Friday, August 10, 2012


Ziwa Nyasa.

Serikali ya Malawi imepuuza tishio la Tanzania kuhusu mzozo wa mpaka kwenye ziwa Nyasa na kusisitiza kwamba ziwa lote ni la Malawi hivyo utafiti wa Mafuta utaendelea.
Waziri wa mambo ya ndani na usalama wa Malawi Uladi Musa amekaririwa akiongea na radio moja na kusema watanzania hawana mamlaka ya kuzuia utafiti wa mafuta uliokua ukifanywa kwenye ziwa hilo, na kama shinikizo litaendelea watawasilisha hiyo ishu kwenye mahakama ya kimataifa.

Gazeti la habari leo limeandika kwamba waziri huyo amesema serikali ya Malawi ina ushahidi kabisa kuthibitisha kwamba ziwa nyasa ni lao na kuna mikataba inayoonyesha, hivyo hoja ya Tanzania haina mantiki.

No comments:

Post a Comment