Monday, October 15, 2012

1. Hii hoteli inaitwa Singita Serengeti The Grumeti Reserves Tanzania na ipo Serengeti, ni hoteli ambayo ndani yake ina lodge 2, camp 1 na house 1 na zote ziko mbalimbali kidogo.

2.Mpaka sasa ni hoteli ambayo mastaa kadhaa wa dunia na matajiri wameshakuja kama Bill Gates, Bill Clinton na mkewe na wengine.

3. Mmiliki wa hii hoteli ni Mmarekani Paul Tudor Jones ambae aliwahi kutoka kwenye list ya matajiri Wamarekani ndani ya jarida la Forbes, kwenye hii hoteli anashea na Luke Bailes.

4. Hii ni Lodge inaitwa Sasakwa ambayo ndio waigizaji mastaa Angelina Jolie na Brad Pitt walifunga ndoa iliyoshuhudiwa na ndugu zao wachache waliokuja nao, siku hiyo Kamera hazikuruhusiwa kabisa kwa mtu yeyote na wala watu hawakutakiwa kusogelea kabisa.

5. Hii hoteli ndio ilitangazwa kuwa namba 1 duniani kati ya hoteli 100 zilizoshindanishwa.

6.Bei ya chini kulala kwenye moja kati ya hizi hoteli ni dola za kimarekani 1050.

7.
8.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
Usafiri huu unapatikana na unatumika kwa kiasi kikubwa. 
(Kwa Hisani ya: millardayo.com)

No comments:

Post a Comment