Tuesday, October 16, 2012

Uwanja wa Nyamagana.

Wakati wa kumuaga Liberatus Barlow aliyekua kamanda wa polisi mkoani Mwanza ambae aliuwawa weekend iliyopitwa kwa kupigwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi ambao walipokutana nae walijifanya polisi wa doria, Mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai nchini (DCI) Robert Manumba amesema polisi wa Mwanza wawe watulivu kwenye kipindi hiki kigumu lakini ni lazima walipe kisasi kwa kuwakamata waliohusika.

Namkariri akisema “nawaombeni tuendeleze utulivu lakini tuhakikishe kwamba tunalipa kisasi cha tukio hili la kikatili kwa kuwakamata waliohusika, hatutalala tutaendelea kuwa na ninyi na kwa kweli kama tunavyokabiliana na uhalifu wowote, auliwe mwananchi wa kawaida, afisa, kiongozi… ni kifo lazima kishughulikiwe”
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo amesema mazingira ya kuuwawa kwa Kamanda Barlow bado hayajawa wazi, alipofika kwenye eneo alilouwawa usiku kati ya saa saba na saa nane akasimama na kuegesha gari kama kawaida na kumteremsha huyo dada yake, ghafla mbele yake wakajitokeza watu wawili ambapo Kamanda alipoona kama kuna mazozo ikabidi awaulize wale jamaa akisema hamnijui? waliporushiana maneno sana ikabidi achukue radio ili kuwasiliana na polisi ambapo kabla ya kufanya hivyo ndio alipigwa risasi.

Namkariri mkuu wa mkoa akisema “amepigwa risasi kutokea mlango wa abiria kwa sababu risasi imepigwa begani na kutokea kwenye maeneo ya shingoni”
.
.
.
.
.

No comments:

Post a Comment