Tuesday, October 2, 2012

.
Mwandishi Shaffih Dauda ameripoti kwamba licha ya kushika nafasi ya pili kutoka mkiani ikiwa na pointi mbili tu baada ya kufungwa mechi mbili na kutoka sare mechi mbili, Timu ya Polisi Moro ni moja ya timu zenye ukuta mgumu zaidi VPL ikiungana na JKT Oljoro, Simba na Azam FC ambazo kwa pamoja zimeruhusu magoli mawili tuu kutinga kwenye nyavu zao.

Azam FC ndiyo timu pekee ambayo imeruhusu magoli kuingia kwenye mechi moja tuu baada ya kukubali kutoka sare 2-2 na Toto Afrika jijini Mwanza huku ikiwa imeondoka bila kuruhusu nyavu zake kutikiswa kwenye mechi tatu za ligi kuu.

Hadi kufikia raundi ya nne, Simba SC ndiyo timu pekee ambayo haijapoteza pointi hata moja baada ya kucheza michezo minne na kushinda yote ambapo polisi Moro imejiwekea rekodi nyingine kwenye VPL raundi ya nne baada ya kuwa timu pekee iliyocheza mechi nne bila kufunga goli hata moja.
.
Hadi kufikia raundi ya nne ya ligi kuu ya Vodacom, kuna vilabu vinne tu ambavyo havijaruhusu kupoteza mchezo hata mmoja hadi sasa, vilabu hivyo ni Toto Africa, JKT Oljoro, Coastal Union, Simba SC na Azam FC.

JKT Ruvu Stars ndiyo iliyoruhusu magoli mengi zaidi ya kufungwa ikiwa imefungwa magoli 10 hadi sasa ikifuatiwa na ndugu zao wa Ruvu Shooting Stars walioruhusu magoli nane kama ilivyo kwa wapiganaji wa African Lyon.

Kwa upande wa magoli klabu ya Simba ndio inayoongoza ikiwa na magoli tisa na kufuatiwa na Azam FC na Yanga pia yenye magoli saba huku vilabu vya Ruvu Shooting Stars na Mtibwa Sugar vikiwa vimetikisa nyavu mara sita kila kimoja. 

Wachezaji Kipre Tchetche wa Azam FC na Husein Javu wa Mtibwa na Nizar Khalfan ndiyo wanaoongoza kufunga magoli kwenye ligi kuu wakiwa na magoli matatu kila mmoja hadi hivi sasa.

Kwa stories zaidi chek na shaffihdauda.com

No comments:

Post a Comment