Friday, June 29, 2012

Wakijiji wajipanga kupambana kutetea haki yao, Waomba Serikali kuingilia kati
********************************
 WANAKIJIJI wa Kimbiji,Wilayani Temeke,nje kidogo ya jiji la Dar-es-salaam, maeneo ya Kigamboni, wamejipanga kupambana na

Askari wa Jeshi wanaokuwa wakifika katika maeneo yao na kuwasumbua wakiwataka kuhama katika maeneo hayo ambayo wao ni wakazi wa asili kwa muda mrefu sasa.


Wananchi hao ambao wamekuwa wakipata usumbufu na vitisho na kuharibiwa mali zao, Makazi na mazao yao,kutokana baadhi

wanajeshi hao ambao wanania ya kutaka kuyachukua maeneo ya wanakijiji wa Kimbiji kwa kutumia nembo ya Jeshi (JWTZ),kinyume cha sheria.


Wakizungumza na mtandao huu baadhi ya wanakijiji hao wamesema kuwa Kuanzia mwaka jana 2011 wanajeshi hao wamekua na tabia ya kuvamia mashamba na makazi ya wanakijiji Kimbiji na kuwanyanyasa huku wakiwataka wananchi hao kuyahama makazi yao huku vyombo vya dola vikiwa vimekaa kimya.


Wanakijiji hao wa Kimbiji wanalalamika kuwaona wanajeshi hao wakiwafanyia unyama na unyanyasaji.bila kujali utu.


Aidha imeelezwa kuwa kuna baadhi ya wanajeshi wamekuwa wakitumia Baru zenye Nembo ya Jeshi na kuzipeleka kwa katika Ofisi ya Serikali ya Kijiji na kutoa vitisho kuwa barua hizo zimetoka Wizarani zikiwataka wananchi kuyahama makazi yao.

 
Wakilalamika Wanakijiji hao wa Kimbiji,wilayani Temeke,Dar-es-salaam, wamesema kuwa hawajawahi hata siku moja kua wala kukaa kikao na serikali au wizara ya Ardhi ili kujulishwa hali halisi ya tukio hilo na kuiomba Serikali kuingilia kati ili kuepusha vurugu zinazoweza kutokea.
 
Kwa maelezo zaidi wasiliana na Uongozi wa Kijiji,Diwani simu Na. 0713768082
Mwenyekiti: Simu namba 0713846688

No comments:

Post a Comment