Tuesday, July 17, 2012

JOYCE BALUHI NDIYE MISS MOROGORO 2012

Miss Morogoro 2012 Joyce Baluhi (katikati) akiwa na washindi wenzake, Salvina Kibona mshindi namba mbili (kushoto) na Irene Thomas mshindi namba tatu mara baada ya kumalizika kwa shindano la Miss Morogoro lililofanyika katika ukumbi wa  Morogoro Hoteli mwishoni mwa wiki.
 
 
Miss Moro Morogoro 2012 Joyce Baluhi kushoto akiwa na Miss Morogoro 20111, Asha Salehe kulia mara baada ya kumkabidhi taji hilo.
 
 
Mgeni rasmi shindano la Miss Morogoro 2012 ambaye ni Afisa Mwendeshaji wa mfuko wa pensheni kanda ya mashariki na kati (PPF) Astronaut Liganga kulia liyesimama akiwa katika picha ya pamoja na Miss Morogoro 2012, Joyce Baluhi aliyekaa, Mratibu wa shindano hilo Frank Kikambako kushoto aliyesimama na warembo wengine walioingia tano bora mara baada ya kutangazwa matokeo na kuwapata washindi.
 
 
Hawa ndiyo warembo waliofanikiwa kuingia hatua ya tano bara kutoka na kuchujwa kupata mshindi wa kwanza, pili na tatu ambao warembo hao watashiriki shindano la Miss Kanda ya Mashariki.
 
  Picha ya pamoja ya washiriki wote 13 ambao walishiriki shindano hilo baada ya kupanda kujukwaani na vazi la ubunifu, ufukweni na jioni katika kinyang'anyiro hicho.
 
  mrembu naye akiwa katika vazi la ubunifu.
 
 
Mrembo Prisca Mengi (18) akipita mbele ya majaji na mashaki na vazi la ubunifu.
 
Rais wa bende ya FM Academia (wazee wa Ngwasuma), Nyoshi El- Saadat akiimba wakati bende yake ikitumbuiza mashabiki waliohudhuria shindano hilo ndani ya viwanja vya wazi vya hoteli ya Morogoro.
 
Mmoja wa wanenguaji wa bendi ya FM Adademia akicheza kwa aina mpya kwa staili ya Vundesa.

JOYCE Baluhi (22) ameibuka katika shindano la kumsaka Miss Morogoro 2012 baada ya kutwaa taji hilo lililokuwa na ushindani wa hali ya juu lililofanyika kwenye viwanja vya wazi vya hoteli ya Morogoro mwishoni wa wiki mkoani hapa.
 
Shindano hilo ambalo lilishirikisha warembe 13 ambapo Salvina Kibona (20) kwa kutwaa nafasi ya pili wakati nafasi ya tatu ikichukuliwa na Irene Thomas (20) ambao walifanikiwa kuvuka katika hatua ya tano bora.

Dalili za Baluhi kutwaa kwa taji hilo zilionekana mapema hasa katika onyesho la vazi la ubunifu, ufukweni na jioni kabla ya kumalizia kizingiti cha mawaswali na kuibua shngwe na ndelemo kutoka kwa mashabiki waliohudhuria shindano hilo kwa kila hatua ambayo akionekana mlimbwende huyu baada ya kulitawala jukwaa.
 
Katika shindano hilo ambalo lilisindikizwa na bendi ya muziki wa dansi ya bende ya FM Academia (wazee wa Ngwasuma) chini ya Rais wao, Nyoshi El- Saadat lilikonga nyoyo za wapenzi wa dansi na shindano hilo ambapo walitumbuiza nyimbo mbalimbali zilizopo katika chati hivi sasa.
 
Mwandaaji wa shindano hilo la Miss Moro 2012, Frank Kikambako alisema kuwa mshindi wa kwanza amejipatia sh400,000 huku mshindi wa pili akipata sh300,000 na mshindi wa tatu akipata zawadi ya sh250,000 na washiriki wote walioshiriki shindano hilo wakiambulia pesa ya sh50,000 kila mmoja kama kifuta jasho.
 
Naye mgeni rasmi katika shindano hilo Afisa Mwendeshaji wa mfuko wa pensheni kanda ya mashariki na kati (PPF), Astronaut Liganga alisema kuwa warembo waliofanikiwa kuingia tano bora na hatimaye kumpata Miss Moro 2012 ambao wote watashiriki shindano la Miss Kanda ya Mashariki kuwa na nidhamu mzuri itayochangia na sifa nyingine kuvuka vikwazo katika shindano hilo.
 
Aliwataja warembo ambao walifanikiwa kutinga hatua ya tano bora ni Nafya Waziri (19) na Betina Lawurence (20).
 
Liganga alisema kuwa sifa pekee katika tasnia nyingi za michezo ikiwemo na urembo ni kuwa na nidhamu mzuri na kuwataka washiriki wengi ambao hawakupata nafasi ya kusonga mbele kuendeleza nidhamu walioionyesha katika kambi ya Miss Morogoro.

No comments:

Post a Comment