Thursday, October 11, 2012

Tanga.
Serikali kwenye mkoa wa Tanga 96.0 imesema itafanya kila linalowezekana kuhakikisha inavunja vitendo vinavyoendelea vya mauaji ya raia kwenye mkoa huo.

Jumla ya watu 11 wameripotiwa kuuwawa kikatili kuanzia septemba 1 mpaka septemba 28 mwaka huu kutokana na sababu mbalimbali kama za kishirikina, sheria mikononi, wivu wa kimapenzi na ujambazi.

Oktoba 8 mwaka huu mlinzi wa kampuni ya Mult System ametekwa na hajulikani alipo mpaka sasa, alitekwa wakati akiwa lindoni kwenye ofisi za halmashauri ya wilaya ya Mkinga ambapo baada ya kutekwa majambazi yalifanikiwa kuiba gari aina ya Landcruiser tukio ambalo lilithibitishwa na Kamanda wa polisi Tanga Costantine Massawe.

Mkuu wa mkoa wa Tanga luteni mstaafu Chiku Galawa amesema jeshi la polisi kwa ujumla halijashindwa kukanbiliana na mauaji hayo ambayo amesema yanauchafulia jina mkoa wa Tanga.

No comments:

Post a Comment