Tuesday, August 7, 2012

G-TiDE WAZINDUA HUDUMA YA EASY TALK

 Kutoka kushoto ni Meneja Masoko wa Kampuni ya G-TiDE Mbwana Mtopa akionesha aina ya simu ambayo inaweza kujisajili katika huduma ya Easy Talk , mwingine ni Nemes Kalugira  akiwa kitengo cha Masoko.
 
Meneja Masoko  wa Kampuni ya G-TiDE Mbwana  Mtopa,katikati ni Chile Kasoga Kitengo cha Habari  na Nemes Kalugiira  kitengo cha Masoko.

KAMPUNI ya simu za Mikononi ya G-TiDE imezindua teknolojia mpya ya mawasiliano inayofahamina kwa jina La Easy talk ambapo  watumiaji wa simu hizo hupata fursa ya kuunganiswa bure .

Watumiaji hupata fursa ya kuwasiliana kwa njia ya sauti na ujumbe mfupi wa maneno kwa ndugu jamaa na marafiki popote walipo hapa nchini na duniani kote.

Meneja wa G-Tide, Mbwana Mtopa alieleza kuwa teknolojia hiyo mpya imefanikiwa kuwapunguzia gharama za mawasiliano watumiaji wote wa simu za G-TiDE ambazo zinapatikana kwa bei rahisi zaidi kuliko zote. Mkutano huo ulifanyika katika ofisi za G-TiDE jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment