Thursday, August 23, 2012




 


MAGAZETI YA LEO IJUMAA TARHE 24/08/2012

 








HAWA NDIO WAREMBO WAWILI WA KENYA WALIOKUBALI MWALIKO WA KUPERFORM DAR JPILI HII.

Marya.
Avril na Marya ambao ni mastaa wa hit single ya ‘Chokoza’ wamekubali mwaliko wa kulimiki stage club Billicanas jumapili hii August 26 2012 kwenye Extreem Bash na itakua ni mara yao ya pili kuja kufanya show pamoja baada ya hiyo hit single ya ‘chokoza’.
Marya.

PICHA ZA TIMU YA YANGA IKIWA RWANDA.

Yanga ambao wako Rwanda kuweka kambi na kutii mwaliko wa Rais Paul Kagame pia, hapa ni walipokua wamekwenda kutembelea nyumba ya makumbusho ya waliouwawa katika mauaji ya kimbari mwaka 1994.
.
.
.
Hapa ni kwenye uwanja wa mazoezi nyuma ya Amahoro.
Picha zote zimepigwa na Saleh Ally wa gazeti la Champion.

Dr Dalaly Kafumu.

   Nafahamu kwenye vyombo vingi vya habari stori iliyochukua nafasi kubwa sana ni pamoja na hukumu iliyotolewa na mahakama iliyomuondoa kwenye ubunge aliekua mbunge wa jimbo la Igunga Dokta Dalaly Peter Kafumu.

Sasa stori mpya kuhusu hiyo hukumu imetoka kwa chama cha mapinduzi kwenyewe ambacho kimetefakari hukumu hiyo na kimejiridhisha kufanya uamuzi wa kukata rufaa kwa sababu haijaridhishwa.

Nape Nnauye ambae ni katibu wa halmashauri kuu ya CCM itikadi na uenezi amesema “tutakata rufaa kupinga uamuzi wa mahakama, hakuna kipya cha msingi ni kwamba tumeamua kukata rufaa, hatukuridhika na hoja zilizotumiwa na jaji kuutengua ushindi wa chama cha Mapinduzi na tunaamini kwenye rufaa tutashinda, hoja za Mahakama ni dhaifu sana”

MWAMVITA MAKAMBA ALA SHAVU LA KUHAMIA J’BURG-SOUTH AFRICA KIKAZI...!

Mwamvita Makamba

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Mwamvita aliandika yafuatayo;

"On the 1st of September 2012, I will officially start a new wave of my career in Johannesburg South Africa, at Vodacom Group. I have had a great time here at home, learnt a lot and grew tremendously personally and professionally.

Thanks to all of you for the support and encouragement as I went about my daily activities here. I will continue to keep in touch and keep sharing my various adventures whenever I go and get stories worth sharing with you. Remember, no matter who you are or where you come from, if you dare to dream, the world is truly your centre stage.
Love, Mwamvita"

Mwamvita alipokwenda kumuaga Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ofisini kwake.Picha kwa hisani ya Ofisi ya Waziri Mkuu

HAYA NDO MABASI YAENDAYO KASI YATAKAYOTUMIKA TANZANIA

 
 
HAYA NDO MABUS YANAYOENDA KASI KULIKO DUNIANI YANAITWA METROBUS
 project hii ilianza Netherland,then Turkey wakacopy,then germany na sasa hivi
Tanzanıa ndo wanatengeneza jijini Dar es salaam.

MCHAKATO WA SERENGETI FIESTA 2012 WAENDELEA KUPAMBA MOTO NDANI YA JIJI LA TANGA

 Mchakato wa Serengeti Fiesta 2012 ndani ya Tanga ukiendelea ndani ya mitaa kadhaa ya jiji hili. Mtangazaji wa Clouds Fm Adamu Mchomvu, hapa vijana wa kazi kutoka Clouds Fm wakiongea na wakazi wa eneo la Magaoni, Taili Tatu Kata ya Mabawa. Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika tarehe 26.8.2012 katika uwanja wa Mkwakwani.
 Mtangazaji wa Clouds Fm Adamu Mchomvu, akiyaendeleza mastori ndani ya kitaa cha Taili tatu eneo la Magaoni, Kata ya Mabawa, Tanga.
 Mwanadada Loveness Love akiwa na Gossip Cop Tz, Sudi Brown.
 ...Wakionyesha umahili wao wa kunwaga.
 ... aha... mimi ni msela siwezi kwenda jela...
 ... vijana walijitahidi kuonyesha umahili wao wa kuchana michano.
 ... Clouds Tv nayo haikukosa.
 Rasi akionyesha umahili wake wa  kuimba rege.
 Adamu Mchomvu akisababisha mambo.
 Gossip- Cop Tz Sudi Brown akiwa katika pozi.
 Mazungumzo ya mtaani yakiendelea.
 Mtangazaji wa Clouds Fm Adamu Mchomvu na Mwanadada Loveness Love.
 ...hata jamaa alikuwa akitiririka machache ndani ya Clouds Fm/Clouds TV.
 Producer wa Home record ya Tanga nae akimwaga madini.
 Show Love ikiendelea.
 Show love ndani ya eneo la Magaoni, Taili Tatu Kata ya Mabawa.

HAYA SASA MBUYI TWITE KASHADONDOKA YOUNG AFRICANS!

BEKI wa kimataifa wa mabingwa wa klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati ‘Kombe la Kagame’ Yanga,  Mbuyi Twite amejiunga na kikosi cha timu hiyo kilichopo  nchini Rwanda.
 Twite ambaye ameziingiza katika msigano timu za Simba na Yanga baada ya kusaini mkataba katika vilabu hivyo akianza Simba na baadaye
Yanga ambayo pia imeliwasilisha jina lake katika usajili wa wachezaji katika shirikisho la Soka Tanzania (TFF) alikuwa kwao Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kwa ajili ya kuiaga familia yake.
 Akizungumza  kwa simu kutoka Kigali nchini Rwanda, Mjumbe wa kamati ya Utendaji ya Yanga Abdallah Binkleb alisema kwamba Twite aliwasili huko jana na leo asubuhi alifanya mazoezi na wenzake katika uwanja wa Amahoro.
 Alisema kama mambo yakienda vema huenda nyota huyo aliyesajiliwa kutoka APR ya huko kesho atashuka  katika dimba la Amahoro akiwa ametinga uzi wa njano na kijani katika mchezo wao na Rayon utakaopigwa jioni.

MAGAZETI YA LEO AUG 23 NA STORI ZAKE KUBWA ZA HARDNEWS NA MICHEZO.

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
tena.
.
.