Wednesday, June 27, 2012

DK. STEVEN ULIMBOKA AOKOTWA MABWEPANDE AKIWA AMEPIGWA MAPANGA


Habari zilizotufikia hivi punde zimeeleza kuwa Kiongozi wa mgomo wa madaktari Bw. Steven Ulimboka ameokotwa maeneo ya Mabwepande akiwa amepigwa mapanga na hali yake ikiwa ni mbaya  Fullshangwe imepata habari kuwa kulikuwa na gari lililokuwa likipeleka katika hospitali ya TMJ Mikochezi na lilipofika hapo walimhamishia kwenye Ambulance na kumuwahisha hospitali ya Muhimbili kitengo cha mifupa Moi kwa matibabu.

Fullshangwe imewasiliana na Kamanda wa polisi mkoa wa Kinondoni Kamanda Kenyela hata hivyo ilipokelewa na msaidizi wake ambaye amesema Kamanda Kenyela amebanwa sana na kazi hivyo tumpigie baadae anaweza kuwa na muda mzuri wa kulizungumzia suala hilo, Haijafahamika bado kama wahusika wa shambulio hilo ni akina nani na tutaendelea kuwataarifu kadiritutakavyopata taarifa

No comments:

Post a Comment