Wednesday, June 27, 2012



.

Uokoaji umetarajiwa kuanza tena leo huko mashariki mwa Uganda ambako vijiji vitatu vilifunikwa na udongo kutokana na maporomoko ya udongo.


Shirika la msalaba mwekundu Uganda limesema zaidi ya watu 18 wamefariki dunia katika maporomoko hayo.


BBC wameandika kwamba zaidi ya nyumba kumi na tano zimefunikwa  kutokana na mvua kubwa.


Hata hivyo bado waliojeruhiwa kwenye eneo hilo wanaendelea kutibiwa baada ya kilichotokea kwenye eneo hilo lenye rutuba la Bududa, linalokuza kahawa na lililopo karibu na mbuga ya wanyama ya mlima Elgon.

No comments:

Post a Comment