Tuesday, July 24, 2012

ZI WAPI TAA ZA KUONGOZEA MAGARI BARABARA YA NYERERE NJIA PANDA YA KEKO?

Ni kama kipindi cha wiki kadhaa sasa eneo hili limekuwa na Taa zinazoruhusu magari ya pande tatu tu huku upande wa taa zinazoruhusu magari yanayotoka Posta yaani yale yanayoelekea Airport hazionekani sasa haikuweza kufahamika kuwa zimeondolewa ama zimegongwa ama kimetokea nini hadi kutokuwepo kwa taa hizo kama ilivyozoeleka. Mogari yayotokea pande tatu za Karume, Keko na Airport yataongozwa na taa vipi yatokayo Posta?? Au hadi litokee la kutokea??

UJENZI WA BARABARA YA BAGAMOYO UNAENDELEA KWA KASI

 Mafundi wa ujenzi wa Barabara ya Bagamoyo, wakiendelea na shughuli ya kuimarisha eneo la Daraja linalojengwa eneo la Bondeni Kawe ambapo kwa sasa tayari sehemu za daraja hilo zimeshaanza kuunganishwa huku magari pia nayo yakitumia sehemu ya barabara mpya wakati ile ya zamani ikibomolewa na kujengwa upya.
 
 Sehemu ya ujenzi wa daraja hilo likifungwa vyuma kwa ajili ya kuanza kuunganishwa.
 
Foleni kubwa ya magari mida ya asubuhi na jioni katika maeneo yote unapoendelea ujenzi huo kuanzia Mwenge.

No comments:

Post a Comment