Tuesday, June 26, 2012

.
Rapper Suma Mnazareth ametangaza kujiunga na Dogo Janja kwenye list ya wasanii waliochini ya uongozi wa kundi la WATANASHATI lililomrudisha Dogo Janja kutoka Arusha wiki iliyopita.
Suma amesema “sababu iliyonifanya niingie Watanashati ni kwamba nimekaa nje ya uongozi kwa muda wangu wote wa Muziki kwa zaidi ya miaka mitatu, nimekua ni mtu ambae nafanya maamuzi mwenyewe kuanzia kwenye kurekodi nyimbo mpaka kusimamia kazi zangu bila usimamizi wa mtu mwingine, hilo ndio naona limekua likinicheleweshea malengo yangu niliyoyapanga kwenye muziki”
“Mimi ndio niliwafata WATANASHATI kwa sababu nilishajifunza kwamba niko kwenye kutafuta maisha na kutafuta inabidi ujue hata kama una vyeti inabidi upeleke vyeti vyako ofisini ili uajiriwe so mimi ndio nikamtafuta meneja Ostaz Juma”

No comments:

Post a Comment