Monday, July 23, 2012

ABIRIA WATUMIAO MELI WAKABIDHIWE TIKETI NA 'LIFE JACKET' KWA PAMOJA DIRISHANI?

KUTOKANA na ajali za mara kwa mara za Meli na boti za kusafirishia abiria, sasa kuna umuhimu wa kila abiria anayekata tiketi dirishani apewe tiketi pamoja na kifaa cha kuokolea maisha, 'Life Jacket'? kwa pamoja ili kupunguza longolongo za wenye vifaa hivyo kutoa visingizio pindi zitokeapo ajali kuwa vifaa vilikuwapo bali abiria hawakuvitumia?

Labda hii itasaidia kuokoa maisha ya watu wengi pindi zinapotokea ajali kama hizi zilizokwishatokea na pia itasaidia kuwafanya wahusika kubeba abiria idadi sawa kulingana na uwezo wa Meli na idadi ya vifaa vilivyopo, hii mnaionaje wadau?

Tena Abiri inabidi uwe mkali pale dirishani wakati ukipewa tiketi yako usipopewa life jacket, unahoji ''Vipi mbona hamnipi na Life Jacket''?.

No comments:

Post a Comment