Wednesday, January 30, 2013

DIAMOND AMKAMATA MMOJA WA WACHAWI WAKE

                           
 Zikiwa zimepita siku 29 tangu alipofanyiwa vurugu za kutosha, wakati wa show yake aliyokuwa akiifanya ndani ya Maisha Club, na kusababisha watu kadhaa kuumia, chupwa kurushwa na mayai viza kurushwa, huku akiachwa bila ya cheni, saa wala miwani alizokuwa amezivaa na kuambulia boooooo kibao, siku ya jumamosi Diamond alipokuwa akielekea Kigamboni kwenye show aliyokuwa anaifanya huko akiwa na msanii Z Anto, alifanikiwa kumkamata mmoja wa walioanzisha vurugu hizo, akiwa ndani ya pantoni nae akielekea kigamboni

KUTOKA BUNGENI DODOMA LEO

Naibu waziri wa Nishati na Madini George Simbachawene akijibu hoja mbalimbali za wizara yake
Baadhi wa wabunge wakielekea katika ukumbi wa mkutano Bungeni mjini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya ya Rais (mahusiano na Uratibu), Stephen Wasira (kulia) akisalimiana na Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema.
Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe(kuli) Godbless Lema (ars mjini- katikati) na Vicent Nyerere- Musoma Mjini
Mwingulu Nchemba (Singida)-kulia, Joseph Selasini (Rombo- katikati),a Mosses Machali (NCCR-Mageuzi- Kigoma mjini) katika viwanja vya bunge.


 Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiongea na waandishi wa habari. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani, Emmanuel Nchimbi

RAIS JOSEPH KABILA WA DRC ATUA DAR LEO KWA ZIARA YA SIKU MOJA

Ndege iliyomchukua Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ikiwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam  mchana wa leo Januari 30, 2013
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimjpokea Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) alipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam mchana wa leo Januari 30, 2013
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimjpokea Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) alipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam mchana wa leo Januari 30, 2013

Tuesday, January 29, 2013

WAJASIRIAMALI WALIVYONUFAIKA NA SAFARI LAGER WEZESHWA

 Mjasiriamali Elizabeth Chami (26), akioka keki kwenye jiko la kisasa alilozawadiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia promosheni ya Safari Lager Wezeshwa 2012, kwenye karakana yake iliyopo Tabata Mawenzi, Dar es Salaam.
 Mfanyakazi wa karakana hiyo, Happiness akiandaa keki kwenye jiko hilo la kisasa.
 Mfanyakazi wa Kiwanda cha kutangeneza Shampoo  cha L &amp, V Intergrated Firm, kilichopo Mikocheni, Dar es Salaam, Hashim Hussein, akipaki katoni za bidhaa hiyo. Kiwanda hicho kilisaidiwa chupa 15,000 baada ya mmiliki wa kiwanda hicho Valerian Luzangi (hayupo pichani) kuwa mmoja wa washindi wa promosheni  ya Safari Lager Wezeshwa 2012.
 Luzangi, akisaidia kupanga vizuri chupa zilizojazwa shampoo. Kushoto ni mfanyakazi wa kiwanda hicho Stahabu Mwinyi.
 Mjasiriamali Valerian Luzangi (38), kulia, akipanga vizuri katoni za shampoo anazozalisha katika kiwanda chake cha L & V Intergrated Firm, kilichopo Mikocheni, Dar es Salaam juzi. Luzangi alisaidiwa chupa 15,000 baada ya kuwa mmoja wa washindi wa promosheni  ya Safari Lager Wezeshwa 2012, Kushoto ni mfanyakazi wake, Hashim Hussein. 
 Wajasiriamali Innocent Mberwa (kulia) na Gosbert Mugisha, wakiweka sawa mfumo wa umwagiliaji katika moja ya mashamba  ya zao la matikiti maji ya Kampuni yao ya  Tin Wax eneo la Minondo, Kata ya Somangila, Kigamboni, Dar es Salaam juzi. Kampuni hiyo ilizawadiwa mfumo huo baada ya kushinda promosheni  ya Safari Lager Wezeshwa 2012. 
 Mjasiriamali Innocent Mberwa akionesha tikiti maji katika moja ya mashamba ya Kampuni yao ya  Tin Wax yaliyopo eneo la Minondo, Kata ya Somangila, Kigamboni, Dar es Salaam juzi. Kampuni hiyo ilizawadiwa mfumo wa maji wa umwagiliaji baada ya kushinda promosheni  ya Safari Lager Wezeshwa 2012,
Wajasiriamali Innocent Mberwa (kulia) na Gosbert Mugisha wakiwa sawa mfumo wa umwagiliaji katika moja ya mashamba  zao la matikiti maji ya Kampuni yao ya  Tin Wax eneo la Minondo, Kata ya Somangila, Kigamboni, Dar es Salaam juzi. Kampuni hiyo ilizawadiwa mfumo huo baada ya kushinda promosheni  ya Safari Lager Wezeshwa 2012,
Baadhi ya vitunguu vinavyozalishwa katika shamba hilo.

MFUMO WA DIGITAL UMENIVUNJA NGUVU NA KUNIPUNGUZA SPEED

Licha ya kufanya karakati za kutengeneza video mpya ya wimbo wake "yatakwisha" aliyofanya na lina, ambayo mpaka hivi sasa ipo katika hatua za mwisho, Ben pol amesema mfumo wa digital umemvunja nguvu na kumpunguzia kasi, kwasababu kumekuwa na mvurugano kwenye televisheni zetu na hivyo kuwa sio kipindi kizuri cha kufanya biashara, maana watu wengi kama asilimia 85 hawana access ya kuona video kwa ufasaha, kwahiyo anaweza akaipoteza tu video hiyo.
 
"nafikiri kuanzia march au april ndio nitatoa maana naamini vitu vitakua vimenyooka, kiujumla nimepanga nitoe video mbili kwa mwaka huu, moja nitoe mwanzoni na nyingine iwe juu ya mwezi wa sita, either wa nane au wa tisa." amesema Ben Pol.

TIMBERLAKE NA JAY Z WAINGIA MTAANI KUSHOOT "SUIT AND TIE

suit-and-tie-1
Ijumaa ya wiki iliyopita, katika mitaa ya LA, mida ya mchana, walionekana wakishoot video ya wimbo wao mpya Suit and Tie, huku wakionekana tayari kuimudu hali ya hewa ambapo kulikua na mvua za hapa na pale.(under umbrella). collable lao saa hii limepanda mpaka nafasi ya 4 katika billboard chart top 100, kutoka nafasi ya 84 wiki yake ya kwanza. album inayofata ya Timberlake 20/20 experience itakua ni album yake ya kwanza ndani ya miaka saba, ambapo mara ya mwisho aliachia mwaka 2006.

RICKY ROSS ANUSURIKA KIFO BAADA YA KURUSHIWA RISASI

 Msanii Ricky Ross, leo asubuhi amenusurika kifo baada ya mtu mmoja aliekua na silaha kurusha risasi kadhaa kwenye gari aina ya Rolls Roys aliyokuwemo Ross na dem mmoja Ft. Lauderdale, Florida na kusababisha kugonga nyumba akijaribu kuongeza mwendo.
Ross hakupatwa na risasi hata moja wakati wa tukio hilo wala dem aliekuwa nae ndani ya gari hilo.
Ripoti zinadai risasi kibao zilirushwa kuelekea kwenye gari hilo mda wa saa kumi na moja asubuhi, na hakuna hata moja iliyoshoot kwenye Rolls.
polisi wanasema gari lingine lilisimama karibu na gari la Ross na mtu mmoja aliekuwa kwenye gari hilo kuanza kurusha risasi kwenye gari la Ross
 Mpaka sasa hakuna alietuhumiwa, kugundulika wala kushikiliwa juu ya tukio hilo

FRANK OCEAN ANATAKA KUFUNGUA MASHTAKA DHIDI YA CHRIS BROWN

frank_ocean_paparazzi 
Jana dunia iligubikwa na habari zilizozunguka kila kona ya mitandao ya jamii, zikielezea ugomvi  uliotekea siku ya jana, kati ya Chris Brown na msanii mwenzake wa r&b Frank Ocean, kwa kile kinachodaiwa ni kugombania parking ya gari katika studio za westlake.
stori iliyokuwepo ni kuwa, Frank alikasirika baada ya Chris Brown kupaki katika parking yake, na Chris Brown alizuiwa kutoka baada ya kumblock kwa nyuma, lakini ugomvi ulianza baada ya Chris brown kujaribu kushikana mkono na Frank Ocean.
chris_brown_angry
sasa the New York Post wameripot kuwa na habari isiyo nzuri baada ya Sheriff wa LA  kutoa repot ya kuwa, Frank anadhumuni la kufungua mashtaka kwa kumpiga ngumi na kuanzisha ugomvi nje ya studio za westlake, west Hollywood, jumapili asubuhi
Polisi wanataka kuongea na Brown ambae bado yupo brobation kwa kipigo alichompa Rihanna mwaka 2009.

USHAHIDI WA PICHA TATU ZA LULU BAADA YA DHAMANA KUKAMILIKA, MUDA MFUPI KABLA YA KUINGIA URAIANI

Lulu na mama yake mzazi wakilia baada ya kukutana nje ya Mahakama, Lulu ameachiwa huru na Mahakama january 29,2013 mchana, pembeni ni mwigizaji Dr. Cheni ambaye amekua karibu na familia ya Lulu kwa muda mrefu sana.
Lulu akiingia kwenye gari.
Machozi ya furaha.

ALICHOSEMA WAZIRI MKUU MTWARA NDIO HIKI

Polisi wakati wa fujo za Mtwara.

Taarifa ikufikie kwamba Waziri mkuu Mizengo Pinda amefanikiwa kutuliza jazba za wakazi wa Mkoa wa Mtwara kwa kuwaeleza kuwa kiwanda cha kusindika gesi ghafi kitajengwa kijijini Madimba mkoani humo ili mabaki yatokanayo na gesi hiyo yatumike kuvutia uwekezaji wa viwanda, hii ikiwa ni kauli tofauti na ya madai ya wakazi hao ambao hasira zao zilichangiwa na taarifa kwamba kiwanda hicho kingejengwa Dar es salaam.

Kwenye mkutano wa majumuisho uliofanyika january 29 2013 Waziri mkuu baada ya kusikiliza madai ya wananchi hao kwa siku mbili mfululizo, amesema hakuna tone la gesi ghafi itakayosafirishwa kwa njia ya bomba.

Namkariri akisema “Imani yangu ni kwamba maelezo yametosheleza, mtakua na kiwanda chenu cha kusindika, mtakua na kiwanda cha kusafisha, mtakua na hayo matawi kadhaa kwa ajili ya uzalishaji wa umeme kwa ajili ya usindikaji wa viwanda”
Mwanzoni madai ya wakazi wa Mtwara yalikua ni kupinga usafirishaji wa gesi ghafi mpaka Dar es salaam wakieleza kwamba huo mpango utafukuza wawekezaji wa viwanda Mtwara ambao ungechochewa na upatikanaji wa malighafi baada ya kusafishwa kwa gesi.
Jengo la Mahakama lililotelekezwa.

Pia wananchi walipinga ujenzi wa mitambo ya kuzalisha umeme kinyerezi Dar es salaam na badala yake wakataka hiyo mitambo ijengwe hukohuko Mtwara.

Kwenye mstari mwingine Waziri Mkuu aliwataka wananchi kumsamehe mkuu wa mkoa wa Mtwara Kanali mstaafu Joseph Simbakalia kwa kauli alizotoa december 21 2012 katika kikao cha kamati ya ushauri pale alipoombwa kuyapokea maandamano ya wakazi wa mkoa huo december 27 ambapo aliwaita wapuuzi na wahaini.

Waziri mkuu katika majumuisho yake aliambatana na Waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo ya kazi profesa Anna Tibaijuka, Waziri wa Uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe, Waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi stadi Dr. Shukuru Kawambwa na Waziri wa mambo ya ndani Dr. Emmanuel Nchimbi.

Katika hizo siku mbili pia Waziri mkuu alikutana na vyama vya siasa vya upinzani, chama cha Mapinduzi CCM, viongozi wa dini ya Kiislamu na Kikristo, Wafanyabiashara, Madiwani na wenyeviti wa mitaa pamoja na Wanaharakati.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.