Sunday, June 23, 2013

ASKARI WA JESHI LA POLISI AFANYA KITENDO CHA UNYAMA KWA MKEWE NA KISHA KUTOWEKA .... RIPOTI KAMILI HII HAPA



Hapa Rehema akiwa wodini katika Hospital ya Rufaa ya mkoa wa Iringa alipokimbizwa kwa matibabu kutokana na kipigo kikali toka kwa askari huyo.
Hapa akionekana mwenye uvimbe  zaidi
Hapa akionyesha majeraha ambayo aliyapata shingoni kutokana na kukabwa shingo na askari huyo
Hapa akiwa hoi kwa kipigo

Bi Rehema Shauri Madongo mkazi wa Wilolesi mjini Iringa akiwa na mtoto wake baada ya kuponea katika tundu la sindano kuuwawa kwa kipigo kutoka kwa mmewe ambaye ni askari polisi mjini Iringa kiasi cha kukimbia nyumba na kurudi kwa wazazi wake
stepen kanyala akiwa na mke wake siku ya harusi yao iliyodumu kwa miaka mitatu sasa
Bi Rehema akiwa nyumbani kwa wazazi wake baada ya kukimbia nyumba yake kutokana na kipigo kisichokwisha
Mama mzazi wa Rehema akiwa Monica Shauri
IGP Mwema

WAKATI jeshi la polisi nchini likiendelea kujiweka karibu na Raia hata kuamua kuanzisha dawati la jinsia katika vituo vya polisi ,kwa mkoa wa Iringa baadhi ya askari wanadaiwa kupiganga na jitihada hizo za polisi kwa kushindwa kuheshimu dawati hilo na badala yake kushiriki kulivunjia heshima jeshi hilo kutokana na kufanya vitendo ambavyo ni kinyume na mkakati wa jeshi hilo katika kuanzisha dawati la jinsia.

Uchunguzi wa mtandao huu wa anaclet-ngoyi.blogspot.com umeonyesha kuwa dawati hilo kwa askari limekosa kuheshimika kutokana na vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia ambavyo baadhi ya askari (30) wamekuwa wakifanya kwa watoto wao na wake zao.

Rehema Shauri Madongo ni mmoja kati ya mwanamke ambaye amebahatika kuolewa na askari polisi kitendo cha upelelezi ambaye anaeleza jinsi alivyotendewa vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa kuteswa na kupigwa kikatili na pindi anapofika polisi hakuna hatua zozote zinazochukuliwa kwa mtuhumiwa huyo ambaye ni askari .

" Mimi niliolewa kwa ndoa na Stephen Kanyala ambae ni askari kitengo cha upelelezi ila baada ya kuolewa ukiwa umepita mwezi mmoja tuo nilianza kushuhudia mateso ya ndoa kutokana na kipigo na mateso makali niliyokuwa nikiyapata"

Anasema kuwa kila wakati pindi anapotaka kujua jambo kutokana kwa mume wake huyo hasa pale anapoona jumbe zenye utata katika simu yake ambazo zimetoka kwa wanawake anaowatambua vizuri amekuwa akijibiwa kwa kipigo kikali.

Rehema alisema kuwa ni rahisi kwake kuweza kuhesabia siku ambazo hajapigwa kuliko kuhesabi siku ambazo amepigwa ambazo ni nyigi zaidi .

Kwa alisema toka ameolewa kila mara amekuwa akipokea kipigo na mbaya zaidi kabla ya kupigwa amekuwa akifungwa mikono kwa pingu zinazotumika kuwafunga watuhumiwa pingu ambazo mume wake huyo amekuwa akizihifadhi ndani ya nyumba .

" Kweli inasikitisha sana kusimulia kwani kabla ya kupigwa nimekuwa nikifungwa pingu mikono kama mharifu sugu na baada ya hapo kipigo kikali kimekuwa kikinikuta ....hadi sasa nimepigwa zaidi ya mara 20 na polisi nimekwenda kuripoti mara tatu na Hospital nimelazwa mara moja ila siku nyingine nimekuwa nikiugulia nyumbani ila nyumbani kwa wazazi nimerudi mara tatu sasa"

Alisema kuwa mbali ya kupigwa na kuumizwa ila kuna mateso mengine ambayo amekuwa akiyapata kutoka kwa mwanaume huyo ni siri yake na hayapaswi kuelezwa hapa kutokana na jinsi ambavyo askari huyo anavyomtenda ukatili wa kinyama.

Hata hivyo alisema kuwa akiwa na mimba ya mwezi mmoja hali ya kipigo ilizidi zaidi na wakati mwingine alipata kumfunga shingo na kanga kwa kutaka kunyonga shingo huku akitishi kumuua .

Alisema kuwa baada ya kujifungua mtoto wa njia ya Oparesheni mwanaume huyo alimpiga kiasi cha kumjeruhi mtoto wa mwezi mmoja kwa kumpiga kofi ambalo lilielekezwa kwake na bahati mbaya likaishia kwa mtoto.

Aidha alisema kuwa kila akifika polisi kufungua kesi hakuna utekelezaji unaofanyika kutokana na polisi kulindana na kuwa suala hilo la askari polisi kulindani lilianza toka wakati kamanda wa polisi akiwa Evarist Mangala ,pia alipofika kamanda Michael Kamuhanda ambaye kwa sasa amehamishwa baada ya cheo kupanda pia amepata kufikisha malalamiko yake ila hakuna jipya ila sasa amefikisha tena suala hilo kwa kamanda mpya RPC Ramadhan Mungi ambae amedai kuwa na imani nae zaidi katika kulishughulikia suala lake

Pia alisema mbali ya kupigwa akiwa nyumbani kwake ila bado anapoamua kukimbia nyumba hiyo na kukimbilia kwa wazazi wake bado askari huyo amekuwa akimfuata na kumpa kipigo mbele ya wazazi wake .

Hivyo alisema katika kunusuru uhai wake kwa sasa ameamua kurudi kwa wazazi wake na suala la ndoa hataki tena .

Kwa upande wake Mama mzazi wa Rehema akiwa Monica Shauri alisema kuwa amechoka kuuguza binti yake kwa kipigo na kuwa kuna wakati mwanaume huyo amekuwa akitishia kumpiga hata yeye.

Hivyo alisema kwa sasa mbali ya kumtoa binti yake Hospital ila wamekuwa wakiishi ndani wamejifungia milango kuogopa askari huyo kuja kuwafanyia ukatili ikiwa ni pamoja na kuwaua kwa risasi kama ambavyo amekuwa akiwatisha mara kwa mara kuwa dawa yao inachemka na ipo siku wataonja mauti.

Bi Shauri alisema mbali ya kuwa yeye ni mmoja wa wacha Mungu kwa maana na Mlokole mzuri ambae kila wakati asubuhi lazima aende kusali ila kwa sasa anaogopa kutoka asubuhi kwa kuhofia kuvamiwa na askari huyo .

Hivyo aliomba jeshi la polisi kuweza kumpa ulinzi yeye na familia yake ama kumkamata mtuhumiwa huyo ambae inadaiwa kwa sasa yupo katika mji wa Iringa ila askari wenzake wanamlinda.

Kuhusu uamuzi wa binti yake wa kuomba ndoa hiyo kuvunjwa alisema anaungana na binti yake kuikataa ndoa hiyo na kuwa kwa sasa wapo tayari kurudisha mahali yake ya Tsh 200,000 ambazo alizitoa kama mahali ili kunusuru uhai wao na uhai wa mtoto wake huyo.

No comments:

Post a Comment