Wednesday, August 15, 2012

HELKOPTA ZA UGANDA ZILIZOPOTEA ZAONEKANA MLIMA WA KENYA, WANAJESHI WAWILI WAFARIKI



Chris Kasaija, rubani wa ngazi za juu wa Jeshi la Anga la Uganda aliokolewa tarehe 14 Agosti huko Nanyuki kutoka mabaki ya helikopta yake. Mabaki ya helikopta mbili za jeshi la Uganda yaligunduliwa siku mbili baada ya kuanguka kwenye mkoa wa mbali wa milimani wa Kenya zikielelekea Somalia. [AFP] 
Na Shirika la AFP
 
Waokoaji waligundua mabaki ya helikopta mbili za Uganda zilizokuwa zimepotea karibu na Mlima wa Kenya siku ya Jumanne (tarehe 14 Agosti), huku wanajeshi wawili wa Uganda wakifariki dunia na watano wakipatikana wakiwa hai. 
Rubani wa ngazi za juu wa Jeshi la Anga la Uganda, Chris Kasaija,  aliokolewa maeneo ya Nanyuki kutoka katika mabaki ya helikopta yake. 

Mabaki ya helikopta mbili za jeshi la Uganda yaligunduliwa siku mbili baada ya kuanguka kwenye mkoa wa mbali wa milimani wa Kenya wakati zikielelekea Somalia kupeleka misaada. 

Makala zinazohusiana 
*Kikosi cha Kenya kujiunga na AMISOM wiki ijayo
 *Uganda yatuma kikosi cha anga kusaidia kupambana na al-Shabaab Somalia
*Kenya kwenye tahadhari kubwa wakati vikosi vinasonga mbele kuelekea Kismayo
"Habari njema ni kwamba tumeweza kuwapata manusura watano na hivi punde wamesafirishwa kwa ndege kuelekea kwenye usalama," alisema Simon Gitau, muhudumu wa ngazi za juu katika Idara ya Wanyamapori ya Kenya, ambayo ilihusika na uokozi. "Wana hali nzuri baada ya kusogea mbali kando ya eneo la ajali."

Mkuu wa Jeshi la Kenya, Jenerali Julius Karangi, aliwaambia waandishi wa habari kwamba moja kati ya helikopta hizo mbili "ilipatikana ikiwa imeungua yote, na nyingine ikining'inia kwenye mlima". Bado watu saba hawajulikani walipo.

Helikopta nne ziliondoka Uganda siku ya Jumapili kwa ajili ya kuelekea mji wa bandari wa Somalia, Kismayo, kuvisaidia vikosi vya Umoja wa Afrika nchini Somalia katika operesheni yake ya kijeshi dhidi ya al-Shabaab.

Moja kati ya helikopta nyengine mbili iliwasili Garissa kama ilivyopangiwa kwa ajili ya kuwekewa mafuta, na nyingine ilitua kwa dharura kwenye Mlima Kenya na kupiga simu ya redio kuomba msaada. Wanatimu wake saba wako salama na imeshaokolewa.

No comments:

Post a Comment