MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AONGOZA KIKAO CHA SMZ NA SMT MJINI DODOMA LEO
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiongoza Kikao cha SMZ na SMT, kiliochofanyika Dodoma Hoteli, leo.
Kulia ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda, na (kushoto) ni Makamu wa pili wa
Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
leo ameongoza Kikao cha SMT na SMZ, kilichofanyika kwenye ukumbi wa
Dodoma Hoteli, mjini Dodoma, leo. Kikao hicho kimehudhuriwa pia na mhe.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi,
Seif Idd, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amani, Ali Juma Shamhuna na
Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) Samih Suluhu pamoja na
Wajumbe washiriki wa kikao hicho ambao ni Mawaziri kutoka serikali zote
mbili za Tanzania Bara na Zanzibar.
Baadhi ya Wajumbe wa Kikao hicho ambao ni Mawaziri kutoka Serikali ya Zanzibar.
Baadhi ya Wajumbe wa Kikao hicho ambao ni Mawaziri kutoka Serikali ya Tanzania Bara.
Baadhi ya Wajumbe wa Kikao hicho ambao ni Mawaziri kutoka Serikali ya Zanzibar.
Baadhi ya Wajumbe wa Kikao hicho ambao ni Mawaziri kutoka Serikali ya Tanzania Bara.
Wajumbe wa Kikao hicho.
Baadhi ya Wajumbe wa Kikao hicho ambao ni Mawaziri kutoka Serikali ya Zanzibar.
*JICHO LANGU NDANI YA MJI WA DODOMA
Mitaa
ya Stendi ya Mabasi yaendayo Mikoa mingine katika Mji wa Dodoma, Eneo
hilo kwa sasa kuna Stendi isiyo rasmi kutokana na ujenzi wa Kituo hicho
ambapo mabasi hulazimika kuegesha pembezoni mwa barabara kubwa huku
yakipakia kwa foleni moja baada ya jingine.
Huku
nako ni stendi ndogo iliyopo Mtaa wa Majengo ambayo huegeshwa magari
yanayokwenda katika vijiji vya Mji wa Dodoma na Wilaya zake.
*MWIGULU NCHEMBA NA PETER MSIGWA NUSURA WAZICHAPE 'KAVU KAVU' DODOMA
Mbunge
wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba (kushoto) akizozana na wabunge wa
Chadema, Mchungaji Peter Msigwa(kulia)mbunge wa Nyamagana, Ezekiah Wenje
(wa pili kulia) na Mbunge wa Musoma Mjini, Vicent Nyerere (wa pili
kushoto) baada ya kukutana nje ya ukumbi wa mikutano wa St Gasper,Dodoma
jana wakati wa semina ya wabunge ya kuhusu Ukimwi.
*******************************************
*Tukio
hilo lilitokea katika viwanja vya Hoteli ya St Gasper nje kidogo ya mji
wa Dodoma, walipokwenda kwa ajili ya kuhudhuria semina ya wabunge
wapambanaji na Ukimwi, ambapo baadhi ya wabunge wa Chadema walihudhuria,
baada ya kutoonekana mjini humo tangu Juni 17 mwaka huu.
Mbunge
wa Jimbo la Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa na mbunge wa
Iramba Magharibi (CCM), Mwigulu Nchemba jana nusura wachapane makonde
baada ya kutupiana maneno ya kashfa, wakituhumiana kuhusika na mlipuko
wa bomu uliotokea Jumamosi iliyopita mkoani Arusha.
Tukio
hilo lilitokea katika viwanja vya Hoteli ya St Gasper nje kidogo ya mji
wa Dodoma, walipokwenda kwa ajili ya kuhudhuria semina ya wabunge
wapambanaji na Ukimwi, ambapo baadhi ya wabunge wa Chadema walihudhuria,
baada ya kutoonekana mjini humo tangu Juni 17 mwaka huu.
Wabunge
hao wa Chadema hawakuhudhuria kikao chochote cha Bunge kutokana na
kwenda mkoani Arusha kwa shughuli mbalimbali, kutokana na mlipuko wa
bomu uliotokea katika mkutano wao wa kuhitimisha kampeni zake za
uchaguzi mdogo wa udiwani katika viwanja vya Soweto, Juni 16 jijini
humo.
Malumbano
hayo yanatokana na Nchemba kuituhumu Chadema kuhusika na mlipuko huo,
Juni 20 mwaka huu wakati akichangia hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali ya
mwaka 2013/2014, akisema chama hicho kilipanga kulipua bomu hilo ili
kuwafanya Watanzania waamini kuwa Serikali ya CCM ndiyo inayohusika na
tukio hilo.
TUKIO LILIVYOANZA:- Wakati
Msigwa akiingia katika ukumbi huo akiwa ameongozana na Mbunge wa
Nyamagana (Chadema), Ezekiah Wenje, walikutana uso kwa uso na Nchemba
ambaye alikuwa akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Said Amour
Arfi.
Baada ya Nchemba kumwona Msigwa alimkaribisha mchungaji huyo akisema; “Karibu sana bwana, salama lakini?”
Hata
hivyo, badala ya kujibu salamu hiyo ya Nchemba, Msigwa alikuja juu na
kumtuhumu Nchemba kwamba anatoa kauli zinazoweza kuvuruga amani ya nchi.
“Wewe
ni mtu hatari sana, haya yote yanasababishwa na wewe, mnatumia damu za
watu kutafuta madaraka,” alisema Msigwa akimtupia maneno Mwigulu.
Baada ya kauli hiyo Nchemba alihoji akisema: “Ki-vipi? Hayo mambo tuyaache, Msigwa achana na haya mambo!”
Baada
ya Nchemba ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM kujibu, Msigwa
alimsogelea karibu na kumnyooshea kidole, huku akiendelea kumtuhumu kuwa
ana siasa chafu zinazopandikiza chuki kwa jamii.
Malumbano
hayo pia yaliingiliwa na Mbunge wa Musoma Mjini (Chadema), Vicent
Nyerere ambaye alimuunga mkono Msigwa, huku akimtuhumu Nchemba kuwa ni
mtu mbaya katika siasa za Tanzania. Katika kile kilichoonekana kutaka
kuweka mambo sawa, Wenje alimvuta Msigwa na kumpeleka ukumbini ili
kuepusha shari baada ya wabunge hao kuzidi kurushiana maneno. Chanzo:-
www.mwananchi.co.tz
*RAIS WA TFF LEODGER TENGA KUFUNGA KOZI YA MAKOCHA JUMANNE
RAIS
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodger Tenga
anatarajia kuwa mgeni rasmi katika ufungaji wa kozi ya makocha wa ngazi
ya pili (Intermediate) itakayofanyika Jumanne kwenye Uwanja wa Taifa
jijini Dar es Salaam, kuanzia saa tano asubuhi.
Kozi hiyo iliyodumu kwa wiki nne, ilifunguliwa rasmi Juni 3 mwaka huu kwenye Ukumbi wa Harbours Club, uliopo Kurasini.
Mkurugenzi
wa Ufundi Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), Joseph
Kanakamfumu, alisema Rais Tenga ameridhia kufunga kozi hiyo baada
kukosekana katika ufunguzi wa kozi hiyo kutokana na majukumu aliyokuwa
nayo.
“Kozi
yetu ya ngazi ya pili itafungwa Jumanne kwenye Uwanja wa Taifa kuanzia
saa tano asubuhi na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),
Leodger Tenga ndiye atatufungia kozi yetu na ameridhia kuwa atakuwa
nasi,” alisema Kanakamfumu.
Alisema
kozi hiyo itakuwa chachu ya kupatikana kwa makocha watakaosaidia
maendeleo ya mchezo huo katika Mkoa wa Dar es Salaam na Taifa kwa
ujumla.
Kozi
hiyo ni ya kwanza kuendeshwa na DRFA tangu kuingia madarakani kwa
uongozi mpya wa chama hicho Desemba 12, chini ya Mwenyekiti Almas
Kassongo.
*MWENYEKITI UVCCM TAIFA SADIFA JUMA HAMISI APINGA MFUMO WA SERIKALI TATU
Sadifa ameyasema hayo wakati akizungumza na
wanachama wasomi wa UVCCM kutoka katika vyuo vikuu mkoani kilimanjaro katika
hafla ya kuwaaga wasomi hao na ambapo pia ametunuku vyeti vya uanachama kwa wanafunzi
312 pamoja na kuwakabidhi kadi za uanachama wanachama wapya.
Amesema bila amani na muungano wa wananchi maendeleo
hayawezi kupatikana katika nchi ambpo aliwataka vijana kuwa mtari wa mbele
kuwaelimisha wananchi wa kawaida juu ya umuhimu wa kuenzi, kudumisha na kuimarisha
muungano wa zanzibar na Tanganyika kama
njia pekee ya kuhakikisha nchi inakuwa na amani siku zote.
Katibu wa UVCCM manispaa ya Moshi, Bwana Makwaiya akisakata Rumba muda mfupi baada ya maandamano kuwasili katika makao makuu ya CCM mkoa wa kilimanjaro |
“Vijana tuna wajibu kubwa wa kuwaenzi waliotuletea
muungano wetu wa sasa, taaluma zetu ziwe dira ya jamii katika kuenzi, kudumisha
na kuimarisha muungano wetu kwani ndio njia pekee ya kusaidia kudumisha amani
na usalama wan chi yetu, tuepuke kujiingiza katika mkumbo wa wale wanaodai nchi
haitatawalika,” amesema
Hata hivyo Sadifa amewataka vijana kutodanganyika na
vyama vinavyoeneza chuki na maandamano yasiyokuwa na msingi wowote huku
akifafanua kuwa kisheria kuandamana na haki ya msingi lakini ifuate sheria na
yassingilie haki za wengine.
Sadifa akikabidhi cheti cha unachama kwa mwanafunzi wa chuo kikuu muccobs jana, jumla ya wanavyuo 312 walipata vyeti vya uanachama wa UVCCM. |
“Chama pekee katika nchi hii ni CCM, kuna vyama
vingine vimeanzishwa ambavyo mimi binafsi naviita ‘Saccos’, hauwezi
ukajikopesha fedha kienyejienyeji kama alivyofanya Dk. Slaa! Vijana tuwe makini
na saccos hizi ambazo ajenda zao ni kukopeshana na vurugu tu,” amesema Sadifa.
Kwa upande wake mwenyekiti wa shirikisho la wanafunzi
wa vyuo vikuu wanachama wa CCM kilimanjaro, Wakati Mtulya akizungumzia
changamoto wanazokumbana nazo, alisema kumekuwa na urasimu ndani ya bodi ya
mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu, ambapo mikopo imekuwa ikitolewa kwa watu
wasiostahili huku walengwa wakiendelea kutaabika.
Sadifa (aliyevaa suti) akiongoza vijana kucheza kwaito katika ukumbi wa CCM mkoa wa Kilimanjaro |
“Mikopo ni yetu, sio ruzuku, lazima tukopeshwe kwa
wakati kwani lazima tutairudisha lakini jambo la kusikitisha, bodi hii imekuwa ikitoa
mikopo kwa watoto wa masaki, huku sisi watoto wea mkulima tukiendelea
kuzungushwa na kuwekewa masharti magumu ili kupata mikopo hiyo, hili ni tatizo,”
amesema Mtulya.
No comments:
Post a Comment