Wednesday, February 13, 2013

.
Mgombea urais katika uchaguzi mkuu ujao wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema mashtaka yanayomkabili ya uhalifu dhidi ya binaadamu katika Mahakama ya uhalifu ya kimataifa ICC hayatomzuia kuiongoza nchini hiyo kama atachaguliwa kuwa rais.

Kenyatta ambae ni naibu Waziri Mkuu ameyasema hayo kwenye mdahalo wa kihistoria na wa kwanza kufanyika nchini Kenya kwa kuhusisha wagombea wote nane wanaoutaka urais.
.
Katika mdahalo huo ambao ulirushwa live na TV mbalimbali za ndani na nje ya Kenya, Waziri mkuu Raila Odinga anayepewa nafasi kubwa ya kushinda kwa mujibu ya kura ya maoni, amesema Kenya haiwezi kuongozwa na mtu alie mbali na Kenya ambapo wengi wanaamini hiko kilikua kijembe kwa Uhuru ambae anamashtaka The Hague.

Odinga alisema hiyo ishu itasababisha changamoto kubwa kwa serikali kuendeshwa kwa kutumia mtandao wa kijamii wa Skype kutokea The Hague iwapo rais atakaechaguliwa ni mwenye mashtaka The Hague.

Mdahalo mwingine kama huo utafanyika tarehe 25 february 2013 ikiwa ni wiki moja kabla ya uchaguzi mkuu March 4 2013.
Timu ya Taifa ya Nigeria ikiwasili Abuja Nigeria.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.