Friday, June 29, 2012

NEWS ALERT: Waziri wa Habari,Vijana Utamaduni na Michezo apata ajali mbaya maeneo ya Nzega Mkoani Tabora mchana huu.

Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Mh.Dkt. Fenella Mukangara (pichani) amepata ajali mbaya mchana huu maeneo ya Nzega Mkoani Tabora wakati akiwa njiani kuelekea Jijini Mwanza kwenye Ufunguzi wa Mashindano ya Taifa ya Mchezo Vishale (Darts) yanazinduliwa leo Jijini humo.

Globu ya Jamii imefanya mawasiliano na Mh. Mukangara na kuthibitisha kupata ajali hiyo ambapo anasema chanzo chake ni kuchomekewa na basi moja la abiria (ambalo hakulitaja jina lake).

"Ni kweli tumepata ajali hapa maeneo ya Nzega Mkoani Tabora wakati tukiwa njiani kuelekea jijini Mwanza ambako leo kunafanyika ufunguzi wa Mashindano ya Taifa ya Mchezo wa Darts,tunashukuru Mungu wote tumetoka salama japo tumepata majeraka katika sehemu mbali mbali za mwili."Alisema Mh. Mukangara.
Tunaendelea kuwasiliana na Mh. Mukangara na tutaendelea kupeana taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment