*MWIGULU NCHEMBA NA PETER MSIGWA NUSURA WAZICHAPE 'KAVU KAVU' DODOMA
Mbunge
wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba (kushoto) akizozana na wabunge wa
Chadema, Mchungaji Peter Msigwa(kulia)mbunge wa Nyamagana, Ezekiah Wenje
(wa pili kulia) na Mbunge wa Musoma Mjini, Vicent Nyerere (wa pili
kushoto) baada ya kukutana nje ya ukumbi wa mikutano wa St Gasper,Dodoma
jana wakati wa semina ya wabunge ya kuhusu Ukimwi.
*******************************************
*Tukio
hilo lilitokea katika viwanja vya Hoteli ya St Gasper nje kidogo ya mji
wa Dodoma, walipokwenda kwa ajili ya kuhudhuria semina ya wabunge
wapambanaji na Ukimwi, ambapo baadhi ya wabunge wa Chadema walihudhuria,
baada ya kutoonekana mjini humo tangu Juni 17 mwaka huu.
Mbunge
wa Jimbo la Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa na mbunge wa
Iramba Magharibi (CCM), Mwigulu Nchemba jana nusura wachapane makonde
baada ya kutupiana maneno ya kashfa, wakituhumiana kuhusika na mlipuko
wa bomu uliotokea Jumamosi iliyopita mkoani Arusha.
Tukio
hilo lilitokea katika viwanja vya Hoteli ya St Gasper nje kidogo ya mji
wa Dodoma, walipokwenda kwa ajili ya kuhudhuria semina ya wabunge
wapambanaji na Ukimwi, ambapo baadhi ya wabunge wa Chadema walihudhuria,
baada ya kutoonekana mjini humo tangu Juni 17 mwaka huu.
Wabunge
hao wa Chadema hawakuhudhuria kikao chochote cha Bunge kutokana na
kwenda mkoani Arusha kwa shughuli mbalimbali, kutokana na mlipuko wa
bomu uliotokea katika mkutano wao wa kuhitimisha kampeni zake za
uchaguzi mdogo wa udiwani katika viwanja vya Soweto, Juni 16 jijini
humo.
Malumbano
hayo yanatokana na Nchemba kuituhumu Chadema kuhusika na mlipuko huo,
Juni 20 mwaka huu wakati akichangia hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali ya
mwaka 2013/2014, akisema chama hicho kilipanga kulipua bomu hilo ili
kuwafanya Watanzania waamini kuwa Serikali ya CCM ndiyo inayohusika na
tukio hilo.
TUKIO LILIVYOANZA:- Wakati
Msigwa akiingia katika ukumbi huo akiwa ameongozana na Mbunge wa
Nyamagana (Chadema), Ezekiah Wenje, walikutana uso kwa uso na Nchemba
ambaye alikuwa akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Said Amour
Arfi.
Baada ya Nchemba kumwona Msigwa alimkaribisha mchungaji huyo akisema; “Karibu sana bwana, salama lakini?”
Hata
hivyo, badala ya kujibu salamu hiyo ya Nchemba, Msigwa alikuja juu na
kumtuhumu Nchemba kwamba anatoa kauli zinazoweza kuvuruga amani ya nchi.
“Wewe
ni mtu hatari sana, haya yote yanasababishwa na wewe, mnatumia damu za
watu kutafuta madaraka,” alisema Msigwa akimtupia maneno Mwigulu.
Baada ya kauli hiyo Nchemba alihoji akisema: “Ki-vipi? Hayo mambo tuyaache, Msigwa achana na haya mambo!”
Baada
ya Nchemba ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM kujibu, Msigwa
alimsogelea karibu na kumnyooshea kidole, huku akiendelea kumtuhumu kuwa
ana siasa chafu zinazopandikiza chuki kwa jamii.
Malumbano
hayo pia yaliingiliwa na Mbunge wa Musoma Mjini (Chadema), Vicent
Nyerere ambaye alimuunga mkono Msigwa, huku akimtuhumu Nchemba kuwa ni
mtu mbaya katika siasa za Tanzania. Katika kile kilichoonekana kutaka
kuweka mambo sawa, Wenje alimvuta Msigwa na kumpeleka ukumbini ili
kuepusha shari baada ya wabunge hao kuzidi kurushiana maneno. Chanzo:-
www.mwananchi.co.tz
No comments:
Post a Comment