Thursday, October 11, 2012

Timbulo ‘Bado kijana’


NYOTA wa muziki wa kizazi kipya nchini, Ally Timbulo ‘Timbulo’ anajipanga kuachia wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la ‘Bado Kijana’.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Timbulo alisema yupo katika hatua za uandaaaji wa kibao hicho ambacho anatarajia kukiingiza sokoni mwanzoni mwa mwezi Novemba.

Mbali na kibao hicho, Timbulo anawataka mashabiki wake wakae mkao wa kula kuna tukio kubwa ambalo amewaandalia kwa lengo la kuwapa burudanni mashabiki wake.

“Mwishoni mwa mwaka huu nimejipanga kuwapa burudani mashabiki wangu, hivyo nipo kwenye mchakato wa kuandaa shoo hiyo ambayo natarajia itakuwa kama Surprise,” alisema Timbulo.

Licha kutaka kutoka na kibao hicho, Timbulo alishawahi tamba na vibao vyake kama Samsoni na Delila, Timbulo wa leo na nyinginezo ambazo zilimtambulisha na kufanya vizuri katika  vituo mbalimbali vya reduo na runinga.

No comments:

Post a Comment