Tuesday, July 24, 2012

UJENZI WA BARABARA YA BAGAMOYO UNAENDELEA KWA KASI

Mafundi wa ujenzi wa Barabara ya Bagamoyo, wakiendelea na shughuli ya kuimarisha eneo la Daraja linalojengwa eneo la Bondeni Kawe ambapo kwa sasa tayari sehemu za daraja hilo zimeshaanza kuunganishwa huku magari pia nayo yakitumia sehemu ya barabara mpya wakati ile ya zamani ikibomolewa na kujengwa upya.* ** * Sehemu ya ujenzi wa daraja hilo likifungwa vyuma kwa ajili ya kuanza kuunganishwa.* ** *Foleni kubwa ya magari mida ya asubuhi na jioni katika maeneo yote unapoendelea ujenzi huo kuanzia Mwenge.*

No comments:

Post a Comment