Saturday, September 22, 2012

EDA SYLIVESTER ATWAA TAJI LA REDD'S MISS TEMEKE 2012 USIKU HUU


Eda Sylvester (katikati) akiwa na mshindi wa pili Flaviana Maeda (kushoto) na mshindi wa tatu Catherine Masumbigana (kulia).
 
MREMBO Eda Sylvester usiku huu amefanikiwa kutwaa taji la Redd's Miss Temeke 2012 katika kinyang'aniro kilichofanyika katika ukumbi wa PTA Sabasaba, Temeke jijini Dar es Salaam. 

Eda Sylvester mwenye umri wa miaka 21 anatoka katika kitongoji cha Kigamboni na Mwanafunzi chuo Kikuu cha Dar es Salaam akichukua Shahada ya Sanaa. Eda anapendelea kusafiri na kuangalia filamu.

Matarajio ya Eda ni kuwa msanii wa Kimataifa na mafanyabiashara mwenye mafanikio ya juu.

Watoto wameiva katika Elimu ya Usalama barabarani Iringa

 Mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya Msingi Malangali, iliyopo mkoani Iringa, Steven Mligo akitoa elimu kwa watoto wenzake juu ya Usalama barabarani na namna mbalimbali za matumizi sahihi ya barabara ikiwa ni pamoja na kutambua alama mbalimbali za barabarani. Mligo alikuwa akitoa elimu hiyo katika banda la Polisi Trafiki lililopo katika maonesho ya Wiki ya Nenda kwa Usalma Kitaifa inayofanyika Mkoani Iringa katika uwanja wa Samora chinbi ya Udhamini wa Kampuni ya simu ya Airtel. 
 
Steven Mligo akitoa mafunzo kwa watoto wenzake na kuonesha dhahiri uwezo wake na jinsi alivyopata elimu hiyo ya usalama barabarani baada ya kupatiwa mafunzo shuleni kwao na maofisa wa Trafiki.
 
Mtaalam wa Elimu kutoka Mfuko wa Elimu Manispaa ya Iringa, Germana Kapinga (kulia) akimsikiliza mkazi wa mjini Iringa aliyetembelea banda lao lililopo katika maonesho ya Wiki ya nenda kwa Usalama viwanja vya Samora mjini Iringa leo.
 Wakazi wa mjini Iringa wakiwa katika banda la ASAS wakijipatia bidhaa mbalimbali zitokanazo na maziwa. 
 
Wakazi wa mjini Iringa wakimsikiliza, Mwenyekiti wa Taasisi ya Usalama barabarani watu wenye Ulemavu, Getram Kabate juu ya alama mpya kuu za makundi matano ya watu wenye ulemavu za usalama barabarani.
 
Kikosi kazi ambacho leo kilikuwa kikitoa elimu ya Usalama barabarani katika Maonesho ya maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani mjini Iringa.
 
 Kwa lugha fasaha unaweza kumuita Fahari! Huyu dume la Ngombe ambalo linakadiriwa kuwa na uzito wa zaidi ya kilo 1000, akiwa katika maonesho ndani ya banda la ASAS DAIRY FARM katika uwanja wa Samora mjini Iringa yanapoendelea maonesho ya Wiki ya Nenda kwa Usalma kitaifa.
 
 Wakazi mbalimbali mjini Iringa, wakiangalia Ng’ombe katika banda la ASAS DAIRY FARM katika uwanja wa Samora mjini Iringa yanapoendelea maonesho ya Wiki ya Nenda kwa Usalma kitaifa.
 
Maofisa wa Kampuni ya Airtel Tanzania wakimlisha majani dume la kisasa la Ng’ombe katika banda la ASAS DAIRY FARM katika uwanja wa Samora mjini Iringa yanapoendelea maonesho ya Wiki ya Nenda kwa Usalma kitaifa. Mbegu za Ng'ombe hao zinatoka Ujerumani.

WAISLAMU WAFANYA MAANDAMANO JIJINI DAR KULAANI FILAMU YA KUMKASHIFU MTUME MOHAMMAD

 
Baadhi ya waislamu wakiwa na mabango yanayolaani filamu ya kashfa dhidi ya Mtume (S.A.W).
Mmoja wa waislamu akionyesha hisia zake wakati wa mkutano.
Askari wa Kikosi cha Kuzuia Ghasia (FFU) wakidumisha ulinzi eneo la mkutano.
Waislamu wakizidi kulaani kashifa hizo kwa nguvu zote.
MAMIA ya waumini wa dini ya Kiislamu leo wamefanya mkutano katika Uwanja wa Kidongo Chekundu uliopo jijni Dar es Salaam wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali wa kulaani filamu ya kumkashifu Mtume Mohammad. 
Katika mkutano huo viongozi wa dini hiyo walitoa tamko lenye vipengele kadhaa, ikiwemo kuiomba serikali kuufunga mara moja Ubalozi wa Marekani nchini.

RAIS KIKWETE AMTEUA MEJA JENERALI SAMUEL ALBERT NDOMBA KUWA MNADHIMU MKUU WA JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA (JWTZ).


Mkuu Mpya wa Jeshi la Kujenga Taifa(JKT) Meja Jenerali Samwel Ndomba akila kiapo mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam.Picha na Maktaba hivi karibuni).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Meja Jenerali Samuel Albert Ndomba kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).endelea kupitia audiface jackson blogspot kupata habari kila siku..Aidha, Rais Kikwete amempandisha cheo Meja Jenerali Ndomba kuwa Luteni Jenerali.
Taarifa iliyotolewa , Ijumaa, Septemba 21, 2012, mjini Dar Es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Y. Sefue kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais – Ikulu, imesema kuwa uteuzi huo unaanza mara moja.
Taarifa hiyo ya Balozi Sefue imesema kuwa kabla ya uteuzi wake, Meja Jenerali Ndomba alikuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Jenerali Ndomba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Luteni Jenerali Abdulrahman  A. Shimbo ambaye amestaafu Jeshi kwa mujibu wa sheria baada ya kufikisha umri wa miaka 60.
            Taarifa ya Balozi Sefue pia imesema kuwa Rais Kikwete amemteua Brigedia Jenerali Raphael Mugoya Muhuga kuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa kuanzia leo, Ijumaa, Septemba 21, 2012. 
Aidha, Rais Kikwete amempandisha cheo Brigedia Jenerali Muhuga kuwa Meja Jenerali.
Kabla ya uteuzi wake, Brigedia Jenerali Muhuga alikuwa Mkuu wa Utawala na Mafunzo wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
21 Septemba, 2012

Diamond Platnumz: Nataka kutengenza ajira kwa vijana wenzangu

MSANII wa Kimataifa wa Tanzania, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ amesema amedhamiria kutoa ajira kwa vijana wengi wa kitanzania kupitia muziki huku pia akileta mapinduzi katika sekta hiyo nchini.
Diamond ambaye ni msanii ghali zaidi kwa sasa Tanzania, amesema kuna watu wengi wenye vipaji ambao wako mtaani au wako katika sekta nyingine lakini hawajui wafanyeje ili kufikia ndoto zao jambo ambalo linahitaji watu wengine wawasaidie kuwafikisha pale wanapotaka.
“Kuna tatizo ambalo lipo katika mambo ya mitindo, muziki. Watu wengi wanachukulia kama uhuni, wengi wanaona kama kuuza sura, yaani mtu aonekane kwenye video ili apate umaarufu, tunatakiwa kubadilisha mawazo haya, Ulaya hata hapo Afrika Kusini wanaonekana kwenye video wanalipwa.
“Mimi nitawalipa wote watakaonekana kwenye video yangu, tutakapofanya usaili kesho wale watakaochanguliwa watalipwa, lakini pia hii inaweza kuwa ni kufunguliwa milango kwenye sekta nyingine, wapo wanaoweza kuonekana wanafaa kwenye matangazo ya biashara, hawa watapata kampuni ambazo zinaweza kuwatumia.
“Katika majaji watakuwepo Raqey Mohammed wa I-View Studios, hawa wanafanya kazi nyingi za matangazo, movie, atakuwepo pia Ally Rehmtulah huyu ni mbunifu anaweza kumuona mtu na akasema huyu anafaa kwa sekta yake, Sammy Cool ni densa na mwalimu hata Missie Popular yeye ni mwandishi na mwanamitindo wanajua wapi kwa kuwafikisha watu wengine’ alisema.
Msanii huyo alisema mafanikio aliyo nayo ya kumiliki nyumba, magari na kujulikana kwake yametokana na muziki, hivyo ana uhakika wapo watu wengine pia kupitia yeye na wanamuziki wengine kama yeye wanaweza kufaidika na kufikia mafanikio kama aliyoyapata.
Diamond alisema usaili huo unafanyika kesho  pale nyumbani Lounge kuanzia saa tano asubuhi. Hii ni mara ya kwanza kwa msanii wa nchini kufanya usaili kwa ajili ya watu watakaonekana kwenye video yake.
Diamond pia ndiye msanii wa kwanza wa muziki wa kizazi kipya kuandaa shoo yake mwenyewe na watu kulipa kiingilio cha sh 50,000. Diamond alifanya hivyo kwenye onyesho alilolipa jina la Diamond are Forever pale Mlimani City, Dar es Salaam.

The Making of Music Video - YEYE by LADY JAY DEE at Lugalo Golf Club

USAHILI WA VIDEO MPYA YA DIAMOND UNAENDELEA NOW HAPA NYUMBANI LOUNGE


KUTOKA UJANATZ MAGAZETI YA LEO YA UDAKU,SIASA NA MICHEZO YA TAREHE 22/09/2012


.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.