Tuesday, June 26, 2012

Hoja ya haja kuhusu ukweli wa ukumbi wa wanahabari Bungeni Dodoma

 
Mpaka sasa ni wapiganaji wachache waliopo ukumbi wa waandishi wa habari, wengine wameendelea kubanana chini na ni fujo tu na wanachokifanya hakuna. chombo kimoja wapo 4 sasa sijui wote wanaandika kipindi cha maswali na majibu? 
 
Unajua kama mtu huna historia na swala la waandishi wa Bunge ni bora ukanyamaza, labda manyerere amesahahu swala la ukumbi wa waaandishi wa habari Bungeni lilivyokuwa. Nimekua nikija kuandika habari Bungeni na najua historia ya Ukumbi wa Waandishi wa Habari, Jengo hilo la kisasa limejengwa kwa kuzingatia mahitaji ya kila mtu, waandishi wa habari ukumbi wao upo juu na una mpaka vimeza vya kisasa vya kuwawezesha kuandika vizuri, lakini cha kushangaza wakati wa Mhe. Sitta akiwa Spika, mmoja wetu akaleta hoja na kutu Convince waandishi wenzie ili tuhamishiwe gallery ya maafisa wa serikali (sehemu ambayo ni ndogo kuliko tulipotengewa awali) kwa madai eti tuwe karibu sana na vioo kupenyeza vimemo kwa wabunge.... tukashauriwa udogo wa eneo wenzetu wakadai panatosha.. enzi hizo tulikuwa  tukifika bungeni waandishi takribani 15 hadi 30.   
 
Sasa mkutano huu wa Bunge tupo waandishi wa Habari zaidi ya 90 kutoka, kila aina ya vyombo vya habari na  blogs, na kila mmoja wetu anang'ang'ana kukaa pale chini tulipojazana eti kuchati huku gallery ya juu ambayo ni hasa iliyo designiwa kuwa press kukiwa empty!!! Ndio maana kelele haziishi na kila saa watu wanapiga story badala ya kufanya kazi. leo hii madai kuwa  tunanyanyaswa  sio kweli tuliyataka wenyewe na kwa kuwa kila mtu anania yake tofauti hata uandishi wetu sasa umekuwa full magumashi tu ..... Jamani manyerere ungeuliza wakongwe kabla hajapiga picha. 
 
Penye ukweli tusifie jamani jengo lilijengwa kwa kukidhi mahitaji, sehemu yetu ipo tuliikataa wenyewe…. Tusiwe domo kayaaaa jama. Kwa kuwa nipo hapa, nakuletea fotooz za ukumbi wetu  na jinsi palivyo empty huku watu wamejazana hapo chini.

Mwandishi Mzalendo, Bungeni

No comments:

Post a Comment