Monday, July 23, 2012

Milovan aipa Simba siku 30



KOCHA wa Simba, Milovan Cirkovic, amesema kikosi chake kinahitaji siku 30 ili kiwe tayari kwa ajili ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara. 
Kauli hiyo ya Milovan, raia wa Serbia, inakuja kufuatia kikosi chake kuanza vibaya katika michuano ya Kombe la Kagame, ingawa kimefanikiwa kutinga katika hatua ya robo fainali.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Milovan alisema wachezaji wake hawakuwa tayari kwa michuano ya Kagame na anahitaji muda ili kuweza kutengeneza timu ambayo itakuwa tishio katika michuano ya ndani na nje ya nchi.

Milovan alisema haogopi kauli za watu wanaoibeza timu yake kwa kuwa anajua kile atakachokifanya ili kuhakikisha kikosi hicho kinatisha.
 
“Kama nilivyokuwa nasema siku zote, Kombe la Kagame halikuwa katika programu zangu, ili Simba iwe tayari inahitaji muda wa siku 30. 
“Muda huu unatosha kuifanya timu ipambane na iwe na uhakika wa kuweza kushiriki kombe lolote,” alisema Milovan.

No comments:

Post a Comment