WASHIRIKI WA MISS TANGA WATEMBELEA MAPANGO YA AMBONI
OXFAM KWA KUPITIA KAMPENI YA GROW YATOA WITO KWA SERIKALI NA SEKTA BINAFSI KUWEKEZA KWA WAKULIMA WADOGO NA WA KATI
Mwanasheria –Mshauri Mwelekezi katika
Masuala ya Haki za Ardhi - Emmanuel Massawe akifafanua jambo kwa wageni
waalikwa wakati wa hafla ya kuwatangaza rasmi mabalozi wa OXFAM katika
Kampeni ya GROW nchini itakayowezesha mfumo wa chakula kuwa wa haki na
salama.
Taasisi isiyo ya kiserikali ya OXFAM
kwa kupitia Kampeni yake ya GROW imewakutanisha pamoja masupa staa saba
wa Tanzania wakiwemo Mbunge wa Kawe Mh. Halima Mdee pamoja na Mbunge wa
Bunge la Afrika Mashariki Mh. Shy-Rose Bhanji kufanyakazi pamoja na
vikundi vya wanawake wajasiriamali na wazalishaji, kwa lengo la
kuhakikisha hakuna mtanzania atakayeteseka kwa njaa wakati mbinu za
kilimo zinaweza kufanikiwa.
Akizungumza wakati wa kuwatambulisha
rasmi mabalozi wa OXFAM kupitia kampeni hiyo, mmoja wa mabalozi hao Bi.
Khadija Mwanamboka amesema kilimo sio tu ni sekta endelevu nchini
Tanzania bali pia ni Nyanja inayowezesha kupatikana kwa chakula kwa
familia na akiba ya chakula kwa taifa kwa kuwa asilimia 80 ya
wajasiriamali nchini ni wakulima.
Nchini Tanzania takwimu zinaonyesha
kuwa zaidi ya asilimia 60 ya wajasiriamali wanawake wanajihusisha na
kilimo kikiwepo cha mbogamboga na matunda.
Aidha kampeni hiyo inakusudia
kuendeleza na kukuza uzalishaji utakaoyafanya mazao hayo ya kilimo kuwa
na bei muafaka kwa faida ya wakulima hao wa chini na wa kati.
Naibu Mkurugenzi Mkazi OXFAM-Justin
Morgan akziungumza na wageni waalikwa namna kampeni hiyo itakavyofanya
kazi zake za uhamasishaji hapa nchini.
Mabalozi wa OXFAM katika kampeni ya GROW wakati wa hafla hiyo.
Khadija Mwanamboka – Mbunifu wa Mavazi akipozi na Tuzo yake mara baada ya kutangazwa rasmi.
Shamim Mwasha Fashion Blogger.
Dina Marious- Mtangazaji wa Redio.
Jacob Stephen Muigizaji.
Masoud Kipanya Mchora Katuni.
Mabalozi wa OXFAM katika kampeni ya GROW katika picha ya pamoja na Naibu Mkurugenzi Mkazi OXFAM-Justin Morgan (wa pili kushoto).
Sehemu ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki.
JUMA FUNDI VS NASIBU RAMADHANI KUPAMBANA SIKU YA IDI PILI
PROMOTA WA MPAMBANO WA MASUMBWI SIDE MKIGOMA KATIKATI AKIWAINUA MIKONO JUU MABONDIA JUMA FUNDI KUSHOTO NA NASSIBU RAMADHANI |
Mabondia wakisaini mkataba |
No comments:
Post a Comment