Sunday, June 23, 2013


MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AONGOZA KIKAO CHA SMZ NA SMT MJINI DODOMA LEO

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongoza Kikao cha SMZ na SMT, kiliochofanyika Dodoma Hoteli, leo. Kulia ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda, na (kushoto) ni Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, leo ameongoza Kikao cha SMT na SMZ, kilichofanyika kwenye ukumbi wa Dodoma Hoteli, mjini Dodoma, leo. Kikao hicho kimehudhuriwa pia na mhe. Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi, Seif Idd, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amani, Ali Juma Shamhuna na Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) Samih Suluhu pamoja na Wajumbe washiriki wa kikao hicho ambao ni Mawaziri kutoka serikali zote mbili za Tanzania Bara na Zanzibar.
 Baadhi ya Wajumbe wa Kikao hicho ambao ni Mawaziri kutoka Serikali ya Zanzibar.
 Baadhi ya Wajumbe wa Kikao hicho ambao ni Mawaziri kutoka Serikali ya Tanzania Bara.
 Baadhi ya Wajumbe wa Kikao hicho ambao ni Mawaziri kutoka Serikali ya Zanzibar.
 Baadhi ya Wajumbe wa Kikao hicho ambao ni Mawaziri kutoka Serikali ya Tanzania Bara.
 Wajumbe wa Kikao hicho.
Baadhi ya Wajumbe wa Kikao hicho ambao ni Mawaziri kutoka Serikali ya Zanzibar.

*HAYA NI MAAGIZO AU NI 'ASANTE OBAMA'?

Mafundi wakiendelea na kazi ya ukarabati wa kumwaga Kokoto na kuzisambaza na kuzikandamiza, pembezoni mwa barabara ya Kilwa, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mazingira kuelekea ujio wa Rais wa Marekani nchini Tanzania, Barack Obama, anayetarajia kuwasili nchini mwezi ujao.

*JICHO LANGU NDANI YA MJI WA DODOMA

 Mitaa ya Stendi ya Mabasi yaendayo Mikoa mingine katika Mji wa Dodoma, Eneo hilo kwa sasa kuna Stendi isiyo rasmi kutokana na ujenzi wa Kituo hicho ambapo mabasi hulazimika kuegesha pembezoni mwa barabara kubwa huku yakipakia kwa foleni moja baada ya jingine.
Huku nako ni stendi ndogo iliyopo Mtaa wa Majengo ambayo huegeshwa magari yanayokwenda katika vijiji vya Mji wa Dodoma na Wilaya zake.

*MWIGULU NCHEMBA NA PETER MSIGWA NUSURA WAZICHAPE 'KAVU KAVU' DODOMA

Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba (kushoto) akizozana na wabunge wa Chadema, Mchungaji Peter Msigwa(kulia)mbunge wa Nyamagana, Ezekiah Wenje (wa pili kulia) na Mbunge wa Musoma Mjini, Vicent Nyerere (wa pili kushoto) baada ya kukutana nje ya ukumbi wa mikutano wa St Gasper,Dodoma jana wakati wa semina ya wabunge ya kuhusu Ukimwi. 
*******************************************
*Tukio hilo lilitokea katika viwanja vya Hoteli ya St Gasper nje kidogo ya mji wa Dodoma, walipokwenda kwa ajili ya kuhudhuria semina ya wabunge wapambanaji na Ukimwi, ambapo baadhi ya wabunge wa Chadema walihudhuria, baada ya kutoonekana mjini humo tangu Juni 17 mwaka huu.

Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa na mbunge wa Iramba Magharibi (CCM), Mwigulu Nchemba jana nusura wachapane makonde baada ya kutupiana maneno ya kashfa, wakituhumiana kuhusika na mlipuko wa bomu uliotokea Jumamosi iliyopita mkoani Arusha.
Tukio hilo lilitokea katika viwanja vya Hoteli ya St Gasper nje kidogo ya mji wa Dodoma, walipokwenda kwa ajili ya kuhudhuria semina ya wabunge wapambanaji na Ukimwi, ambapo baadhi ya wabunge wa Chadema walihudhuria, baada ya kutoonekana mjini humo tangu Juni 17 mwaka huu.
Wabunge hao wa Chadema hawakuhudhuria kikao chochote cha Bunge kutokana na kwenda mkoani Arusha kwa shughuli mbalimbali, kutokana na mlipuko wa bomu uliotokea katika mkutano wao wa kuhitimisha kampeni zake za uchaguzi mdogo wa udiwani katika viwanja vya Soweto, Juni 16 jijini humo.
Malumbano hayo yanatokana na Nchemba kuituhumu Chadema kuhusika na mlipuko huo, Juni 20 mwaka huu wakati akichangia hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka 2013/2014, akisema chama hicho kilipanga kulipua bomu hilo ili kuwafanya Watanzania waamini kuwa Serikali ya CCM ndiyo inayohusika na tukio hilo.
TUKIO LILIVYOANZA:- Wakati Msigwa akiingia katika ukumbi huo akiwa ameongozana na Mbunge wa Nyamagana (Chadema), Ezekiah Wenje, walikutana uso kwa uso na Nchemba ambaye alikuwa akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Said Amour Arfi.
Baada ya Nchemba kumwona Msigwa alimkaribisha mchungaji huyo akisema; “Karibu sana bwana, salama lakini?”
Hata hivyo, badala ya kujibu salamu hiyo ya Nchemba, Msigwa alikuja juu na kumtuhumu Nchemba kwamba anatoa kauli zinazoweza kuvuruga amani ya nchi.
“Wewe ni mtu hatari sana, haya yote yanasababishwa na wewe, mnatumia damu za watu kutafuta madaraka,” alisema Msigwa akimtupia maneno Mwigulu.
Baada ya kauli hiyo Nchemba alihoji akisema: “Ki-vipi? Hayo mambo tuyaache, Msigwa achana na haya mambo!”
Baada ya Nchemba ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM kujibu, Msigwa alimsogelea karibu na kumnyooshea kidole, huku akiendelea kumtuhumu kuwa ana siasa chafu zinazopandikiza chuki kwa jamii.
Malumbano hayo pia yaliingiliwa na Mbunge wa Musoma Mjini (Chadema), Vicent Nyerere ambaye alimuunga mkono Msigwa, huku akimtuhumu Nchemba kuwa ni mtu mbaya katika siasa za Tanzania. Katika kile kilichoonekana kutaka kuweka mambo sawa, Wenje alimvuta Msigwa na kumpeleka ukumbini ili kuepusha shari baada ya wabunge hao kuzidi kurushiana maneno. Chanzo:- www.mwananchi.co.tz

*RAIS WA TFF LEODGER TENGA KUFUNGA KOZI YA MAKOCHA JUMANNE

RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodger Tenga anatarajia kuwa mgeni rasmi katika ufungaji wa kozi ya makocha wa ngazi ya pili (Intermediate) itakayofanyika Jumanne kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, kuanzia saa tano asubuhi.

Kozi hiyo iliyodumu kwa wiki nne, ilifunguliwa rasmi Juni 3 mwaka huu kwenye Ukumbi wa Harbours Club, uliopo Kurasini.

Mkurugenzi wa Ufundi Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), Joseph Kanakamfumu, alisema Rais Tenga ameridhia kufunga kozi hiyo baada kukosekana katika ufunguzi wa kozi hiyo kutokana na majukumu aliyokuwa nayo.

“Kozi yetu ya ngazi ya pili itafungwa Jumanne kwenye Uwanja wa Taifa kuanzia saa tano asubuhi na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodger Tenga ndiye atatufungia kozi yetu na ameridhia kuwa atakuwa nasi,” alisema Kanakamfumu.

Alisema kozi hiyo itakuwa chachu ya kupatikana kwa makocha watakaosaidia maendeleo ya mchezo huo katika Mkoa wa Dar es Salaam na Taifa kwa ujumla.

Kozi hiyo ni ya kwanza kuendeshwa na DRFA tangu kuingia madarakani kwa uongozi mpya wa chama hicho Desemba 12, chini ya Mwenyekiti Almas Kassongo.

*MWENYEKITI UVCCM TAIFA SADIFA JUMA HAMISI APINGA MFUMO WA SERIKALI TATU

Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Sadifa Juma Hamisi (katikati) akiwa na mwenyekiti wa UVCCM kilimanjaro, Fredrick Mushi (kulia) na Kaimu Katibu wa CCM mkoa wa Kilimanjaro, Aluu Segamba katika Hafla ya kutunuku Vyeti kwa wanachama wa UVCCM vyuo vikuu Kilimanjaro.
***********************************

MWENYEKITI wa Umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi Taifa (UVCCM), Sadifa Juma Hamisi, amepinga vikali kuwepo kwa mfumo wa serikali tatu kama inavyopendekeza rasimu ya katiba mpya.

Sadifa ameyasema hayo wakati akizungumza na wanachama wasomi wa UVCCM kutoka katika vyuo vikuu mkoani kilimanjaro katika hafla ya kuwaaga wasomi hao na ambapo pia ametunuku vyeti vya uanachama kwa wanafunzi 312 pamoja na kuwakabidhi kadi za uanachama wanachama wapya.

Mwenyekiti wa UVCCM Kilimanjaro akiongoza maandamano kuelekea katika ukumbi wa CCM mkoa ambapo ndipo ilikofanyikia mkutano mkubwa wa UVCCM jana. Mwenyekiti huyo ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Donge (CCM) zanzibar, amesema uwepo mfumo wa serikali tatu ni mzigo mkubwa kwani kutokana na uduni wa uchumi wan chi yetu itakuwa vigumu kuendesha serikali tatu kwa maana ya serikali ya Zanzibar, serikali ya Tanzania bara na ule wa muungano.
Viongozi waandamizi wa CCM mkoani Kilimanajro katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa.  “Jamani tusidanganyane, kuendesha serikali tatu ni mzigo, kwa uduni wa uchumi wetu sidhani kama itakuwa rahisi kuendesha serikali tatu, kama kutakuwa na serikali tatu kuna hatari ya kuvunjika kwa muungano wetu huu maana uwezo kuchangia hatuna, tutajiingiza kwenye matatizo makubwa, vijana tuwe makini na tutumie taaluma zetu kuhimiza umuhimu wa kuwepo kwa muungano huu wa sasa,"
Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Sadifa Juma Hamisi Akipokea Maandamano ya Wanafunzi wa Vyuo vikuu Kilimanjaro ambao ni makada wa UVCCM mkoani Kilimanjaro. Aidha Sadifa amewahimiza vijana kuwa mfano mzuri kwa jamii huku akiwahimiza kuwa waadilifu, wazalendo, kujiamini na kuwa na nidhamu hali ambayo itasaidia kuwepo kwa amani na usalama wa nchi.

Amesema bila amani na muungano wa wananchi maendeleo hayawezi kupatikana katika nchi ambpo aliwataka vijana kuwa mtari wa mbele kuwaelimisha wananchi wa kawaida juu ya umuhimu wa kuenzi, kudumisha na kuimarisha muungano wa zanzibar na Tanganyika  kama njia pekee ya kuhakikisha nchi inakuwa na amani siku zote.
Katibu wa UVCCM manispaa ya Moshi, Bwana Makwaiya akisakata Rumba muda mfupi baada ya maandamano kuwasili katika makao makuu ya CCM mkoa wa kilimanjaro

“Vijana tuna wajibu kubwa wa kuwaenzi waliotuletea muungano wetu wa sasa, taaluma zetu ziwe dira ya jamii katika kuenzi, kudumisha na kuimarisha muungano wetu kwani ndio njia pekee ya kusaidia kudumisha amani na usalama wan chi yetu, tuepuke kujiingiza katika mkumbo wa wale wanaodai nchi haitatawalika,” amesema

Hata hivyo Sadifa amewataka vijana kutodanganyika na vyama vinavyoeneza chuki na maandamano yasiyokuwa na msingi wowote huku akifafanua kuwa kisheria kuandamana na haki ya msingi lakini ifuate sheria na yassingilie haki za wengine.
Sadifa akikabidhi cheti cha unachama kwa mwanafunzi wa chuo kikuu muccobs jana, jumla ya wanavyuo 312 walipata vyeti vya uanachama wa UVCCM.

“Chama pekee katika nchi hii ni CCM, kuna vyama vingine vimeanzishwa ambavyo mimi binafsi naviita ‘Saccos’, hauwezi ukajikopesha fedha kienyejienyeji kama alivyofanya Dk. Slaa! Vijana tuwe makini na saccos hizi ambazo ajenda zao ni kukopeshana na vurugu tu,” amesema Sadifa.

Kwa upande wake mwenyekiti wa shirikisho la wanafunzi wa vyuo vikuu wanachama wa CCM kilimanjaro, Wakati Mtulya akizungumzia changamoto wanazokumbana nazo, alisema kumekuwa na urasimu ndani ya bodi ya mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu, ambapo mikopo imekuwa ikitolewa kwa watu wasiostahili huku walengwa wakiendelea kutaabika.
Mwenyekiti wa shirikisho la Vyuo Vikuu mkoani Kilimanjaro, Wakati Mtulya. Amesema kuwa kumekuwa na mchezo ndani ya bodi hiyo, ambapo mikopo imekuwa ikitolewa kwa watoto wa matajiri huku wastahili ‘watoto wa wakulima’ wakibaki kuzungushwa na kuwekewa masharti magumu ya kupata mikopo hiyo jambo ambalo limekuwa likichangia kuwepo kwa vitendo vibaya miongoni mwa wanafunzi hao.
Sadifa (aliyevaa suti) akiongoza vijana kucheza kwaito katika ukumbi wa CCM mkoa wa Kilimanjaro
“Mikopo ni yetu, sio ruzuku, lazima tukopeshwe kwa wakati kwani lazima tutairudisha lakini jambo la kusikitisha, bodi hii imekuwa ikitoa mikopo kwa watoto wa masaki, huku sisi watoto wea mkulima tukiendelea kuzungushwa na kuwekewa masharti magumu ili kupata mikopo hiyo, hili ni tatizo,” amesema Mtulya.

No comments:

Post a Comment