Thursday, October 4, 2012

RAIS WA IBF AZITEMBELEA OFISI ZA DHL DAR-ES-SALAAM!

Pichani Ngowi mwenye miwani akiwa amesimama na wafanyakazi wa DHL! Picha Imetumwa  na (Uongozi IBF).
Kampuni ya kusafirisha vifurushi ya DHL inatoa punguzo kwa kusafirisha vifurushi katika promosheni yake inayoendelea sasa!
Hayo yalibainishwa wakati Rais wa IBF Afrika, Masharikiu ya Kati, Ghuba ya Uarabu na Uajemi Onesmo Alfred McBride Ngowi alipotembelea ofisi zao leo katika jengo la Peugeot . jijini Dar-Es-Salaam na kupiga picha na wafanyakazi wa DHL.
Ngowi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Baraza la Ngumi la Jumuiya ya Madola (CBC), Rais wa Shirikisho la Ngumi la Afrika ya Mashariki na Kati (ECAPBA) na Rais wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC) alifurahishwa sana na huduma wanazotoa DHL na kuwahimiza wafanyakazi wake waendelee na kutoa huduma hizo nzuri!

No comments:

Post a Comment