Sunday, March 31, 2013

TAMASHA LA UTANGULIZI LA AIRTEL YATOSHA LATIKISA MKOA WA MOROGORO LEO.

Wasanii wa kundi la Vichekesho la Kinoko lenye maskani yake Kinondoni jijini Dar, wakiwakilisha wakati wa tamasha la utangulizi maalum kwa Uzinduzi wa huduma ya AIRTEL Yatosha lililofanyika mkoani Morogoro.
Jukwaani ni mmoja wa wasanii chipukizi wa mkoni Morogoro akiwakilisha wakati Airtel wapolifanya tamasha maalum la uzinduzi wa huduma ya Airtel Yatosha mjini humo.
Wakazi wa Morogoro waliendelea kujitokeza kwa wingi jukwaani kujiunga na huduma ya Airtel Yatosha kwa Kupiga  namba *149*99#,na kupokelewa vyema na wakazi wa mji huo.
Wakazi wa Morogoro walijitokeza kwa wingi jukwaani kujiunga na huduma ya Airtel yatosha kwa Kupiga  namba *149*99#.
Sehemu ya umati wa watu waliojitokeza viawanja vya shule ya msingi Sabasaba kushuhudia shamra shamra za uzinduzi wa maalum wa huduma ya AIRTEL Yatosha mjini Morogoro
========  =======  =======  ====

Airtel yatosha yapokelewa kwa kishindo na umati wa wakazi wa morogoro waliojitokeza kwa wingi leo katika viwanja vya Sabasaba vilivyopo mjini morogoro wakati Airtel ilipofanya tamasha la utangulizi leo na kutumbuizwa na wasanii wa kundi la Vichekesho la KINOKO lenye maskani yake toka jijini Dar es salaam

Akiongea wakati wa tamasha hilo la Utangulizi meneja uhusino wa Airtel Jackson Mmbando alisema “Airtel YATOSHA imefanikiwa  kupunguza gharama za mawasiliano nchini hivyo tumeamua kuingia Morogoro kwa kishindo kuanza matamasha yetu ya kutoa elimu kuhusu huduma hii ya Airtel yatosha ili wananchi waitumie na kufaidika zaidi" alisema.
 Zaidi zaidi pia tumejipanga kutoa burudani kwa wananchi kwa kufanya matamsha haya ambapo tutazunguka kila pande waliko wateja wetu ili pia kuendeleza ushkaji wetu na wateja wetu nchini Tanzania.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

Basi la Sai Baba lapoteza muelekeo na kuingia vichakani,watu watano wajeruhiwa

 

 ABIRIA wapatao 45 waliokuwa wakisafiri na basi la kampuni ya Sai
baba,kutoka Jijini Dar es salaam kwenda Masasi,mkoani
Mtwara,wamenusulika kifo,kufuatia gari yao kuacha njia na kuingia vichakani.


Tukio la ajali hiyo limetokea maeneo ya kijiji na kata ya
Mbanja,iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Lindi,Katika ajali hiyo watu watano akiwemo dereva na kondakta ndiyo
waliokuwa wameumia na kukimbizwa Hospitali ya mkoa wa Lindi, Sokoine kwa
matibabu.


Waliojeruhiwa ni,Juma Mtoi (Dereva),Said Mkumbwa (Kondakta) wakazi wa
Jijini Dar es salaam,na kwa upande wa abiria ni John Kasawala
(21),mkazi wa kijiji cha Nangamba,wilaya ya Nanyumbu,mkoani
Mtwara,Noel Akui (35) mkaazi wa wilaya ya Masasi,mkoani Mtwara na
Kuruthumu Ally (25) wakazi wa mji wa Lindi.


Said Mkumbwa ambaye ni kondakta wa basi hilo, amesema kwamba chanzo
cha ajali hiyo ni kupasuka kwa tairi la mbele upande wa kulia kwa
dreva, ambapo liliacha njia na kutumbukia mtoni chini ya daraja la
Mbanja.


Akasema basi lake lililokuwa limebeba abiria 45 lilikuwa likitoka
Jijini Dar es salaam kuelekea wilaya ya Masasi,mkoani Mtwara,kufuatana
na ruti zake.


“Tulikuwa tikitokea Dar es salaam kwenda Masasi,kwani ndiyo ruti yetu
ilivyo, na ndipo tulipofika eneo hilo mpira wa tairi ya mbele upande
wa dereva likapasuka na kukosa mwelekeo kisha likagonga kingo ndogo ya
daraja na kutumbukia mtoni,,,,,,,,,tunachoshukuru ni kwamba wote
tumetoka tukiwa hao hakuna aliyepoteza maisha”Alisema Mkumbwa.


Kuruthumu Ally ambaye amepata michubuko kiasi usoni na mabegani na
John Kasawala aliyeumia kichwani,kwa nyakati tafauti walisema wao
walikuwa wamekaa sehemu ya mbele walisema wakiwa wanaendelea na safari
yao hiyo,ghafla walisikia mlio mkubwa kasha basi lao kuyumba na
kutumbukia chini ya daraja.


Akizungumza kwa niaba ya kaimu mganga mfawidhi wa Hospitali
hiyo,Dkt,Edgar Mlawa amesema majeruhi hao wameumia sehemu mbalimbali
ya miili yao,ikiwemo vichwani na hali zao zinaendelea vizuri na kuna
mategemeo ya kuweza kuendelea na safari zao kama kawaida.


“Hapa Hospitalini wamefikishwa majeruhi watano tu,akiwemo
dereva,kondakta wake na abiria watatu,mmoja wao ni mwanamke, ambapo
wote hao hakuna aliyekuwa sirias kwa kuumia licha ya kupata majeraha
sehemu mbalimbali ya miili yao.ikiwa ni pamoja na vichwani”Alisema
Dkt,Mlaw
a.

RAIS KIKWETE AIFARIJI FAMILIA YA MAREHMU ADOLAR MAPUNDA

m3

m1
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo wakati alipokwenda kutoa pole nyumbani kwa Mkurugenzi Mkuu mstaafu wa TTCL Marehemu Adolar Mapunda huko Tegeta, Dar es salaam jana Machi 29, 2013. Marehemu Mapunda, ambaye pia alipata kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Tanzania Standard Newspapers na Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
m2
 
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo wakati alipokwenda kutoa pole nyumbani kwa Mkurugenzi Mkuu mstaafu wa TTCL Marehemu Adolar Mapunda huko Tegeta, Dar es salaam jana Machi 29, 2013. Marehemu Mapunda, ambaye pia alipata kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Tanzania Standard Newspapers na Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji mjane wa marehemu Adolar Mapunda huko Tegeta, Dar es salaam jana Machi 29, 2013. Marehemu Mapunda, ambaye pia alipata kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Tanzania Standard Newspapers na Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, alifariki usiku wa kuamkia jana. m4
 
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiifariji familia ya marehemu Adolar Mapunda huko Tegeta, Dar es salaam jana Machi 29, 2013. Marehemu Mapunda, ambaye pia alipata kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Tanzania Standard Newspapers na Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, alifariki usiku wa kuamkia jana. m5
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na mtoto wa marehemu Adolar Mapunda huko Tegeta, Dar es salaam jana Machi 29, 2013. Marehemu Mapunda, ambaye pia alipata kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Tanzania Standard Newspapers na Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, alifariki usiku wa kuamkia jana.

Taarifa ya Jeshi la Polisi Kuhusu sikukuu ya Pasaka



JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI
JESHI LA POLISI TANZANIA

Anuani ya Simu
“MKUUPOLISI”

Ofisi ya Inspekta Jenerali wa Polisi,
Simu : (022) 2110734

Makao Makuu ya Polisi,
Fax Na. (022) 2135556
S.L.P. 9141,

28/03/2013

TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI

1. KATIKA KUELEKEA SIKUKUU YA PASAKA, INAYOTARAJIWA KUADHIMISHWA KUANZIA TAREHE 29 MACHI HADI TAREHE 1 APRILI, 2013. JESHI LA POLISI LINAPENDA KUWAONDOA HOFU WANANCHI WOTE KUWA LIMEJIPANGA KIKAMILIFU KATIKA KUIMARISHA USALAMA WA RAIA NA MALI ZAO KWA KIPINDI CHOTE CHA SIKUKUU NA BAADA YA SIKUKUU, HIVYO WANANCHI WASHEREKEE SIKUKUU KWA AMANI NA UTULIVU, PASIPO VITENDO AMA VIASHIRIA VYOVYOTE VYA UVUNJIFU WA AMANI.

2. IKUMBUKWE KUWA, WANANCHI WENYE IMANI YA KIKRISTO NA HATA MADHEHEBU MENGINE HUTUMIA MUDA HUO KWENDA KUABUDU PAMOJA NA MUENDELEZO WA SHEREHE HIZO KWENYE MAENEO MBALIMBALI YA STAREHE. UZOEFU UNAONYESHA KUWA BAADHI YA WATU HUTUMIA KIPINDI HICHO CHA SIKUKUU KUFANYA MATUKIO YA UHALIFU KUTOKANA NA MIKUSANYIKO HIYO YA WATU KATIKA MAENEO MBALIMBALI.

3. JESHI LA POLISI LINAPENDA KUWAONDOA HOFU WANANCHI NA WAUMINI WOTE KUWA, ULINZI UMEIMARISHWA KWENYE MAENEO YOTE YA KUABUDIA, FUKWE ZA BAHARI, SEHEMU ZA STAREHE NA MAENEO MENGINE YOTE AMBAYO YATAKUWA NA MIKUSANYIKO MIKUBWA YA WATU.AIDHA, TUNAPENDA KUWATAHADHARISHA WALE WOTE AMBAO WATAKUWA WAKITUMIA BARABARA, KUWA MAKINI KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI NA HASA KWA MADEREVA KUEPUKA KWENDA MWENDO KASI NA KUTUMIA VILEVI WAWAPO KAZINI.

4. VILEVILE, JESHI LA POLISI LINAWATAKA WANANCHI KUONDOA HOFU NA KUWAPUUZA WATU WACHACHE AMA KIKUNDI CHA WATU WANAOTUMIA KIPINDI HIKI CHA SIKUKUU KUWATIA HOFU KWA KUSAMBAZA MESEJI ZA VITISHO KWA WATU MBALIMBALI KWA LENGO LA KUVURUGA AMANI NA UTULIVU KATIKA KIPINDI HIKI CHA SIKUKUU. KITENDO HICHO CHA KUSAMBAZA MESEJI ZA VITISHO KWA WANANCHI NI UHALIFU KAMA UHALIFU MWINGINE NA WAKIBAINIKA HATUA ZA KISHERIA ZITACHUKULIWA DHIDI YAO.

5. KATIKA KUHAKIKISHA USALAMA KWENYE KUMBI ZA STAREHE, WAMILIKI WA KUMBI HIZO WAZINGATIE UHALALI NA MATUMIZI YA KUMBI ZAO KATIKA UINGIZAJI WA WATU KULINGANA NA UWEZO WA KUMBI HIZO, BADALA YA KUENDEKEZA TAMAA YA FEDHA KWA KUJAZA WATU KUPITA KIASI. VILEVILE, WAZAZI WAWE MAKINI NA WATOTO WAO NA HASA DISKO TOTO, ILI KUEPUKA AJALI NA MATUKIO MENGINE YANAYOWEZA KUSABABISHA MADHARA JUU YAO.

6. JESHI LA POLISI LINATOA TAHADHARI KWA WANANCHI WOTE KWAMBA, WATOKAPO KWENYE MAKAZI YAO WASIACHE NYUMBA WAZI AMA BILA MTU NA WATOE TAARIFA KWA MAJIRANI ZAO, NA PALE WANAPOWATILIA MASHAKA WATU WASIOWAFAHAMU WASIKAE KIMYA BALI WATOE TAARIFA KWA JESHI LA POLISI AU VIONGOZI WAO WA SERIKALI YA MTAA, SHEHIA, KIJIJI AU KITONGOJI ILI HATUA ZA HARAKA ZIWEZE KUCHUKULIWA.

7. MWISHO, NAPENDA KUWAHAKIKISHIA WANANCHI KWAMBA, JESHI LA POLISI LINATEKELEZA MAJUKUMU YAKE KWA KUZINGATIA SHERIA ZA NCHI NA HIVYO HALITAWAJIBIKA KUMWONEA HURUMA AMA UPENDELEO MTU YEYOTE ATAKAYEENDA KINYUME NA SHERIA ZA NCHI.
NAWATAKIENI WATANZANIA WOTE PASAKA NJEMA.

IMETOLEWA NA:
ADVERA SENSO
MSEMAJI WA JESHI LA POLISI (T)

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi:' Watu waliyoko karibu na jengo jingine la ghorofa 15 lililojengwa na mkandarasi wa kwanza aliyejenga jengo la ghorofa 16 na Kuporomoka Nakusababisha vifo vya Watu 22 ,kuhama mara moja na ubomoaji ufanyike bila kuleta madhara.'

Picha Juu ni jengo jingine la ghorofa 15 lililojengwa na mkandarasi aliyesababisha jengo la ghorofa 16 kuanguka na kusababisha vifo vya watu 22 hadi sasa ambalo waziri lukuvi ametoa maelekezo kubomolewa
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi
---
Dar es Salaam. Idadi ya watu waliokufa kutokana na kufukiwa na kifusi cha jengo la ghorofa 16 lililoporomoka juzi asubuhi jijini Dar es Salaam, imefikia 22.
 
Habari zilizopatikana kutoka eneo la uokoaji na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova zinaeleza kuwa miili iliyopatikana imepelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili.
 
Jengo hilo lililokuwa likijengwa mkabala na Msikiti wa Shia Ithnasheri ulioko Barabara ya Indira Gandhi na Kampuni ya Lucky Construction Limited liliporomoka saa 2.30 asubuhi wakati mafundi na vibarua wakiendelea na ujenzi huku chini watoto wakicheza mpira na mama lishe wakiendelea na biashara zao kama kawaida.

Ona Jinsi Zoezi la Uokoaji Linavyoendelea Kwa Masaa 48 Baada Ya Jengo la Ghorofa 16 Kudondoka Jijini Dar es Salaam na Kusababisha Vifo vya Watu


Picha juu zinaonyesha zoezi likiendelea usiku na mchana
Kikosi cha Huduma ya Kwanza Kipo Kwa zaidi ya masaa 48 sasa
Kazi ya uchimbaji wa kifusi ukiendelea
Sehemu ya kifusi kizito kikiwa tayari kuchimbuliwa
Kazi ya Uchimbaji wa kifusi ikiwa inaendelea kwa masaa zaidi ya 48 mpaka sasa
Zoezi la kuangalia kama kuna miili iliyofukiwa kwenye kifusi ikiendelea alfajiri ya leo