Wednesday, June 19, 2013


Didier Drogba kurudi kwenye timu ya taifa .

image
Mshambuliaji wa Galatasaray ya Uturuki Didier Drogba amehakikishiwa nafasi yake kwenye kikosi cha timu ya taifa baada ya kuachwa kwenye mechi mbili za kufuzu kwa kombe la dunia mwaka 2014.

Kocha wa timu ya taifa ya Ivory Coasta Mfaransa Sabri Lamouchi amesema kuwa atakuwa “mwendawazimu” kama akimuacha mchezaji mwenye uwezo na mchango mkubwa kwa timu ya taifa kama Drogba na kuachwa kwake kwenye vikosi vya hivi karibuni hakuamini kuwa amewekwa pembeni moja kwa moja.

Lamouchi aliongeza kuwa Drogba alihitaji kupumzishwa baada ya kuitumikia timu ya taifa kwa muda mrefu lakini haimaanishi kuwa hatacheza tena kwenye timu hiyo.

Drogba hajaichezea timu yake ya taifa tangu ilipotolewa na Nigeria kwenye michuano ya kombe la mataifa ya Afrika na mawazo ya wengi ni kwamba Drogba hatarudi tena kwenye timu hiyo baada ya kuonekana umri umemtupa mkono na kiwango chake kushuka.

Ivory Coast imekuwa ikiwatumia washambuliaji kama Lacina Traore na Wilfred Bony ambao walifungakwenye mechi ya jumapili dhidi ya Taifa Stars huku Dorgba akiwa ameachwa. Bony alimaliza msimu uliopita kama mshambuliaji bora wa Kiafrika Barani Ulaya akiwa amefunga mabao 30 kwenye ligi ya Uholanzi.

Didier Drogba huenda akaitwa kwenye kikosi cha Ivory Coast kitakachoitwa mwezi wa nane kwa ajili ya mechi za kirafiki za kimataifa ikiwemo mechi dhidi ya Mexico.

No comments:

Post a Comment