Sunday, July 29, 2012

Tanzanite.
Tanzania ilimfahamu msanii anaitwa Tanzanite baada ya kuanza kuimba juu ya beat za nyimbo za Diamond Platnums kwa kutumia melody ile ile kasoro mashairi tu, kitu ambacho pia alikua akikifanya bila ruhusa ya Diamond na kilishawahi kuleta ugomvi kati yao.
Baada ya kukaa kwa muda, Tanzanite ametangaza msimamo wake wa sasa kwenye maisha ya sanaa.

Amesema “sasa hivi sikopi tena nyimbo za wasanii wengine, kuna ngoma nimefanya na Kitale inaitwa Namwaga radhi na hapa nipo kwenye mazoezi niko na dancers wangu kwa ajili ya kufanya kitu cha ajabu, mwezi wa Ramadhani ukiisha watu watarajie”

Tanzanite ambae ana kesi ya ubakaji iliyomfanya awekwe segerea kwa miezi miwili kabla ya kupata dhamana, amesema “sitamani sana kukopi natamani kuonyesha uwezo wangu japo kuonyesha uwezo wangu mi mwenyewe imekua ngumu alafu nimeona kama kukopi imekua njia rahisi sana kufanya vizuri, mi naona kukopi ndio ilikua inanitoa sana kwa sababu nikifanya kitu changu nafasi sipati”

No comments:

Post a Comment