kutoka kundi hilo la Gotagious Danceteam Africa lililokuwa likip[oromosha burudani kali.
 
Burudani ya vijana hawa ilikuwa ni ya nguvu na yakuvutia. 
 
  furaha ya watazamaji haikuweza kufichika...
 
  Burudani ya Disco iliporomoshwa na mkali huyu kutoka majuu
 
 Wadau wa Masai Camp ya mjiji Arusha wakilamba picha ya pamoja usiku wa jana wakati wakitambulisha upya kiota hichi cha maraha.
 
  Teddy Mapunda 'Aunt T' akishow love na mmoja wa waendeshaji wa Masai Camp
 
Burudani iliachiwa mpaka majogoo na watu waliruka majoka ya hatari.....ilikuwa ni raha tupu.

Linex - Aifola (Official Video)

Sunday, July 29, 2012

EBSS YAENDELEA KUCHANA MBUGA NA WEEKEND HII ILIKUA MKOANI TANGA

DIGNAH MBETELA KUTOKEA DODOMA AKIWA MBELE YA MAJAJI KWA MARANYINGINE KUJARIBU KUPATA NAFASI YA KWENDA DAR ES SALAAM.
Usaili wa Zantel Epiq Bong Star Search, umekamilika mkoani Tanga katika ukumbi wa klabu ya La Casa Chica. Mwamko wa washiriki umekuwa kama ulivyotegemewa ambapo zaidi ya washiriki 300 walikuwa wamesha jisajiri kwanza kwa ajiri ya kufanya usaili siku ya leo. Washiriki wengi walioshindwa kupata nafasi katika mikoa usaili uliopitia wamejitokeza katika mkoa wa Tanga kitu ambacho kimeongeza ushindani kwa washiriki kutokea eneo hili la Tanga.
WASHIRIKI WAKIWA NA HAMASA YA KUWAONA MAJAJI


MSHEWA MUSSA AKIWAKIRISHA TENA KWA MARA NYINGINE BAADA YA KUKOSA NAFASI MKOANI ARUSHA.

WASHIRIKI WAKIWA KATIKA MSTARI WAKISUBIRI KUINGIA KUFANYA USAILI
FAISAL JAFARI KUTOKEA TANGA AKISUBIRIA USAILI