Thursday, June 20, 2013

Waziri mkuu Pinda azindua mradi wa kuimarisha halmashauri za miji 18 Tanzania bara

Kaimu katibu mkuu ofisi ya waziri mkuu Tamisemi,Jumanne Sageni akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuimarisha halmashauri za miji 18 Tanzania bara uliofanyika mjini Moshi.
Mwakilishi wa benki ya dunia,mkurugenzi mkazi Philippe Dongies akitoa hoyuba yake wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuimarisha halmashauri za miji 18 Tanzania bara uliofanyika mjini Moshi.
Washiriki wa warsha hiyo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Tamisemi, Hawa Ghasia akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuimarisha halmashauri za miji 18 Tanzania bara uliofanyika mjini Moshi.
Waziri mkuu Mizengo Pinda akiwahutubia washiriki wa warsha ya uzinduzi wa mradi wa kuimarisha halmashauri za miji 18 Tanzania bara uliofanyika mjini Moshi.
Washiri wa warsha hiyo.
Waziri mkuu Mizengo Pinda akikata utepe katika vitabu kuashiria kuzinduliwa kwa mradi wa kuimarisha halmashauri za miji 18 Tanzania bara,Uzinduzi huo uliofanyika mjini Moshi.Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Tamisemi, Hawa Ghasia na kulia ni Mwakilishi wa benki ya dunia,mkurugenzi mkazi Philippe Dongies wakishuhudia.
Waziri mkuu Mizengo Pinda akionesha makablasha kuashiria kuzinduliwa kwa mradi wa kuimarisha halmashauri za miji 18 Tanzania bara,Uzinduzi huo uliofanyika mjini Moshi.Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Tamisemi, Hawa Ghasia na kulia ni Mwakilishi wa benki ya dunia,mkurugenzi mkazi Philippe Dongies wakishuhudia.
Washiriki katika picha ya pamoja.
Waziri mkuu akisalimiana na mmiliki wa ukumbi wa Moringe hall uliopo mjini Moshi ambako kumefanyika uzinduzi wa mradi wa kuimarisha halmashauri za miji 18 Tanzania bara.

Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii,Moshi

SERIKALI imesema tatizo la ufuatiliaji wa karibu wa miradi iliyoibuliwa na halmashauri za wilaya nchini sanjari na utekelezaji wake ndio chanzo cha ubadhirifu na matokeo mabaya katika utekelezaji wa miradi hiyo kwa baadhi ya halmashauri.

Hayo yameelezwa jana na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuimarisha halmashauri za miji 18 Tanzania bara iliyofanyika katika ukumbi wa Moringe katika manispaa ya Moshi.

Waziri mkuu Pinda alisema katika mradi huo serikali kuu itahakikisha inaufuatilia kwa karibu na ili kujenga imani kwa wananchi na wafadhili wa mradi huu ambao ni benki ya Dunia na kwamba iwapo miji hiyo itatekeleza mradi huo vizuri na kwa viwango vinavyotakiwa, serikali itapata nguvu ya kufanya mazungumzo ya namna ya kuiangalia miji mingine.

Alisema mafanikio ya mradi huo utaongeza matumaini kwa wananchi na pia kuwavutia wadau wengine kushirikiana na halmashauri za hapa nchini katika kuteleza miradi ya kimaendeleo, ambapo pia alitoa rai kwa wakurugenzi wa halmashauri zilizoko kwenye mradi huo kutosita kuomba ushauri pale itakapoonekana kuna vikwazo katika kuutekeleza.

“Mradi huu unatuhusu sote, halmashauri na wananchi, kila mtu awajibike kulipa kodi zinazotakiwa kwa ajili ya maendeleo ya halmashauri zetu na kuwezesha utoaji wa huduma nyingine ikiwemo utunzaji wa mradii huu katika halmashauri zote husika”, alisema Pinda.

Waziri Mkuu Pinda aliendelea kusema kuwa kuteuliwa kwa Tanzania kuwa nchi ya kwanza Barani Afrika kufanya majaribio ya mfumo wa miradi ya aina hiyo inaonyesha dhahiri jinsi Tanzania inavyoaminika na kusifika kimataifa na kwamba ni vyema mradi huo ukatekelezwa vizuri ili kuilinda heshima hiyo.

“Mkishindwa nyinyi ni kwamba Tanzania imeshindwa, hivyo serikali haitakuwa tayari kusikia visingizio wala sababu zozote zitakazolenga kukwamisha kazi hii njema”, alisema Pinda.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Tamisemi, Hawa Ghasia, amesema mradi huo unaotarajiwa kutekelezwa katika kipindi cha miaka mitano ijayo na kuleta mabadiliko makubwa Tanzania.

Ghasia amesema mradi huu utazihusisha halmashauri za Morogoro, Tabora, Moshi, Sumbawanga, Shinyanga, Songea, Singida, Musoma, Iringa, Njombe, Lindi, Bukoba, Kibaha, Babati, Geita, Korogwe, Mpanda na Bariadi .

Naye Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, hapa nchini Philippe Dangier, alisema benki hiyo imeipa Tanzania mkopo wa Dola za Marekani 255 milioni zitakazotumika katika kutekeleza mradi huo unaotarajiwa kukamilika mwaka 2018.

No comments:

Post a Comment