Tuesday, October 16, 2012

.
Kanisa la  Pentekoste (MMPT) lililopo Buronge katika Manispaa ya Kigoma/Ujiji limechomwa moto na kuteketezwa kabisa na watu wasiojulikana.

Uchomaji wa Kanisa hilo umeleta hofu kwamba huenda chuki za kidini na uchomaji wa makanisa ukazidi kuenea Tanzania.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma Frasser Kashai amesema hilo tukio lilitokea juzi usiku saa nne ambapo mali mbalimbali zenye thamani ya Shilingi milioni moja laki tatu na elfu thelathini na saba ziliteketea.

Sababu za kuchomwa kwa kanisa hilo hazijafahamika na wala hakuna mtu aliyejeruhiwa lakini upelelezi unaendelea  ili kuwapata waliohusika.

No comments:

Post a Comment