Didier Drogba kurudi kwenye timu ya taifa .
Mshambuliaji
wa Galatasaray ya Uturuki Didier Drogba amehakikishiwa nafasi yake
kwenye kikosi cha timu ya taifa baada ya kuachwa kwenye mechi mbili za
kufuzu kwa kombe la dunia mwaka 2014.
Kocha wa timu ya taifa ya Ivory Coasta Mfaransa Sabri Lamouchi
amesema kuwa atakuwa “mwendawazimu” kama akimuacha mchezaji mwenye uwezo
na mchango mkubwa kwa timu ya taifa kama Drogba na kuachwa kwake kwenye
vikosi vya hivi karibuni hakuamini kuwa amewekwa pembeni moja kwa moja.
Lamouchi aliongeza kuwa Drogba alihitaji kupumzishwa baada ya
kuitumikia timu ya taifa kwa muda mrefu lakini haimaanishi kuwa
hatacheza tena kwenye timu hiyo.
Drogba hajaichezea timu yake ya taifa tangu ilipotolewa na Nigeria
kwenye michuano ya kombe la mataifa ya Afrika na mawazo ya wengi ni
kwamba Drogba hatarudi tena kwenye timu hiyo baada ya kuonekana umri
umemtupa mkono na kiwango chake kushuka.
Ivory Coast imekuwa ikiwatumia washambuliaji kama Lacina Traore na
Wilfred Bony ambao walifungakwenye mechi ya jumapili dhidi ya Taifa
Stars huku Dorgba akiwa ameachwa. Bony alimaliza msimu uliopita kama
mshambuliaji bora wa Kiafrika Barani Ulaya akiwa amefunga mabao 30
kwenye ligi ya Uholanzi.
Didier Drogba huenda akaitwa kwenye kikosi cha Ivory Coast
kitakachoitwa mwezi wa nane kwa ajili ya mechi za kirafiki za kimataifa
ikiwemo mechi dhidi ya Mexico.
No comments:
Post a Comment