Wednesday, June 26, 2013

WANAFUNZI WALIOSOMA SHULE ZA KATA VYUO VIKUU WAMTAKA LOWASSA AWANIE URAIS 2015


Mbunge wa Monduli, ambaye pia ni waziri mkuu mstaafu, Edward Lowasa, akisalimiana na wanafunzi wa chuo kikuu cha UDOM waliotoka shule za sekondari za kata, wakati walipofika nyumbani kwake mkoani Dodoma kutoa shukrani zao kwa hatua waliyofikia kielimu.


Hamida Salum mwanafunzi wa mwaka wa kwanza UDOM, akizungumza kwenye hafla hiyo.

Mh. Lowasa katikati, Dkt. Mahanga (Kulia) na Parseko Korne wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi hao.
 

WASANII WATAMBA TAMASHA LA FILAMU LA GRAND MALT

Na Mwandishi Wetu
WASANII mbalimbali watakaoshiriki katika Tamasha la Tamasha la Wazi la Filamu Tanzania, maarufu kama ‘Grand Malt Tanzania Open Film Festival’ ambalo litafanyika katika Viwanja vya Nyamagana jijini Mwanza, wameanza kutoa tambo zao.
 
Tamasha hilo linatarajiwa kuanza Jumatatu ijayo, ambapo kutakuwa na maonyesho mbalimbali ya filamu pamoja na burudani za muziki kutoka bendi ya Extra Bongo, pamoja na ngoma za asili.
 
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wasanii hao walisema tamasha hilo litawafungua macho wengi ikiwa pamoja na kupata kujua kile ambacho wanakifanya wakati wakirekodi sinema zao.
 
Msanii mahiri wa filamu, Aunty Ezekiel alisema atakuwepo Mwanza kipindi chote cha tamasha hilo na akataka mashabiki wafike kwa wingi kushuhudia filamu kali zaidi ambazo amezicheza katika siku za karibuni, ambazo zitaonyeshwa bure.
 
“Mimi ndiye mkali wao, Watanzania waje kushuhudia kile ambacho tumekifanya,” alisema Aunty Ezekiel, kauli ambayo iliungwa mkono na Jacqueline Wolper aliyedai naye atakuwepo, ila ndiye pia anayejiamini ni ‘mzuri’ zaidi katika mambo ya filamu.
 
Irene Uwoya alitamba atafunika wengi katika tamasha hilo, huku Vicent Kigosi ‘ray’ na Jacob Steven ‘JB’ nao wakijinasibu watafanya vitu adimu zaidi katika tamasha hilo linalosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wengi wa filamu hapa nchini.
 
Mkurugenzi wa Extra Bongo, Ally Choki alitamba watafanya kweli zaidi siku ya uzinduzi kwani watapiga vibao vipya na kutoa shoo mpya kwa mashabiki watakaojitokeza kipindi chote cha tamasha hilo.
 
“Tumejiandaa vya kutosha, tuna shoo mpya na ya aina yake, ambayo si ya kukosa. Waje tu waone Extra Bongo itakachofanya ni nini,” alisema Choki.
 
Mratibu wa Tamasha hilo aliye pia Mkurugenzi wa Sophia Records, Musa Kissoky, alisema kwa sasa kinachosubiriwa ni siku ya tamasha tu na kusema wasanii wengi wa filamu watakuwepo hapo.
 
“Kwa sasa maandalizi yamekamilika kwa asilimia 90, yaani tunaleta kitu tofauti ambacho watu watashangaa, ndio maana mpaka sasa wengi wanapigwa na bumbuwazi kuhusu kile tutakachofanya siku hiyo,” alisema.
 
Naye Meneja wa kinywaji cha Grand Malt walio wadhamini wakuu wa tamasha hilo, Consolata Adam, alisema wameamua kufanya kweli zaidi kwani wanataka kuona Watanzania wanapata kitu chenye uhakika.
 
“Tumejipanga katika hili na wala hatutanii kwani tunataka kuwawezesha wakazi wa Mwanza na maeneo ya jirani kuhudhuria tamasha hili kwa wingi . Tunawakaribisha watu wote wenye mapenzi na filamu zetu za Tanzania kufika na kushuhudia tamasha hili ambalo mwaka huu limeboreshwa zaidi,” alisema Consolata.
 
Tamasha la Filamu la Grand Malt linatarajiwa kuanza Julai 1-7, mwaka huu huku kukiwa na filamu mbalimbali zitakazooneshwa katika kipindi hicho. Filamu zote hizo ni kutoka Tanzania.
 
Tamasha hilo la filamu limedhaminiwa na kinywaji cha Grand Malt kisicho na kilevi ambacho kinazalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa kushirikiana vyema na ISAMILO LODGE ya Mwanza.

RAIS WA TFF LEODGER TENGA WATAKA MAKOCHA WALIOMALIZA KOZI KUIBUA VIPAJI VYA SOKA NCHINI

Mhitimu wa kozi ya ukocha wa mpira wa miguu kwa ngazi ya pili, Seleman Matola akipongezwa na Rais wa Shirikisho la Soka nchini, Leodgar Tenga kwenye sherehe zilizofanyika Uwanja wa Taifa. Kulia ni Mwenyekiti wa DRFA Almas Kassongo na (kushoto) Mkurungenzi wa Ufundi TFF, Sunday Kayuni.
***********************************
RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodger Tenga, amewataka makocha kuhakikisha wanaibua vipaji vya watoto ili kuwa na vipaji vingi baadaye.
Tenga alikuwa mgeni rasmi katika ufungaji wa kozi hiyo ya ngazi ya pili  iliyofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kozi hiyo iliyoendeshwa na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa Dar es Salaam (DRFA), ilianza Juni 3 huku ikishirikisha zaidi ya makocha 58.
Tenga alisema Bara la Afrika ndilo bara lenye upungufu mkubwa wa wachezaji watoto, tofauti na mabara mengine, kitu ambacho kinarudisha nyuma maendeleo ya soka.
“Hili ndilo bara ambalo lipo nyuma katika kuibua vipaji, mfano nchi ya Ujerumani pekee ina watoto zaidi ya milioni  moja ambao wanaandaliwa, lakini hapa sijui kama wanafika hata idadi hiyo, hivyo kuna changamoto kubwa katika hilo,” alisema.
Aliwataka kuhakikisha wanayatumia mafunzo hayo katika kuleta mabadiliko katika soka hapa nchini, ambapo pia aliwapongeza kwa kushiriki katika kozi hiyo.
Naye Mwenyekiti wa DRFA, Almas Kassongo amesema kozi hiyo itakuwa mkombozi wa makocha kusaidia timu zao kufanya vizuri na kuendeleza mchezo huo nchini.
"Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Rais wa TFF kwa kukubali kuwa nasi licha ya majukumu mengi aliyonayo, lakini niseme tu kwamba kozi hii imekuwa ya mafanikio kutokana na kushirikisha wachezaji wengi wa zamani," alisema.
Baadhi ya washiriki waliohitimu kozi hiyo ni pamoja na Moses Mkandawile, Shedrack Nsajigwa, Ibrahim Masoud Maestro, Shaffih Dauda, Rahel Pallangyo, Ally Yusuph Tigana, Emanuel Gabriel, Jemedari Said, Benard Mwalala, Edibily Lunyamila, Seleman Matola na wengineo.

TANZANIA YASHINDA TUZO 3 ZA UTUMISHI WA UMMA BARANI AFRIKA NCHINI GHANA.

 
Tanzania imeshinda tuzo tatu za juu za ubunifu katika Utumishi wa Umma, barani Afrika, kufuatia Tasisi tatu za Tanzania, kushinda nafasi ya kwanza, na kukabidhiwa vikombe vya ushindi na rais wa Ghana, wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku ya Utumishi wa Umma barani Afrika, yaliyofanyika jana mjini Accra nchini Ghana.
Taasisi za Tanzania zilizoshinda ni Ofisi ya  Ukaguzi ya Taifa, (NAO), Wakala wa Vipimo, (WMA),  na Wakala wa Vitambulisho vya Taifa, (NIDA) kufuatia kufanya vizuri katika maonyesho ya  siku 7 ya shughuli mbalimbali za utumishi wa umma yaliyofikia kilele tarehe 23/06/2013.
Akiuzungumzia ushindi huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Mhe. Celina Kombani, amezipongeza taasisi hizo, zilizolitea sifa taifa hili na kuelezea kufarijika kwake na ushiriki wa  mkubwa wa Tasisi za Tanzania katika maonyesho hayo ambapo jumla ya taasisi 42 kutoka Tanzania, zilishiri.
Akisoma hotuba katika kilele cha maandimisho hayo, Mhe. Kombani ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mawaziri wa Utumishi Barani Afrika, amewataka watumishi wa umma kote barani Afrika, kuwatumikia wananchi kwa  bidii,
unyenyekevu, uadilifu wa hali ya juu, na kueleza utumishi wa umma ni kuwatumikia watu.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Gearge Yambesi, amekiri kuwa Tanzania ni moja ya nchi zinazofanya vizuri sana katika utumishi wa umma barani Afrika, hali inayofanya Tanzania kujijengea heshima kubwa barani Afrika na Ulimwenguni kwa ujumla.
Wakizungumzia kuhusu ushiriki wa Tanzania katika maonyesho hayo, Waziri , Mhe. Celina Kombani,  na Katibu Mkuu, Bwana. George Yambesi, wanaeleza zaidi.
Akizungumzia maonyesho hayo, Mkurugenzi wa Kampuni ya Press and Public Relations (PPR), Bw. Pascal Mayualla, amesema mfulululizo wa vipindi vya redio na Televisheni, kuhusu ushiriki wa Tanzania, katika Maonyesho ya Utumishi wa Umma barani Afrika, vitaanza kuonekane kesho, katika vituo mbalimbali vya redio na Televisheni. 
 

WANAWAKE WANA UWEZO WA KUBADILISHA MAISHA YA MTANZANIA

Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa Kwa Wote (EOTF), Mama Anna Mkapa akitoa hotuba yake  wakati wa ufunguzi  wa mafunzo ya siku tatu ya wanawake wajasiriamali yanayoendelea kwenye  ukumbi wa Bwalo la Maafisa la Jeshi la Kujenga Taifa (JKT),Mgulani jijini Dar es salaam.
***************************************
WANAWAKE wakiwezeshwa kiuchumi na kupatiwa elimu ya msingi ya ujasiriamali, kuepuka maradhi hatarishi na kufahamu haki zao katika jamii, umasikini utapungua,  kipato  kitaongezeka na maisha ya Watanzania yatabadilika. 
 Hayo  yalisemwa leo na Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa Kwa Wote (EOTF), Mama Anna Mkapa wakati wa ufunguzi  wa mafunzo ya siku tatu ya  wanawake wajasiriamali yanayoendelea kwenye  ukumbi wa Bwalo la Maafisa la Jeshi la Kujenga Taifa (JKT),Mgulani jijini Dar es salaam.

Mama Anna Mkapa ambaye pia ni Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa   alisema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wa kiuchumi na kijamii  wajasiriamali  hao kutoka mikoa yote Tanzania Bara na Visiwani, ambapo jumla ya wanawake wapatao 264 wanashiriki.

“Mfuko wa Fursa Sawa Kwa Wote umekusudia kwa nguvu zake zote kuendeleza vita ya hii ya kuwawezesha wanawake  nchini  kujikwamua katika wimbi la umasikini, maradhi na ujinga,” alisisitiza Mama Mkapa.
 Aidha ameiomba Serikali, Asasi za kiraia, taasisi za dini, wahisani binfasi ndani na nje ya nchi, kusaidia  wanawke haswa wa vijijini   kujikwamua na umasikini. 

 Mama Mkapa  aliongeza  kuwa mfuko huo, kwa kipindi cha miaka 16  zaidi ya wanawake 6,820 wamepata mafunzo ya stadi za biashara na wengine  4,500 wamepata fursa ya kushiriki maonyesho mbalimbali ya ndani na nje ya nchi kwa kupitia EOTF ili  kutangaza na kuuza bidhaa zao.

 Naye Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko Dk. Abdallah Kigoda  akifungua mafunzo hayo alisema  Serikali imeanzisha utaratibu wa kuweka kumbukumbu za mkopo katika mabenki kwa kupitia ‘Credit Reference Bureau’ ili kuweza kusaidia kuwafahamu wateja, na kuwaasa wajasiriamali wanapokopa wakumbuke kulipa kwani uaminifu ni kitu muhimu katika biashara.
“Suala lingine la kulipa kipaumbele ni lile la kuongeza thamani ya mazao wanayoyazalisha na tuache kuwazalishia watu wengine bidhaa wakaenda  kuongezea thamani kidogo tu kama vile kwa kufunga na kuweka nembo ya kibiashara na kuuza kwa bei kubwa,” alisema Dk. Kigoda. 
Aliahidi kuwa Wizara yake iko makini kufanya linalowezekana kushirikiana na wajasiliamali hao kutatua  tatizo hilo la kuuza malighafi badala ya bidhaa iliyoongezwa thamani  ili kuongeza ajira na kupunguza umasikini.

MO AWA MTANZANIA WA KWANZA KUTAMBULIKA NA JARIDA LA KIMATAIFA LA FORBES AFRIKA

942331_578714148840668_773339795_n
-Mo mjasirimali kijana mwenye mafanikio ya kipekee katika bara la Afrika.

Mjasirimali mchapakazi na Mbunge Kijana nchini Tanzania, Mohammed Dewji (MO) ametajwa katika jarida la Kimataifa la mabilionea duniani katika Nyanja za biashara (Forbes Africa Magazine) kama mjasirimali mwenye umri mdogo mwenye mafanikio ya kuigwa hapa Afrika na duniani kwa ujumla taarifa la Jarida hilo limeeleza.
 
Kwa mujibu wa taarifa hizo toka kwa Jarida hilo la Forbes African Magazine linasema amekuwa Mtanzania wa Kwanza kupata kuhojiwa na (Forbes Magazine) mafaniko, changamoto na matatizo kadhaa kwenye uwanja wa biashara kwenye ukanda huu wa Afrika Mashariki na kati.
 
Mo akihojiwa na Jarida hilo alisema toka kwenye masaa mia moja kwa wiki na kutengeneza faida ya Millioni 85 dola za kimarekani! Ni mafanikio makubwa katika biashara Afrika.
 
Anasema ni safari ya takribani miaka 12 ya ushindani wa kibiashara ndani ya mipaka ya Tanzania na Afrika kwa ujumla.
 
“Nani anaweza kufikiri kwamba tunaweza kubadilisha biashara yetu toka Millioni 30 za kimarekani hadi dola Billioni 1.1 ndani ya miaka 12 tu,’ alinukuliwa akisema.

WAREMBO KUENDELEA NA MBIO ZA KUMVUA TAJI REDD'S MISS TANZANIA BRIGITTE ALFRED

KINYANG’ANYIRO cha kumpata Redd’s Miss Tanzania kwa mwaka huu kinazidi kushika kasi na sasa, kazi kubwa ipo katika ngazi ya kanda, pale kutakapokuwa na kazi ya kumsaka mrembo wao ndani ya wiki hii.

Kazi kubwa itakuwa katika kumpata Redd’s Miss Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Redd’s Miss Kanda ya Mashariki na Redd’s Miss Kanda ya Ziwa.
Shughuli itaanza kesho, wakati warembo zaidi ya kumi watakapopanda jukwaani katika Ukumbi wa Mikutano wa Mtende, uliopo Soweto Mbeya, kumsaka Redd’s Miss Nyanda za Juu Kusini.
Katika shindano hilo linalotarajiwa kuanza saa 2 usiku, burudani kali inatarajiwa kutolewa na bendi ya FM Academia, huku kiingilio kikiwa ni Sh 10,000 kwa viti vya kawaida na Sh 25,000 kwa viti maalumu.
Keshokutwa itakuwa kazi pevu kwa warembo wa Redd’s Miss Kanda ya Mashariki, ambao watapanda jukwaani katika hoteli ya Nashera mjini Morogoro, kumsaka yule atakayefanikiwa kutwaa taji.
Wanne Star pamoja na wasanii wengine wa Morogoro ndio watakaonogesha shindano hilo, ambalo kiingilio chake kitakuwa Sh 10,000 kwa viti vya kawaida na Sh 20,000 viti maalumu.
Siku hiyo pia atasakwa Redd’s Miss Kanda ya Ziwa, shindano ambalo litafanyika katika ukumbi wa Nyerere ndani ya hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza.
Pia kutakuwa na burudani za kumwaga zitakazoongozwa na mkali wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz akishirikiana na Michael Ross na kiingilio kitakuwa Sh 20,000 viti vya kawaida na Sh 40,000 viti maalumu.
Shindano la Redd’s Miss Tanzania kwa sasa linadhaminiwa na kinywaji cha Redd’s Original kinachozalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).

MFALME MSWATI ATUA NCHINI LEO KUHUDHURIA MKUTANO WA 'SMAT PATNERSHIP' JUNI 28

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Mfalme Mswati wa (ii) wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam ,Mfalme Mswati wa ii, ametua nchini kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa 'Smat Patnership' unaotarajia kuanza Juni 28 mwaka huu.
 Mfalme Mswati, akishuka kwenye ndege yake wakati alipowasili nchini.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Mfalme Mswati ii, baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Mfalme Mswati wa ii, ametua nchini kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa 'Smat Patnership' unaotarajia kuanza Juni 28 mwaka huu.
Wasaidizi wake wakiimba nyimbo za kikabila kabla ya Mfalme wao kushuka ndegeni, haikuweza kufahamika kuwa ilikuwa ni mila za kwao ama walikuwa wakitambika ama nini kilikuwa kikiendelea.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Mfalme Mswati ii, baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Mfalme Mswati wa ii, ametua nchini kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa 'Smat Patnership' unaotarajia kuanza Juni 28 mwaka huu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika mazungumzo na Mfalme Mswati ii, mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa 'Smat Patnership', unaotarajia kuanza Juni 28. Kushoto ni mke wa Mfalme Mswati.

UNIC NA TAYODEA WAENDESHA SEMINA YA KUPINGA MATUMIZI NA BIASHARA YA MADAWA YA KULEVYA JIJINI TANGA

_DSC1214
Afisa uhusiano wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Usia Nkhoma Ledama akiwasilisha ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu siku ya kimataifa ya kupinga matumizi na biashara haramu ya madawa ya kulevya kwenye kongamano la vijana kuhusu madawa ya kulevya mjini Tanga.
_DSC1161
Afisa habari wa kituo cha taarifa cha Umoja wa mataifa (UNIC) Usia Nkhoma Ledama akikabidhi Beji ya utambulisho kwa mmoja wa vijana aliyekaa miezi sita kwenye nyumba ya mafunzo ya waathirika wa madawa ya kulevya bila kutumia madawa hayo mjini Tanga katika kituo cha Tanga Sober House.
_DSC1215
Pichani juu na chini ni baadhi ya vijana wakifuatilia semina ya kupinga matumizi na biashara haramu ya madawa ya kulevya iliyoandaliwa na Kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) kwa kushirikiana na TAYODEA.
_DSC1215
_DSC1179
Ujumbe kutoka Ofisi za Umoja wa Mataifa Dar es Salaam, waandishi wa habari na watumiaji wa dawa za kulevya walioonyesha nia ya kuacha kutumia dawa hizo mjini Tanga, ambao wapo kwenye nyumba ya mafunzo ya kuwawezesha kuachana na dawa hizo (TANGA SOBER HOUSE) iliyopo Tanga. Ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kupinga matumizi na biashara ya dawa za kulevya ambayo hufanyika 26 June kila mwaka. Kitaifa maadhimisho hayo yanafanyika mjini Dodoma.

MUME AMKAMATA MKEWE KWA SANGOMA AKITAKA KUTEKETEZA FAMILIA KISHIRIKINA KIBAHA

 Mtuhumiwa huyo akiwa ndani ya gari la polisi baada ya kukamatwa akiwa na Mganga wake, hapa wakipelekwa Kituo cha Polisi. 
Mtuhumiwa akiwa ndani ya  chumba cha mganga na mganga wake aitwaye Yahaya.
Mtuhumiwa  wa kutaka kuuwa kwa imani za kishirikina aliyetambuliwa kwa jina la Margareth Simon Nkwera, akiwa ndani ya chumba cha Mganga wa Jadi alikokamatiwa alipokwenda kutekeleza suala lake la kutaka kujaribu kuua. 

Hapa akiwa katika mahojiano na mzee wa ukoo wa Shirima, Afisa wa Jeshi la Polisi daraja la Kwanza,  Joseph Shirima mara baada ya kumkamata live kwa Sangoma huyo baada ya kuwekewa mitego.Habari hii imetolewa na mwenyekiti wa ukoo wa shirima Bw. Godilisten Hendrick Shirima.


Mama huyo aliyejulikana kwa jina la Magreth simon Nkwera ambae ni mtoto wa kwanza wa Mnadhimu mkuu wa kwanza wa JWTZ, Brig Gen Simon Nkwera amekamatwa jana huko maeneo ya Maili Mbili Kibaha Mkoa wa Pwani akiwa kwa Mganga wa kienyeji akijaribu kutekeleza jaribio lake la kuwauwa baadhi ya watoto wa mumewe na baadhi ya ndugu zake kwa imani za kishirikina.
HABARI HII IMETOLEWA NA:-Makamu mwenyekiti wa ukoo wa Shirima Bw. Godilisten 
Hendrick Shirima +225 753 170 271
KWA USHIRIKIANO NA:- Mzee wa ukoo wa Shirima Bw. Joseph Shirima, 0719948241
NA:- Mume wa mtuhumiwa Mzee Douglas Shirima, 0658386628

BALOZI IDDI AZINDUA JENGO LA SKULI YA MIWANI JIMBO LA UZINI UNGUJA

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akisalimiana ana Wanafunzi wa Skuli ya Msingi wa Miwani, baada ya kuzinduliwa rasmi kwa jengo lao jipya. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, akilizindua rasmi jengo jipya la madarasa mawili ya Skuli ya Msingi ya Miwani iliyomo ndani ya Jimbo la Uzini.
 Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mh. Mohd Raza akimpatia maelezo ya ujenzi wa Jengo la Skuli ya Msingi ya Miwani Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif mara baada ya kulizindua rasmi.
Balozi Seif akimpongeza Msaidizi Mkurugenzi wa Benki ya Watu wa Zanzibar  { PBZ } Ame Haji Makame kwa hatua ya benki hiyo kusaidia vikalio kwenye jengo jipya la skuli ya msingi ya miwani. Kulia yao ni Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mh. Mohd Raza Hassan na Pembeni yao Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kusini Dr. Islamu Idriss.
*********************************
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema  wakati umefika kwa Wananchi kuwa na hadhari katika kuangalia Mtu mwenye muelekeo wa kuwafaa katika kuwasimamia kusukuma mbele maendeleo yao wanayoyahitaji kwenye maeneo yao.
Kauli hiyo aliitoa wakati akizindua rasmi jengo jipya na la kisasa la Skuli ya Msingi  ya Miwani ndani ya Jimbo la Uzini lililojengwa ndani ya kipindi cha miezi miwili na Mwakilishi wa Jimbo hilo Mh. Mohd Raza Hassan.
Balozi Seif alisema ile tabia ya baadhi ya wananchi kukumbatia watu wanaoendeleza ubinafsi inafaa kupigwa vita kwa hali yoyote ile kwa vile inachangia kuzorotesha kasi ya Maendeleo ya Wananachi.
Aliwahimiza Viongozi, washirika na wahisani zikiwemo Taasisi za Kijamii na zile za maendeleo zilizomo katika Halmashauri za Wilaya kujikita zaidi katika kuunga mkono juhudi za Wananachi kwenye sekta za Mendeleo na Kiuchumi wakiangalia zaidi ile sekta muhimu ya Elimu.
“ Siku zote tunasema tuwekeze kwenye elimu ambayo watoto wetu itawasaidia wao wenyewe kwa kupata muelekeo na mafanikio ya maisha yao sambamba na kusaidia familia zinazowazunguuka “. Alisisitiza Balozi Seif.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alimpongeza Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mh. Mohd Raza kwa hatua yake aliyochukuwa ya ujenzi wa Jengo hilo la madarasa mawili lililokamilika huduma zote ikiwemo vikalio ambalo limesaidia kuiepusha Skuli ya Miwani kuchukuwa wanafunzi katika mikondo miwili.
Balozi Seif alisema juhudi za Mwakilishi huyo ni miongoni mwa utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2010 ya CCM pamoja na kukamilisha ahadi alizotowa wakati wa kuomba ridhaa ya kuliongoza Jimbo hilo.
Aliwakumbusha Viongozi wengine wa Jimbo, Wilaya na hata mkoa kuunga mkono jitihada za Wananachi wa Miwani katika kukamilisha jengo jengine la Madarasa  Sita la Skuli hiyo ambalo linahitaji nguvu za ziada za Viongozi hao likiwa limekwama kwa  miaka minne sasa.
Alisema katika kuunga mkono juhudi hizo za Wananchi ambapo zinahitajika kiasi cha shilingi Milioni Tisa { 9,000,000/- } kukamilisha hatua ya linta ili likabidhiwe  Wizara ya Elimu  na Mafunzo ya Amali kwa Ukamilishaji aliahidi kuchangia Shilingi Milioni Mbili { 2,000,000/- }.
“ Sisi viongozi kuanzia Wawakilishi wa kuteuliwa, Mbunge, Madiwani na hata halmashauri za Wilaya tunalazimika kuunga mkono juhudi hizi ili kutowavunja moyo wananchi tunaowaongoza katika Majimbo yetu “. Alikumbusha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.
Akitoa salamu za Benki ya Watu wa Zanzibar { PBZ } iliyosaidia Vikalio vyote vya jengo hilo Meza 100 na Viti 100 vyenye thamani ya shilingi Milioni 16,000,000/-  Msaidizi Mkurugenzi Mtendaji wa Benki  hiyo  Ame Haji Makame amesema benki hiyo itaendelea kuunga mkono juhudi za Wananchi popote pale.
Nd. Ame alisema benki ya Watu wa Zanzibar inajali maendeleo ya Jamii na wakati mwengine kushawishika kusaidia miradi yao tofauti ikiwemo zaidi sekta ya elimu ambayo ndio mkombozi wa Taifa lolote.
Naye kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Bibi Mwanaidi Saleh amempongeza Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mh. Raza kwa juhudi zake za kusaidia nguvu za Wizara hiyo katika ukamilishaji wa majengo  ya Skuli.
Bibi Mwanaidi alisema juhudi za Mwakilishi huyo za kukamilisha majengo mawili ya Skuli ndani ya Jimbo hilo limeipunguzia mzigo mkubwa Wizara ya Elimu wa kukamilisha majengo kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa na wizara hiyo.
Katibu Mkuu huyo wa Wizara ya Elimu amewakumbusha Wananchi katika maeneo mbali mbali Nchini kuhakikisha kwamba majengo ya skuli wanayoyaanzisha yanatengewa vyumba maalum kwa ajili ya vitengo vya Kompyuta.
Alisema Wizara imeanzisha mfumo maalum wa mafunzo ya kompyuta kuanzia elimu ya msingi kwa lengo la kuwawezesha wanafunzi wa Zanzibar kwenda sambamba na mabadiliko ya sayansi na Teknolojia yaliyopo Duniani.
Akitoa shukrani zake katika hafla hiyo ya uzinduzi wa jengo jipya la Skuli ya Miwani iliyomo ndani ya Jimbo la Uzini Mwakilishi wa Jimbo hilo Mh. Mohd Raza Hassan alisema kwamba uwepo wa Viongozi katika Jamii upo kwa ajili ya kusimamia matakwa ya Wananchi.
Mh. Raza alisema tabia ya baadhi ya Viongozi kuigonganisha vichwa jamii ni kutowafanyia haki Wananachi wanaowaongoza na hatimae inaviza maendeleo yao na kuwaongezea chuki na fitna baina yao.
Mapema katika Risala yao iliyosomwa na Mwalimu  wa Skuli ya Msingi ya Miwani Juma Abdulla wananchi hao wa Kijiji cha Miwani walisema bado wanakabiliwa na changamoto kadhaa ndani ya Kijiji hicho.
Mwalimu Juma alizitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na ukosefu wa bara bara, mashine za uchapaji , ukosefu wa Daktari katika kituo chao cha Afya pamoja na umaliziaji wa jengo lao la madarasa sita ambalo linaweza kusaidia muendelezo wa mkondo mmoja tu skulini hapo.
Jengo jipya  la  madarasa mawili la Skuli ya Msingi ya Miwani litakalokuwa na uwezo wa kuchukuwa wanafunzi 122 ambapo wanafunzi  56 kwa kila chumba  lilijengwa ndani ya kipindi cha miezi miwili kwa gharama za shilingi Milioni 30,000,000/- .
Katika hafla hiyo Mwakilishi wa Jimbo la Uzini pia alikabidhi Mchango wa Shilingi Milioni Mbili kwa ajili ya Kusaidia maandalizi ya Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 50 ya Mapinduzi Mtukufu ya Zanzibar hapo mwaka 2014.
Fedha hizo zitasaidia katika Ofisi ya Mkoa Kusini Unguja, Wilaya ya Kati, Jimbo la Uzini Kichama pamoja na kukabidhi pia mipira kwa ajili ya Timu za Skuli 12 zilizomo ndani ya Jimbo la Uzini.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
26/6/2013.

JUMA KASEJA ATUPIWA VILAGO RASMI SIMBA, ATOWEKA MAZOEZINI, ALAANI KUFANYIWA FUJO MORO

KLABU ya Simba ya Jijini Dar es Salaam, leo imetangaza rasmi kumtema Nahodha wake ambaye pia ni Nahodha wa timu ya Taifa na Simba, Juma Kaseja,  ambaye alikuwa akiwaumiza vichwa viongozi wa Klabu hiyo.

Awali Kaseja, alikuwa akikaririwa na Vyombo vya habari kuwa hajajua 
hatima yake na Klabu ya Simba na kuhusishwa ukimya wake na kuhamia Timu ya Azam, ambao awali walionyesha nia ya kumhitaji.

Lakini alipohojiwa Kaseja, alisema kuwa bado alikuwa akihitaji 
kupumzika ili kujua kuwa atasaini tena sima ama la, na kwa upande wa 
Azam, walipohojiwa kuhusiana na hilo, nao waliruka Kimanga kuonyesha 
nia ya kumhitaji Kipa huyo namba moja wa Simba.
Hili la kutunguliwa mabao kama haya si sababu za kutemwa, kipa 
huyu nambamoja, lazima kuna sababu iliyojificha nyuma ya pazia, 
'Kisiasa zaidi', na wala haiingii akilini kuwambiwa Kaseja ameshuka 
kiwangi kama wanavyoeleza mashabiki na viongozi wa Simba.

Akizungumza na mtandao huu Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel 
Kamwaga alisema kuwa mpaka wanawasili kwenye Uwanja wa Kinesi 
jioni ya leo kwa ajili ya mazoezi ya timu hiyo, Kipa huyo hakuwepo 
mazoezini ambapo Ezekile, alisema kuwa inawezekana ameathirika kisaikolojia baada ya kufanyiwa vurugu na mashabiki wa Simbo mkoani Morogoro wiki iliyopita.
Nao Uongozi wa Klabu hiyo, leo umeweka wazi kuwa hawatakuwa na
 Kipa huyo katika msimu ujao, na kutangaza rasmi kuwa wamevunja 
ndoa yao rasmi leo, bila kueleza sababu za kumuacha kipa huyo, huku ikielezwa kuwa huenda ikawa ni dau alilohitaji kipa huyo, jambo ambalo limekanushwa na Uongozi huo.

Hatimaye uongozi wa klabu ya Simba kupitia kwa mwenyekiti wa 
kamati ya usajili Zacharia Hans Pope umetangaza rasmi kuachana 
na mlinda mlango mkongwe wa timu hiyo  Juma Kaseja.
Hans Pope ameyasema hayo katika  kipindi cha michezo  cha Radio 
One jijini Dar es Salaam.
Kaseja akifungwa bao katika moja ya mchezo wake.
Amesema hawatomuongezea mkataba Kaseja na wamempa baraka za 
kutafuta timu nyingine.

 Kwa muda mrefu Simba ilikuwa ikisuasua kumpa mkataba Kaseja 
aliyeidakia Simba kwa takribani miaka 10, na hatimaye leo 
wamethibitisha rasmi kumuacha Kaseja.

“Juma ndio basi tena kaka, Kasema yeye na Simba basi, 
amesononeshwa mno na jinsi alivyodhalilishwa baada ya mechi ya Morogoro,”alisikika akisema mchezaji mmoja wa Simba baada ya 
mazoezi Kinesi leo.

Kaseja alitukanwa na kutishiwa maisha na mashabiki wa Simba 
baada ya mechi dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Jamhuri, 
Morogoro wakimtuhumu kufungwa mabao ya kizembe.
Milovan, akiwa hoi katika moja ya mchezo akiwa Mocha wa simba.
Ikumbukwe ni hivi karibuni tu Klabu hiyo, ilimtupia vilango aliyekuwa 
Kocha Mkuu wake, Milovan Circkovic, kwa madai ya kutotimiza malengo
 ya Klabu hiyo kwa kufanya vizuri katika michezo ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara iliyomalizika hivi karibuni, na sasa leo ni zamu ya Juma Kaseja, huku ikiwa tayari imeshafanya hivyo kwa kuwatoa kwa mkopo wachezaji wake, Vipenzi vya mashabiki wa timu hiyo, Haruna Moshi 'Boban' aliyepelekwa katika timu ya Coastal Union ya Tanga, na Juma Nyoso, huku ikitabiriwa anayeguata akawa ni Amir Maftah, ambaye ametetewa na Ofisa habari wa timu hiyo kuwa hayupoa mazoezini kwa sabau ana ruhusa maalum kutokana na kufunga ndoa hivi majuzi.
Juma Kaseja katika moja ya kazi nzuri aliyoifanya akiwa na Simba msimu wa 2012.