Wednesday, October 10, 2012

AIRTEL YATEMBELEA  WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUMU WA UHURU MCHANGANYIKO

 Afisa uhusiano na matukio  wa Airtel  Dangio Kaniki akiwapatia chai watoto shule ya Uhuru Mchanganyiko wakati Airtel ilipotembelea shule hiyo  itakayofaidika na mpango maalumu wa  Airtel kwa kushirikiana na BAMVITA wenye lengo la kuchangia vitabu kwa watoto wenye mahitaji maalum .  Airtel imeanza kutembelea shule zilizopo Dar es Salaam pamoja na mikoani na kubainisha matatizo wanayokumbana nayo ili kuona namna ya kuwasaidia watoto hao wenye mahitaji maalum. 

Airtel Communication and event officer Dangio Kaniki serve breakfast to Uhuru Mchanganyiko children during Airtel visit to school yesterday; the school is one of the beneficiaries of the project launched by Airtel in partnership with BAMVITA aiming to facilitate teaching aids to students with special needs. Airtel has started visiting school in Dar and upcountry to realize their need and mobilize funds to support children with special needs.
 Meneja huduma za jamii wa Airtel Hawa Batuli (katikati)akiongea na mwalimu mkuu wa shule ya Uhuru Mchanganyiko Anna Mang'enya wakati Airtel ilipotembelea shuleni hapo jana. Airtel imeanza kutembelea shule zilizopo Dar es Salaam pamoja na mikoani na kubainisha matatizo wanayokumbana nayo ili kuona namna ya kuwasaidia watoto hao wenye mahitaji maalum.  Kushoto ni Afisa uhusiano na matukio  wa Airtel  Dangio Kaniki.

Airtel Social Responsibility Manager Hawa Batuli(middle) speaks to Uhuru Mchanganyiko school Head teacher during Airtel visit to the school, Airtel has started visiting school in Dar and upcountry to realize their need and mobilize funds to support children with special needs. On the left is Airtel Communication and event officer Dangio Kaniki
 Afisa uhusiano na matukio  wa Airtel  Dangio Kaniki akinywa chai pamoja na watoto wa shule ya Uhuru Mchanganyiko wakati Airtel ilipotembelea shule hiyo  itakayofaidika na mpango maalumu wa  Airtel kwa kushirikiana na BAMVITA wenye lengo la kuchangia vitabu kwa watoto wenye mahitaji maalum .  Airtel imeanza kutembelea shule zilizopo Dar es Salaam pamoja na mikoani na kubainisha matatizo wanayokumbana nayo ili kuona namna ya kuwasaidia watoto hao wenye mahitaji maalum. 

Airtel Communication and event officer Dangio Kaniki having  breakfast with Uhuru Mchanganyiko children during Airtel visit to the school yesterday; the school is one of the beneficiaries of the project launched by Airtel in partnership with BAMVITA aiming to facilitate teaching aids to students with special needs. Airtel has started visiting school in Dar and upcountry to realize their need and mobilize funds to support children with special needs.
Meneja huduma za jamii wa Airtel Hawa Batuli (kushoto) akimshukurua mwalimu mkuu wa shule ya Uhuru Mchanganyiko Anna Mang'enya kwa kuwapokea walipotembelea shule hapo ambapo Airtel imeanza kutembelea shule zilizopo Dar es Salaam pamoja na mikoani na kubainisha matatizo wanayokumbana nayo ili kuona namna ya kuwasaidia watoto hao wenye mahitaji maalum.  Kushoto ni Afisa uhusiano na matukio  wa Airtel  Dangio Kaniki .Airtel Social Responsibility Manager Hawa Batuli(middle) shake hands thanking Uhuru Mchanganyiko school Head teacher for hosting Airtel visit to the school, Airtel has started visiting school in Dar and upcountry to realize their need and mobilize funds to support children with special needs. On the left is Airtel Communication and event officer Dangio Kaniki.

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imewahimiza watanzania kuendelea kuchangia katika mradi wa kuchangia vifaa kwa ajili ya watoto wenye mahitaji maalum unaoendeshwa na Kampuni ya Airtel kwa kushirikiana na  Baraza la maendeleo ya vitabu Tanzania (Bamvita)

Afisa uhusiano na matukio wa Airtel Dangio Kaniki amesema kampuni hiyo ikiwa na Balozi wake, AY imeanza kutembelea shule zilizopo Dar es Salaam pamoja na mikoani na kubainisha matatizo wanayokumbana nayo ili kuona namna ya kuwasaidia watoto hao wenye mahitaji maalum. Airtel inaamini kwamba watoto hao wenye mahitaji maalum wakiwezeshwa kielimu wataweza kutimiza ndoto zao na kuchangia katika maendeleo ya kiuchumi nchini.

Akiongea wakati walipotembelea shuleni hapo Meneja huduma kwa jamii Hawa Bayumi alisema ” Ni matumaini yetu kuwa watanzania na wale wasio watanzania kwa ujumla wataendelea kutuunga mkono ili kuweza kutimiza lengo hili la awali na kisha kuongeza shule za mikoani mara baada ya kukamilisha mahitaji haya katika shule hizi za Dar es Salaam. Kampeni hii itaendeshwa kwa muda wa miezi mitatu , na watanzania wanaweza kuchangia kwa kutuma neno “Vitabu”  kwenda namba 15626  na utakuwa umechangia shilingi 200 katika mradi huu au kupitia Airtel Money unapiga *150*60# ingiza jina la biashara VITABU na kuchangia kiwango chochote kile. Tunachukua fulsa hii  kuwaomba  watanzania wote kuchangia ili kuwafikia watoto wengi zaidi nchin”
Nae Mwalimu Mkuu wa shule ya Uhuru Mchanganyiko Anna Mang'enya amesema “shule hiyo inakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo uhaba wa vifaa vya kufundishia. bila vifaa hivyo maalum itakuwa vigumu kwa wanafunzi kutimiza ndoto zao zakuendelea kielimu”.

Aidha Ameishukuru Airtel na BAMVITA kwa kuweza kuanzisha mradi huu na kuweza kuwahamasisha watanzania kuchangia ili waweze kupata vitendea kazi  na kuongeza kuwa shule hiyo bado inakabiliwa na changamoto nyingi katika elimu hivyo kuiomba kampuni hiyo kuendelea kuisaidia katika mambo mengine.
  Zena Yahaya Mwanafunzi Uhuru Mchanganyiko alikuwa na haya ya kuongeza “tunawashukuru Airtel kwa kuja kututembelea leo, tunawaomba watanzania wote waendelee kutusaidia kwa kushirikiana na Airtel  katika mradi huu wa Vitabu ili kuweza kutusaidia katika kununua vifaa vya kutusaidia hapa shuleni na kuhakikisha tunapata elimu bora.”

Airtel inatambua umuhimu wa Elimu na tunaamini Tanzania itajengwa na sisi wenyewe hivyo basi lengo la  mradi huu ni kutoa nafasi kwa jamii yetu kuweza kuchangia elimu  ya msingi kwa watoto wenye mahitaji maalum kwa kuwanunulia vitabu na nyenzo za walimu kufundishia. Kwa kuanzia tumeanza kutembelea shule mbili za jijinini Dar es Salaam zitafaidika na mpango huu ambazo ni Sinza Maalum, Uhuru Mchanganyiko ikifuatiwa na Buguruni Viziw.

No comments:

Post a Comment