Thursday, October 11, 2012

RICK ROSS AFANYA KWELI MPAKA BHAAAAS


Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti SBL Bw Ephraim Mafuru akitangaza mshindi wa bahati nasibu ya magari mawili kwa mkoa wa Dar es salaam iliyoendeshwa katika matamasha yote ya Serengeti Fiesta mwaka huu kutoka kulia ni Bw. Mrisho kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha , Rugambo Rodney Meneja masoko wa Push Mobile na kushoto ni Mkurugenzi wa Clouds Entarteinment Bw Joseph Kusaga wakishuhudia tukio hilo.


Mtu mzima Rick Ross “The Boss” kutoka nchini Marekani hivi sasa yuko jukwaani kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2012 linalofanyika kwenye viwanja vya Leaders Kinondoni jijini Dar salaam ,anakamua ile mbaya na mashabiki wamepagawa vyakutosha kwa kila anachowaelekeza kufuata wanafuata jamaa amefunika mbaya, hiii ni mara yake ya kwanza kufanya onesho nchini Tanzania.


Rick Ross akiendelea kupagawisha mashabiki wake usiku huu kwenye viwanja vya…





Rick Ross akiendelea kupagawisha mashabiki wake usiku huu kwenye viwanja vya Leaders.


Watu wa usalama wakijaribu kudhibiti rapsha zilizokuwa zikijitokeza  kutokana na mashabiki wengi kuwa na hamu ya kumuona mwanamuziki Rick Ross.


Bibi Cheka na Stiko kutoka pande za TMK nao wakafanya mambo makubwa,



Pichani chini na juu mashabiki wakishangilia kwa nguvu wakati wanamuziki huyo akiimba jukwaani.


Rachel Mwanamuziki wa Bongofleva kutoka kundi la THT akicheza na mmoja wa wacheza shoo wake  katika Tamasha la Serengeti Fiesta linalofanyika usiku kuu kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam ambapo pamoja na wasanii mbalimbali wakali wa nyumbani, mwanamuziki maarufu wa Hiphop kutoka nchini Marekani Rick Ross “The Boss” atahitimisha tamasha hilo kwa shoo kali usiku huu.


zamu ya Lina wa THT akiwa jukwaani akiimba wimbo wake wa nampenda ambao umewafanya mashabiki wa muziki kuitikia kwa nguvu wakati akiwaimbisha hapa akipozi kwa staili ya aina yake huku akiwaimbisha mashabiki wake.


Mtangazaji wa Clouds kipindi cha Amplifire Milad Ayo kulia akipozi kwa picha na mdau kutoka Gazeti la Babkubwa .


Kutoka kushoto ni Rachel, Lina na Daina wote kutoka THT wakiwa tayari kwa kazi ya kuburudisha mashabiki wa Tamasha la Serengeti Fiesa 2012.


Michael Jackson wa Bongo akifanya vitu vyake mbele ya mashabiki wake alivuta hisia za wengi kutokana na kuigiza uchezaji wa marehemu Michael Jackson wa Marekani, pichani ni nyomi ya mashabiki waliojitokeza katika tamasha hilo kwenye viwanja vya Leaders

No comments:

Post a Comment