Sunday, June 23, 2013

WAKAZI WA DOM WANAVYOISOTEA SHOO YA KILIMANJARO MUSIC TOUR 'KIKWETU KWETU' UWANJA WA JAMHURI MUDA HUU

 Wakazi wa Mjini Dodoma wakiwa katika foleni ya kuingia Uwanja wa Jamhuri kushuhudia Shoo kabambe ya Kilimanjaro Tanzania Music Tour 2013 'Kiwetu Kwetu' iliyoanza hivi punde uwanjani hapo, ambapo leo wakazi wa Dom watawaona 'Live' wasanii wa muziki wa kizazi kipya walioshiriki katika kinyang'anyiro cha kuwania tuzo hizo hivi karibuni jijini Dar. Baadhi ya Wasanii hao watakaoshambulia jukwaa ni pamoja na Prof. Jay, Lady Jay Dee, Ommy Dimpoz, Roma Mkatoliki, Ally Kiba, Linex na wengine wengi.
 Jukwaa litakalotumiwa na wasanii hao kutoa burudani....
 Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha Chanel 5, Patrick Nyembela, akiwasili uwanjani hapo kwa ajili ya kuweka mitambo yake sawa kurusha live......
 Mafundi wakijipanga kuweka sawa mitambo.....
 Mabaunsa wakidhiti pande za milangoni.....
 Patrick Nyembela, akishoo Love na naniliu.......
 Hii ni sehemu ya foleni ya kuingia uwanjani humo kushuhudia shoo hiyo.
 Mageti yote yakiwa bize kuruhusu wakazi wa Dodoma kuingia uwanjani humo.
 Mtangazaji wa Televisheni ya Chanel 5, Patrick Nyembela, (aliyesimama nyuma) akiwa na timu yake nzima tayari wakijiandaa kuanza kazi ya kurusha Live shoo hiyo ya kukata na shoka iliyoanza hivi punde pande za Uwanja wa Jamhuri, mjini Dodoma.
 Wasimamizi au wasema chochote wa Shoo hiyo, Zembwela (kushoto) na Abdallah Ambua, wakishoo Love kabla ya kuanza libeneke hilo.
 Foleni ya kuingia uwanjani kama kawa......
 Foleni ....................
Sehemu ya wakazi wa mjini Dodoma, ambao tayari wamefanikiwa kutinga ndani ya viwanja hivyo.

No comments:

Post a Comment