Monday, July 30, 2012

MWENGE YATWAA KOMBE LA POLISI JAMII WILAYA YA KIPOLISI KINONDONI

Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kinondoni,(SSP)Willbrod Mutafungwa akisom risala mbele ya mgeni rasmi Naibu meya wa manispaa ya Kinondoni Songoro Mnyonge, wakati wa kufunga michezo ya Polisi jamii katika wilaya ya Kipolisi Kinondoni juzi. (Picha na Abdallah Khamis)

Na Abdallah Khamis

TIMU ya Polisi Jamii Mwenge, juzi ilijinyakulia zawadi ya shilingi milioni moja, kikombe pamoja na jezi seti moja baada ya kuibamiza timu ya Polisi jamii ya Mwananyamala Kisiwani kwa bao 1-0, katika fainali ya Polisi Jamaii wilaya ya Kipolisi Kinondoni mchezo uliofanyika katika uwanja wa Biafra.

Katika michuano hiyo iliyoanza julai 9 mwaka huu,mshindi wa pili timu ya Polisi jamii Mwananyamala kisiwani ilijinyakulia sh.500,000, jezi pamoja na Kikombe huku timu ya Polisi jamii Kinondoni muslim ikijipatia zawadi ya Sh.250,000 kwa kuwa washindi wa tatu

Akikabidhi zawadi kwa washindi mgeni rasmi katika fainali hizo Naibu meya wa manispaa ya Kinondoni Songoro Mnyonge, alisema watahakikisha michezo hiyo inakuwa endelevu kwa manispaa kushirikiana na jeshi la polisi pamoja na wadau wengine ili kuwafanya vijana waepukane na uhalifu

Mnyonge alisema malengo ya mashindano yamefikiwa  kwa kiasi kikubwa kwa kuwa vijana wa kata zote katika wilaya ya kipolisi Kinondoni, walipatiwa elimu  ya kuachana na madawa ya kulevya namna ya kutoa taarifa za kuzuia uhalifu pamoja na kuachana na dawa za kulevya katika siku zote za mashindano.

Kwa upande wake mkuu wa polisi wilaya ya Kipolisi Kinondoni Willbrod Mutafungwa alisema timu zilizoshiriki zilikuwqa 14 kutoka katika kata nane za wilaya hiyo.

Mutafungwa ambaye pia ndiye alikuwa mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya michezo hiyo alisema kwa kuwa ni mar ya kwanza kwea michezo hiyo kusimamiwa na wilaya yake Kipolisi watahakikisha mapungufu yaliyojitokeza hayajirudii pindi watakapoandaa michezo hiyo kwa wakati mwingine.

No comments:

Post a Comment